Ambassador
JF-Expert Member
- Jun 2, 2008
- 933
- 75
Ni rafiki yako wa karibu sana, mmeshibana kiasi cha kushea siri zenu hata za ndani. Wewe umeolewa na shoga yako hajaolewa.
Mara shoga yako anakueleza kuwa ana mpango wa kuzaa na anaomba mbegu toka kwa mme wako kwa njia ya test tube. Hayuko tayari kulala na shemejiye kutokana na jinsi mnavyoheshimiana na hadhani kama akipewa mbegu kwenye test tube italeta madhara yoyote katika mahusiano yenu. Yuko tayari kugharimia zoezi zima la utoaji na upandikizaji mbegu kwa kukushirikisha wewe. Vilevile yuko tayari kumtunza mtoto mwenyewe bila kuisumbua familia yenu kwani ana uwezo wa kufanya hivyo.
Kina dada wa JF, kama ni wewe utamkubalia? Wadau wengine, hii mnaionaje?