Wanawake acheni kuzaa na waume za watu ilihali waume zenu wapo

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Kulingana na kazi ninayofanya ya utatuzi wa migogoro ya kijamii nimepokea kesi nyingi za wanawake za watu kuzaa na wanaume wengine wakati waume zao wapo hai

Nimegundua wanawake wa watu wanapodate au kuchepuka na wanaume za watu huzaa nao pia na mbaya zaidi mwanamke humwambia mchepuko wake mtoto wake katika familia yao na mbaya zaidi anamwambie "Yule mwanao baba ake anampenda balaa"

Kesi nyingi wanawake waliopo kwenye ndoa wanazaa na michepuko na wanawake muda mwingne wanashindwa kutunza siri hujikuta anawaambia wanaweka mashoga wenzio

Mfano *Mama x alienda kupiga stories salon moja na stories ziliponoga akawaambia" Siyo wew tu mbona na mimi nimezaa na mchepuko wangu na mme wangu anampenda sana mwanangu na hii mimba nahisi kama siyo ya mchepuko ni bahati kwa sababu siku nanasa huu ujauzito nilikutana na mchepuko saa 2 asubuhi jioni nikakutana na mme wangu ,hii inanipa utata mbegu ya nani iliwahi"

Mwanamke mmoja salon kampelekea habari rafiki wa mme wa mwanamke x na habari zikafika kwa mwanaume

Fujo zikaanza mwanamke x akakataa katakata kuwa alisema hivyo walikuwa wanasimuliana kwenye filamu moja

Kesi ikatufikia nilipombana mwanamke chemba peke yetu na kumtunzia Siri akakubali na nikamwambia umefanya makosa sana kusema na kama upo kwenye ndoa hata mchepuko hapaswi kujua kuwa umezaa naye,hii itakuvunjia ndoa

Rai yangu wanawake wenzangu mliopo kwenye ndoa zaeni na waume zenu acheni kuzaa na michepuko kwa misifa au kisa unapendwa na mchepuko

Wengine wafanya hivo kama kisasi kwa waume zao,kumbukeni watoto unaozaa watatunzwa na kulelewa na mme wako ,akigundua kuna kitu hakipo sawa unawapa watoto wakati mgumu

Kwa maelezo hayo nimefanya utafiti mdogo nikagundua haya

1,Wanawake wa vijijini wanachepuka sana kuliko wa mjini

2. Wanawake ambao wapo nyumbani bila kujishughulisha wanachepuka zaidi

3. Wanawake walioolewa ndoa za mitala wanachepuka zaidi

4. Wanawake wanaotumia mitandao ya kijamii zaidi wanachepuka zaidi

5. Wanawake waliokatika ndoa yenye uchumi wa Kati wanachepuka na hasa na vijana wasio na mwelekeo

6. Wanawake single mothers hawachepuki sana ukilinganisha na walio kwenye ndoa

7. Wanawake waliohudhuria sekondari Kati ya kidato cha kwanza na cha nne wanachepuka zaidi kuliko msingi,six na chuo

8. Wanawake wenye makalio makubwa huchepuka zaidi

9. Wanawake weusi huchepuka zaidi

Asanteni
 
...nakubaliana na hoja ya kuwa wanawake wa vijijini wanachepuka Sana! Issue sijui Ni ulimbukeni,umaskini au malezi na wale form four failures' wa shule za kata nao mh!
 
Kwanza jua kwenye ndoa ndiko kuliko na changamoto kubwa kuliko mahali pengine popote.

Pili juwa wengi wameingia kwenye ndoa bila sababu na wengine wameingia kwenye ndoa na sababu ila isio ya msingi.

Tatu nafsi ya mwanadamu haina mwisho wa kuridhika, ikipata hiki itatamani kile ikipata kile itatamani hiki, hii imepelekea utatanishi sana kwenye ndoa pale mlengwa anapokutana na kitu tofauti na alichokitarajia.

Mwisho wa yote mwanamke ndie anayebeba mzigo wote kwa sababu matokeo huonekana kwake kuliko mwanaume.

Ukiona mwanamke amezaa na mtu na mwanaume nje hali yupo na mwanaume nyumbani juwa lawama za kwanza kabisa ni kwa mwanaume.
 
sitetei, lakini nataka nikufahamishe kuwa "ndoa za maskini zina amani kuliko vile unafikiri wewe"
Sawa ila starehe ya maskini ni ngono, kwa hio mwenye kauchumi kakunua pombe vilabuni na mboga kama samaki na kitimoto au nyama choma, mwenye ngo'ombe, ndizi, Kahawa, nanasi etc wanafaidi sana.
 
sawa ila starehe ya maskini ni ngono, kwa hio mwenye kauchumi kakunua pombe vilabuni na mboga kama samaki na kitimoto au nyama choma, mwenye ngo'ombe, ndizi, Kahawa, nanasi etc wanafaidi sana
umewahi kuwa maskini?
 
Wake za watu kuchepuka ni kweli, kuchepuka hadi kufikia kuzaa ni kweli zaidi
 
Hapo namba 1 nimekupata vizuri sana. Na shida nadhani ni umasikini.

Kuna siku nilienda mkoani hapo nikakuta kesi ya dada kutembea na mchungaji na kisha mumewe akajua mwanamke akawa mkali na mchungaji akisema kuna maono huyo mwanamke inabidi akakae kanisani ili kufukuza shetani anayeingia katika hiyo ndoa.

Ila sababu ni umasikini mchungaji anatumia sadaka na maombi feki kumhadaa mke wa mtu. Wanafamilia nao pande mbili zote wamekuwa kama misukule walirogwa.

Wanaona kabisa mwanaume anakosewa adabu na mkewe na anafanya umalaya na uhasi ila wanatoa macho na kutochangia chochote zaidi ya kumtazama yule mwanaume kwa macho ya huyu ni mchungaji usigombane nae sio vizuri.

Sasa yule mwanaume ukiomuona maisikini hadi anatia huruma. Ni wale vijana wa kijijini anaependa familia yake masikini na anapambana ili maisha yawe mazuri ila mkewe anamuangusha kupitia maswala ya imani na wana watoto wadogo.

Nikasema huyu kijana apate tu ujasiri tu achukue watoto awapeleke kwa bibi yao. Aondoke akatafute maisha mengine kimya kimya.
 
Back
Top Bottom