Rafiki kipenzi wa Dar Es Salaam

Rafiki kipenzi wa Dar Es Salaam

Pole sana mkuu inauma sana kumpoteza mpenz wako huku sababu ukiwa niww hata kama ulikuwa haujazama kiviile
Sallamu wakuu!!
Kwanza niweke wazi kwamba huu ni uzi wangu wa kwanza hapa Jf toka niwe mwanafamilia,japo nilikuwa nafuatilia kimya kimya kabla ya kujiunga.
______ _______ _______ _______
Tarehe 09/08/014
MBEYA
Nilikua ndio kwanza nimeshuka kwenye kituo cha mwanjelwa nikitokea vwawa wilayani Mbozi kuja mjini kwa dhamira kuu ya kushuhudia 'show' ya Kili pale city Pub lakini kabla sijachukua uelekeo katika eneo la tukio nikaona vema nipite kwenye mashine ya ATM(ni karibu na sehemu ya show) ili niweze ku 'boost' mfuko wangu.

Astalavista! Astalavista!
Nilisikia sauti ikiita jina langu lakini sikujali sana kwasababu mbili kubwa,Mosi mimi ni mgeni hapa mkoani Mbeya lakini sababu ya pili ni ule umati wa watu ambao ulikua unaelekea City Pub hivyo niliamini kulikua na Astalavista mwingine.

Astalavista!! Awamu hii liliitwa jina na kufuatia kushikwa bega'
Astalavista....(katika hali ya kutoamini macho yake)
Norah...,nilijikuta nataja jina lake pia..Tuliongea mengi kwa muda mfupi lakini kubwa ni pale aliponipa taarifa ya kutokuwepo duniani kwa mpenzi wangu wa Dar(sijisikii vizuri nikitaja jina hapa,naomba aleweke hivyo.)

WAY BACK...2010
MTWARA.
Nilikutana na Mpenzi wa Dar maeneo ya Bima ndani ya jengo la Internet Cafe,baada ya maelezo mengi na urafiki wa ghafla tulioutengeneza alinieleza anatokea Dar Es Salaam kaja Mtwara kusoma.Baada ya kumaliza kile kilichotupeleka pale akaniomba nimsindikize hosteli kwao maeneo ya 'India Kotazi' kitu ambacho kilikuja kuwa ndio maisha yangu ya kila siku kwenda hosteli hapo na ndio sababu kubwa ya mimi kufahamiana na Norah.

IN RELATION WITH....
Nina amini kabisa Mpenzi wa Dar alikua na mapenzi ya dhati na mimi japo kwa upande wangu nilimchukulia kama mtu wa kupita tu,lakini kwa mazingira hayo hayo niliweza kumfanya mpenzi wa Dar awafahamu baadhi ya ndugu na rafiki zangu.Niliweza kuwafahamu ndugu zake pia na walinipa heshima kubwa huku wakinitaka niwe huru kuwatembelea pale nyumbani kwao(Dar-kimara mavurunza)
Maisha yaliendelea
Tulifanya mengi
Tukapanga mengi pia.

LIKIZO/VURUGU ZA GESI
2013.
Mpenzi wa Dar alikua ndio anamalizia mitihani ya mwisho lakini hadi anapanda gari hatukuweza kuonana na wakati huo simu yangu haikuwa hewani na nilikua niko mbali na mji kukimbia dhahama ambalo lilitokea wakati ule.
Kwa upande wake pia alishindwa kutoka kwenda hata pale ninapoishi kwa kuhofia yale yale yaliyonikimbiza mimi.

Simu yake haikupatikana tena
Hata rafiki zake ambao aliwaacha chuo nao pia hawakuweza kumpata.

JUL 2013 KIMARA MAVURUNZA
Nafika kwa kina Mpenzi wa Dar na tumaini la kumwona au kupewa taarifa za wapi yupo kwa sasa.
Ni kinyume chake
Taarifa ni kwamba watu wale wameuza eneo lile na kuamishia makazi yao Kibaha Maili moja.
.
.
Nimeshindwa kuandika kila kitu wakuu naomba nihitimishe hivi:
kwa maelezo ya Norah,Mpenzi wa Dar alifariki wakati akiwa kwenye harakati za kujifungua(ujauzito wake niliufahamu kabla ya kuachana kule Mtwara na nilikua tayari kwa kuitwa baba)

KAMA KWELI KUNA MAISHA BAADA YA HAPA DUNIANI
BASI BAADHI YA MASWALI YANGU NITAPATA MAJIBU MAZURI TOKA KWAKE MWENYEWE.

Bye..
 
Hii clip yako imenikumbusha ndoto nilioiota usiku wakuamkia leo,
nimemuota aliyekuwa mpenz wangu ambae nimeachana nae 2weeks ago amefariki,aisee niliumiaje!tena ukizingatia bado ananicall kila cku kuniomba msamaha turudiane.NILIJIKUTA NIMESTUKA TOKA USINGIZN NIKIWA NA MAUMIVU YA MOYO,ILIKUWA BADO KIDOGO NIM CALL ILA NIKAMPOTEZEA.INAUMA SANA AISEE
 
Hahaha, ni mento bwana. Ila moe namaanisha anajaribu kuwa wewe. Nina hakika kichwani yuko sawa.

mzima wewe? Natafuta zawadi.

Ahaha thanks for the appreciation. Kajitahidi ila kazidisha hisia kuliko kufikisha ujumbe.

Niambie zawadi ya nini nikusaidie??
 
Maskini pole sana kama ni kweli.Na kama watu huwa hamna hata future nao kwanini uliamua kumpa mimba mdada wa watu?may be sasa hivi tungekuwepo nae
Kwani moja ya matokeo ya free P wewe unadhani ni nini?
 
Hahaha, ni mento bwana. Ila moe namaanisha anajaribu kuwa wewe. Nina hakika kichwani yuko sawa.

mzima wewe? Natafuta zawadi.

Kama ni zawadi ya ushindi basi ntafute mimi...
 
mhm!! mbona kidogo haiingii akilini hii ati!! Asprin hii stori si inafanana sana na zile stori za Mentor vile au naota nini?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom