Kuzaa mapema sio kupata msaada/ suluhu za uzeeni

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
KUZAA MAPEMA SIO KUPATA MSAADA/SULUHU ZA UZEENI

Anaandika Robert Heriel,
Kionambali.

"Nazaa mapema ili nipate wakunisaidia uzeeni"
Hapo ataanza kupiga hesabu, "nikifikisha miaka 35 mtoto atakuwa na miaka 10, nikifikisha 45, mtoto wangu atakuwa na 20, hapo nguvu zitakuwa zinaanza kuyoyoma, lakini nitakuwa sinatabu na mtu. Nikifikisha 55, mtoto wangu kashakuwa dume la mbegu au jike la Simba. Hapo sitakosa miambili miambili"
Atameza mate, kisha atasema, kuzaa mapema Raha"

Nani kasema Ulimwengu huu kuna MTU yupo kwaajili yako? Ni Nani huyo?

Taikon Baada ya kufanya chunguzi zangu, ambazo kwa muda huu nazitolea hesabu, nimekaa na Bibi na Babu zangu wenye idadi ya kutosha na umri wa kutosha. Nimejifunza mengi Kutoka kwao, wamenipa uzoefu na mausia Yao. Na kila utakaponiona naandika ujue ni sehemu ndogo ya kile nilichokipata Kutoka kwao kisha kukifanyia uchunguzi wangu binafsi Kwa sababu zakuambiwa unachanganya na zakwako.
Hata hivi leo, haya niyasemayo Mimi Taikon, yasiwe sheria kwako Bali yapokee kisha ukayafanyie uchunguzi wako binafsi.

Kuzaa mapema kuna faida zake na hasara zake, hata hivyo hasara ni nyingi kuliko faida hasa Kwa Zama hizi za ubeberu. Faida kubwa ya kuzaa mapema ni kuyawahi majukumu mapema ya kuandaa kizazi chako, sasa unaweza kuwa unaandaa kizazi tegemezi na Maskini au unaweza kuandaa kizazi kinachojitegemea na chenye utajiri.

Lakini kuzaa mapema maana yake ni nini?
Kuzaa mapema ni kitendo cha kuyawahi majukumu ya Uzazi na ulezi Kabla ya maandalizi au yakujipanga.
Hii itahusisha;

I) suala la umri,
Ii) Hali ya uchumi, na
iii) Utayari.

Kwenye umri kutahusisha mambo ya Akili, hisia, maumbile, Roho n.k. Mtu anaweza akazaa mtoto Wakati Akili yake haijakomaa, au hisia zake bado zinamambo ya kitoto. Hali hii inaweza kuhatarisha malezi na makuzi ha mtoto atakayezaliwa.

Hali ya uchumi, itahusisha uwezo wa kujisimamia, kujitegemea na kutegemewa. Kabla ya kiumbe chochote hakijabeba mimba ni lazima factor ya kujimudu, kujitegemea na kutegemewa na kile kiumbe atakachokileta izingatiwe. Iwe ni ndege, wanyama au Samaki. Haiwezekani kiumbe kibebe mimba Kabla ya kujitegemea.
Kwa upande wa binadamu, ni lazima mtu aweze kujitegemea na awe na uwezo wa kujilisha, kujisimamia na uwezo wa kulisha na kusimamia familia atakayoianzisha.

Wazazi hutoa mafunzo Kwa Watoto wao, mafunzo ya kujidhibiti kitabia hasa zile tabia zenye nguvu lakini zenye matokeo hasi ndani ya jamii, mafunzo ya kufanya kazi na kuzalisha Mali, mafunzo ya kujilinda na maadui iwe wanyama, magonjwa au maadui Watu. Mafunzo ya kukabiliana na nyakati ngumu. Mafunzo ya uongozi na utawala ndani ya nyumba. Mtoto akishahitimu basi atakuwa tayari kuanzisha na kuleta Watoto Duniani.

Ukomavu kiumri wa Kiakili, kihisia na kimwili ukiaunganisha na kujitegemea kiuchumi na kujisimamia ndio italeta Nia na Utayari wa kuanzisha Familia.

Nia au Utayari wowote wa MTU kutaka kuzaa mtoto na kuanzisha familia Kabla ya ukomavu wa Kiakili, kihisia na kimaumbile, Kabla ya kuweza kujitegemea kiuchumi na kuweza kujisimamia na kutegemewa itachukulia kama Tamaa Mbaya ya kushindwa kujidhibiti kitabia.

Hauwezi ukazaa Mtoto alafu ukampeleka kwa Bibi au mjomba au Ndugu au MTU yeyote Wakati wewe ungali hai. Hiyo ni dalili ya ubinafsi na upunguani, au kukosa maadili na kuharakia mambo Kwa pupa.

