Rafiki kipenzi wa Dar Es Salaam

Rafiki kipenzi wa Dar Es Salaam

astalavista

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2014
Posts
261
Reaction score
304
Sallamu wakuu!!
Kwanza niweke wazi kwamba huu ni uzi wangu wa kwanza hapa Jf toka niwe mwanafamilia,japo nilikuwa nafuatilia kimya kimya kabla ya kujiunga.
______ _______ _______ _______
Tarehe 09/08/014
MBEYA
Nilikua ndio kwanza nimeshuka kwenye kituo cha mwanjelwa nikitokea vwawa wilayani Mbozi kuja mjini kwa dhamira kuu ya kushuhudia 'show' ya Kili pale city Pub lakini kabla sijachukua uelekeo katika eneo la tukio nikaona vema nipite kwenye mashine ya ATM(ni karibu na sehemu ya show) ili niweze ku 'boost' mfuko wangu.

Astalavista! Astalavista!
Nilisikia sauti ikiita jina langu lakini sikujali sana kwasababu mbili kubwa,Mosi mimi ni mgeni hapa mkoani Mbeya lakini sababu ya pili ni ule umati wa watu ambao ulikua unaelekea City Pub hivyo niliamini kulikua na Astalavista mwingine.

Astalavista!! Awamu hii liliitwa jina na kufuatia kushikwa bega'
Astalavista....(katika hali ya kutoamini macho yake)
Norah...,nilijikuta nataja jina lake pia..Tuliongea mengi kwa muda mfupi lakini kubwa ni pale aliponipa taarifa ya kutokuwepo duniani kwa mpenzi wangu wa Dar(sijisikii vizuri nikitaja jina hapa,naomba aleweke hivyo.)

WAY BACK...2010
MTWARA.
Nilikutana na Mpenzi wa Dar maeneo ya Bima ndani ya jengo la Internet Cafe,baada ya maelezo mengi na urafiki wa ghafla tulioutengeneza alinieleza anatokea Dar Es Salaam kaja Mtwara kusoma.Baada ya kumaliza kile kilichotupeleka pale akaniomba nimsindikize hosteli kwao maeneo ya 'India Kotazi' kitu ambacho kilikuja kuwa ndio maisha yangu ya kila siku kwenda hosteli hapo na ndio sababu kubwa ya mimi kufahamiana na Norah.

IN RELATION WITH....
Nina amini kabisa Mpenzi wa Dar alikua na mapenzi ya dhati na mimi japo kwa upande wangu nilimchukulia kama mtu wa kupita tu,lakini kwa mazingira hayo hayo niliweza kumfanya mpenzi wa Dar awafahamu baadhi ya ndugu na rafiki zangu.Niliweza kuwafahamu ndugu zake pia na walinipa heshima kubwa huku wakinitaka niwe huru kuwatembelea pale nyumbani kwao(Dar-kimara mavurunza)
Maisha yaliendelea
Tulifanya mengi
Tukapanga mengi pia.

LIKIZO/VURUGU ZA GESI
2013.
Mpenzi wa Dar alikua ndio anamalizia mitihani ya mwisho lakini hadi anapanda gari hatukuweza kuonana na wakati huo simu yangu haikuwa hewani na nilikua niko mbali na mji kukimbia dhahama ambalo lilitokea wakati ule.
Kwa upande wake pia alishindwa kutoka kwenda hata pale ninapoishi kwa kuhofia yale yale yaliyonikimbiza mimi.

Simu yake haikupatikana tena
Hata rafiki zake ambao aliwaacha chuo nao pia hawakuweza kumpata.

JUL 2013 KIMARA MAVURUNZA
Nafika kwa kina Mpenzi wa Dar na tumaini la kumwona au kupewa taarifa za wapi yupo kwa sasa.
Ni kinyume chake
Taarifa ni kwamba watu wale wameuza eneo lile na kuamishia makazi yao Kibaha Maili moja.
.
.
Nimeshindwa kuandika kila kitu wakuu naomba nihitimishe hivi:
kwa maelezo ya Norah,Mpenzi wa Dar alifariki wakati akiwa kwenye harakati za kujifungua(ujauzito wake niliufahamu kabla ya kuachana kule Mtwara na nilikua tayari kwa kuitwa baba)

KAMA KWELI KUNA MAISHA BAADA YA HAPA DUNIANI
BASI BAADHI YA MASWALI YANGU NITAPATA MAJIBU MAZURI TOKA KWAKE MWENYEWE.

Bye..
 
Pole kwa kufiwa ,ila kuna kitu sielewi hapo na Bongo movie hii,hao ndugu zake au rafiki zake uliotambulishwa nao hawakua hata na contact nae?au hata contact za wazee wake?
Au kwanini hata hakukutafuta kupitia hata rafiki na ndugu zako?
(Just curiosity)
 
Pole sana kwa mkasa wa kumpoteza mwenzi wako.
 
You don't sound original. You sound Mentor.

anyways, pole.
 
Last edited by a moderator:
Sijapenda ulivomuita mpenzi wa dar... ingawa umepangalia kifilamu...... haya kaka mkubwa Astalavistah
 
Maskini pole sana kama ni kweli.Na kama watu huwa hamna hata future nao kwanini uliamua kumpa mimba mdada wa watu?may be sasa hivi tungekuwepo nae
 
Pole kwa kufiwa ,ila kuna kitu sielewi hapo na Bongo movie hii,hao ndugu zake au rafiki zake uliotambulishwa nao hawakua hata na contact nae?au hata contact za wazee wake?
Au kwanini hata hakukutafuta kupitia hata rafiki na ndugu zako?
(Just curiosity)

stori ni ndefu mkuu,hayo uyasemayo na mengine mengi yapo lakini kwasababu zilizo nje ya uwezo wangu niliomba niishie pale.
 
Back
Top Bottom