Habari za majukumu members, ngoja nielekee moja kwa moja kwenye kisa husika. Nimepanga chumba hapa moro, vyumba viwili vinavyofuata baada ya chumba changu ni vya mshikaji wangu ambaye ni mtoto wa mwenye nyumba anaishi hapo kwao na mkewe pamoja na mtoto wake mmoja.
Siku moja akaniambia twenzetu tukapige vyombo kidogo kuna kuna kitu nataka unisaidie. Basi tukaenda baa ya karibu na maskani, tukaagiza vinywaji na jamaa akafunguka kwamba anaomba ushauri kuhusu masahiba yanayomkuta akiwa chumbani na mke wake, anasema mkewe anamlalamikia sana kwa nini bado wanaishi kwenye nyumba ya wazazi wa mwanaume ( ingawa vyumba vya mbele vinawapangaji nikiwemo na mimi), mkewe anataka wahamie eneo lingine maana anavyoendelea kubaki hapo kwao eti yeye mumewe anaendelea kubakia kuwa mtoto wa mama. Akaendelea kuniambia kwamba eti mkewe anadai anachukia kila siku kwenda kula nyumba kubwa na familia ya mumewe.
Jamaa yangu huyo ni dereva wa mafuso anasema aliamuaga kuishi hapo kwao kwavile kwanza hapo halipi kodi zaid ya kuchangia umeme na maji, pili kupunguza masimango ya kwenda kuishi kwenye nyumba za kupanga, mimi binafsi nikamwambia anipe muda wa kutafakari ili nimpe ushauri wenye tija, nikaona itakuwa vyema kama nitapata mawazo yenu wadau ili wikiendi hii jamaa akirudi toka mkoani nikae nae nimpe ushauri sahihi kama kuishi nyumbani kwa wazazi wake akiwa pamoja na mkewe ni kweli anabaki kuwa mtoto wa mama au lah..