Haijalishi Sisi Watoto wengi tumelelewa na kukulia Kwa Bibi au Ndugu Wakati wazazi wetu wapo hai, lakini ukweli thabiti wenye Dawa ya kuiponya jamii lazima usemwe. Huwezi ukazaa mapema ukategemea matokeo mazuri uzeeni. Zaidi Sana upo kwenye nafasi nzuri ya Kupata matokeo mabaya Zaidi.

Sababu pekee ya mtoto kulelewa na Ndugu au jamaa au Bibi(Mama yako) ni wewe Kupatwa na Mauti au Kufungwa Jela, hakuna zaidi ya hapo.

Kuzaa mapema ni ubinafsi wa kiwango cha juu ambao utaleta matokeo ambayo wengi yamewaumiza mioyo Yao. Mtoto wako atahitaji nafasi yako kama mzazi kwake, atahitaji Kupata upendo na malezi Kutoka Kwako.
Na kamwe hutoweza kuutoa Upendo na malezi Kwa mtoto uliyemzaa mapema na hiyo haitakuwa msaada na SULUHU njema nyakati za uzee wako.

Kutokomaa Kiakili, kimaumbile na kihisia inaweza kukufanya uonekane ulifanya uamuzi wa haraka/mapema kuzaa na hii itakufanya usijali Watoto hao.

Kuzaa mapema lazima kufanyike ndani ya familia ya Watu Wawili yaani Mwanamke na Mwanaume waliokatika nafasi Sawa zenye Utayari wa Kupata Watoto. Hii itafanya kila mmoja ndani ya familia kuona thamani ya mtoto ndani ya Familia. Kila kitu kitafanyika kwaajili ya kukuza Watoto kwaajili ya maandalizi Yao ya Maisha. Na sio kuwaandaa Watoto kwaajili ya Maisha yenu ya uzeeni.

Kuzaa mapema au Kwa haraka huchangia ndoa nyingi za siku hizi kuvunjika, Kwa sababu mmoja wa wanandoa anaweza kuwa alifanha uamuzi wa mapema na haraka Kabla ya Wakati wake kufika. Uteketeke wa Akili na hisia za mwanandoa mmoja kama haujakomaa kamwe hawezi kujali thamani ya kile walichokileta Duniani.

Haki za malezi ya Baba na mtoto hawatajali. Wao Watafikiri zaidi kuhusu matunzo ya chakula na mavazi na mambo mengine na hii itaonyesha wazi kabisa Watu hao walifanya uamuzi wa mapema katika kuwapata Watoto hao.

Ni muhimu, kuzaa ukiwa tayari umekomaa kiumri, upo vizuri kiuchumi yaani unaweza kujihudumia na kuwahudumia wanafamilia yako(MKE na watoto) na kuwa na Nia na utayari (huu utakuja automatically ukishakuwa na Sifa mbili za juu). Hii itakupa matokeo mazuri sio wewe tuu Bali Watoto wako, jamii yako na Ulimwengu Kwa ujumla.

Taikon Acha nipumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ukichelewa sana watoto wako watakuja kukuita babu badala ya baba.

Hiyo ni misemo tuu ya Watu wenye Akili ndogo.

Kuzaa mapema hakukufanyi usiitwe Babu.
Wapo wazee lakini Kwa namna walivyoyaishi Maisha Yao wanaafya njema na wanaonekana Vijana alafu kuna Watu wanamiaka 45 tuu lakini wanaonekana wazee.

Mtoto wako uliyemuandaa kuwa Bora hawezi kukuona Babu ikiwa umemuwekea mazingira wezeshi.
Lakini mtoto wako hata ungekuwa kijana Sana lakini kama hukumuwekea mazingira rafiki atakuona Mzee wake ni mjinga, msalaba, na mzigo WA misumari.
 
KUZAA MAPEMA SIO KUPATA
Kuzaa mapema kuna faida sana kuliko kuchelewa.ukijipanga vizuri ni bora uzae mapema.sio unastaafu au ni mfanyabiashara una 55 bado unasomesha hicho ni kitanzi bwana mdogo.mimi ni mhanga wa kuchelewa kuzaa hapa nilipo najuta sana.sio kwamba sitapata msaada lakini hata baada ya kustaafu natakiwa mafao yangu yatumike kuwasomesha wanangu.
 
Sijakataa suala la mtu kuitwa babu, hilo lipo tu kiuhalisia kulingana na wakati.

Pointi yangu kwako ni moja tu, unaposisitiza watu wachelewe kuzaa [japo hujasema wachelewe mpaka kufikia miaka mingapi] unajiweka kwenye mtego wa majukumu ya kulea wakati ambapo umri na nguvu vitakuwa vimekutupa mkono.

Lakini pia, muonekano wako kwa wanao utakuwa haufanani na ule wa baba kwa wanae, huu ndio uhalisia, bila kujali kama una uwezo wa kuwalea au vinginevyo, na sio hii story uliyotupigia hapa.
 
Sijakataa suala la mtu kuitwa babu, hilo lipo tu kiuhalisia kulingana na wakati.

Pointi yangu kwako ni moja tu, unaposisitiza watu wachelewe kuzaa [japo hujasema wachelewe mpaka kufikia miaka mingapi] unajiweka kwenye mtego wa majukumu ya kulea wakati ambapo umri na nguvu vitakuwa vimekutupa mkono, lakini pia muonekano wako kwa wanao utakuwa haufanani na ule wa baba kwa mwanae, huu ndio uhalisia, na sio hii story uliyotupigia hapa.

Sijasema Watu wachelewe kuzaa Mkuu.
Nmesema Watu wazae wakishakuwa wamekomaa Kiakili, hisia na kimaumbile, pili, wakishakuwa na uwezo wa kujitegemea, kujisimamia na kutegemewa, tatu, Utayari.

Hausikii Wanawake wakilalamika kuwa Watoto wametelekezwa?
Hunasikia maelfu ya kesi dunaini kuhusu matunzo ya Watoto.

Vipi kuhusu malezi ya Watoto?

Kuhusu muonekano Ipo kwenye ishu ya Umri Mkuu
 
Automatically unapodai kuzaa mapema sio suluhisho la jambo fulani, basi kinyume chake ndio, au vinginevyo hutaki kabisa watu wazae!.
 
Kuzaa mapema kuna faida sana kuliko kuchelewa.ukijipanga vizuri ni bora uzae mapema.sio unastaafu au ni mfanyabiashara una 55 bado unasomesha hicho ni kitanzi bwana mdogo.mimi ni mhanga wa kuchelewa kuzaa hapa nilipo najuta sana.sio kwamba sitapata msaada lakini hata baada ya kustaafu natakiwa mafao yangu yatumike kuwasomesha wanangu.

Mimi nimezungumzia kuzaa mapema, sinazungumzia kuchelewa kuzaa.
Jambo moja la hakika ni kuwa Matokeo ya kuzaa mapema na kuchelewa kuzaa yanafanana Kwa kiwango kikubwa.
 
Nachukizwa sana na wazazi wanao zaa ili waje wawe mizigo kwa watoto wao, wakati wanasahau kwamba wakati huo watoto wao watakua pia wana majukumu yao.
Kuzaa mapema ni jambo jema ili watoto wakuwe ukingali bado hauja chakaa.
Lakini pia ni wajibu wa mzazi kuandaa maisha yake ya uzeeni/kustaafu.
 
Umesema kweli Kabisa.
Sisi wazazi wa kiafrika wengi wetu tunazaa mapema sio Kwa lengo la kukuza Watoto vyema ili wajiandae Kwa Maisha Yao, hapana, bali tunazaa mapema ili tuwahi Kupata matunda ya kuzaa.

Unakuta Mzee anamiaka 55 lakini anamsumbua kijana wake wa miaka 28 ATI amtumie Pesa vinginevyo atamlaani.
Alafu huyo kijana kazi yenyewe anayoifanya utabaki mdomo wazi
 
Sijakataa suala la mtu kuitwa babu, hilo lipo tu kiuhalisia kulingana na wakati.

Pointi yangu kwako ni moja tu, unaposisitiza watu wachelewe kuzaa [japo hujasema wachelewe mpaka kufikia miaka mingapi] unajiweka kwenye mtego wa majukumu ya kulea wakati ambapo umri na nguvu vitakuwa vimekutupa mkono.

Lakini pia, muonekano wako kwa wanao utakuwa haufanani na ule wa baba kwa wanae, huu ndio uhalisia, bila kujali kama una uwezo wa kuwalea au vinginevyo, na sio hii story uliyotupigia hapa.
Mkuu jamaa pale mwanzo kaichambua dhana ya kuchelewa kuzaa, ila wengi wenu naona mmekomalia kwenye umri hamgusii uchumi na afya ya akili.

Mtu anaweza kua na 30 yrs lakini akili ya kitoto, kujisimamia yeye tu hawezi huyo anaachwa akue kwanza. Akizaa akiwa na akili hizo atatafsiriwa kama kazaa mapema.
 
Sio issue za msaada tu, ama suluhu uzeeni bali huathiri hadi issue za Population Growth. Now days increase in population is a big threat to nature.

Because, you have to understand this people consume vast amount of food, water, energy and area for shelter. That creates environmental catastrophe by pollute and add some waste materials in the environment.

We must understand an Exponential Population Growth and it's consequences.
 
Nachukizwa sana na wazazi wanao zaa ili waje wawe mizigo kwa watoto wao, wakati wanasahau kwamba wakati huo watoto wao watakua pia wana majukumu yao.
Kuzaa mapema ni jambo jema ili watoto wakuwe ukingali bado hauja chakaa.
Lakini pia ni wajibu wa mzazi kuandaa maisha yake ya uzeeni/kustaafu.
Wazazi wa kiafrika wana vituko sana...yaan ni anazaa kwa ajili ya kupata faida Fulani mbeleni kutoka kwa mtoto mweeh,
 
Back
Top Bottom