Wokovu si dini, wala si Jambo jipya.
Wokovu ni Kuuacha utu wa zamani (Matendo yasiyo mpendeza Mungu, mfano Ulevi, Uzinzi, Uongo, Uuaji, Wizi, Lugha mbaya n.k), na Kumrudia Mungu na kuanza kufanya yaliyo kadiri ya maelekezo ya Mungu.
Wokovu ni neema tuipatayo kwa njia YA IMANI KUPITIA YESU KRISTO WA NAZARETH.. Sasa Kama mtu Hamuamini Yesu Kristo wa Nazareth Basi ni wazi kuwa bado hujafikiwa/hujaipata Neema hii..
UAMUZI unabaki kwako Sasa, Kuifuata neema hii tuipatayo kwa njia ya imani kupitia KRISTO Bwana wetu au Kubakia huko uliko (Ambako wewe unaona kunakufaa).. Ukiichagua neema hii Sawa, Ukibaki Uliko Pia Sawa.
Kuipata neema hii na kuiishi kikamilifu kimwili na kiroho basi wewe unayo nafasi ya kuurithi ufalme wa Mungu, lakini kuipata na kuyarudia maovu au kutoiishi sawasawa (Yani nusu kwa Yesu nusu unafuataa matendo na tamaa za Mwilini) Basi ni wazi kuwa huna nafasi katika ufalme wa Bwana, maana Mungu hapendi vuguvugu.. Chagua Sasa, Kuwa Moto au Baridi.
UAMUZI NI wako, njoo kwa Yesu au Ubaki huko uliko, Hakuna atakayekulazimisha.
Nisamehe Sana nimeandika mambo mengi, lakini yote ni katika kukuelezea juu ya wokovu/kuokoka... Sasa Basi naomba nitoe mjumuisho wa nilicho andika.
Ili uokoke, kwanza inakupasa kumuamini Mungu na Mwanaye Yesu Kristo ambaye kupitia huyo ndio utapata huo wokovu... Sasa Kama humwamini Kristo huwezi kuuamini wokovu.
Asante na Kwaheri.