Radio Industry: Wamiliki au wanaotaka kumiliki radion stations karibuni hapa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Radio Industry: Wamiliki au wanaotaka kumiliki radion stations karibuni hapa.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Radio Producer, Sep 10, 2012.

 1. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Wadau,

  Leo napenda kushare kuhusu soko la biashara ya radio nchini Tanzania. Kiukweli hili soko linazidi kushuka kila kuitwapo leo nakuzifanya radio nyingi zishindwe kabisa kusonga mbele au kujiendesha. Nimeshuhudia radio mbili mkoa fulani hapa TZ zikiwa katika hali mbaya na zinaweza kufa muda wowote.

  Mambo yanayosababisha kushuka kwa soko hili ni:-

  1. Kuongezeka kwa radio stations Tanzania.
  2. Uhuru au utandawazi kuongezeka. Mfano badala ya mtu kupeleka tangazo lake radioni anaweka facebook au JF na linawafikia watu wengi tu.
  3. Kukosekana kwa elimu ya masoko katika radios na kukosekana kwa ubunifu.
  N.K

  Ukweli uko hivi tatizo kubwa ambalo linaleta hali hii ni wamiliki wa radio kushindwa kutambua soko la radio Tanzania.
  Radio nyingi zilizo mikoa ya kanda ya ziwa, kati na kaskazini zina nafasi kubwa sana ya kuimarisha masoko yao.
  Kikubwa kabisa mafunzo yanahitajika, masoko ya radio ni tofauti na masoko ya nafaka. Hapa unahitaji elimu ya kutosha na ya kuendana na taaluma hiyo. Mfano ili radio ijiimarishe kiuchumi ni lazima maeneo yafuatayo yaimarike:-

  1. Programming (Mfumo mzima wa vipindi kwani ndo vitakusanya wasikilizaji na radio yenye wasikilizaji wengi inamshawishi sana mteja kuleta matangazo yake) Hapa yanahitajika mafunzo maalum.

  2. Wafanyakazi (Katika dunia hii ya leo unahitaji wafanyakazi wabunifu si tu wenye elimu kubwa hapana, wenye uwezo wa kubuni vitu vipya na kufuata vision ya radio basi mambo yatakunyokea)

  3. Productions (Ni lazima radio yako iandae vipindi vinavyoendana na matakwa ya wasikilizaji)

  4. Technical (Ufundi pia katika radio lazima uzingatiwe maana ukiwa sifuri badala ya kupata pesa na kuitumia kwa mambo mengine zinaishia kutengeneza vifaa vya radio tu)

  5. Marketing (hili somo ni tamu sana na ni pana na ndiyo KEY pointi ya kuongeza kipato cha radio yako)

  Tunaweza kutoa huduma hizi kwa urahisi:-
  1. Kutoa mafunzo ya marketing
  2. Unaweza kutupa tender hata ya miezi kadhaa kukusaidia radio yako iingie kwenye ushindani wa soko.
  3. Consultancy yote inayohusiana na radio including uuzaji wa vifaa, uanshaji wa radio n.k

  niPM kwa maelezo zaidi.
   
 2. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Radio hata kama zikiwa nyingi kiasi gani katika mkoa uliopo inaweza kujiendesha na ikakupatia faida nzuri tu, cha msingi IFANYE IWE NA USHINDANI.
   
 3. Jaslaws

  Jaslaws JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 5,129
  Likes Received: 2,186
  Trophy Points: 280
  Sijaelewa hapa "sababu inayofanya kupungua kwa radio stations ni kuongezeka kwa vituo vya radio??
   
 4. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Mkuu, ni kuongezeka kwa radio stations kunasababisha kupungua kwa soko la biashara ya radio. Radio zinakuwa na vipato visivyokidhi mahitaji kwa lugha rahisi hasara!
   
 5. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Radio siku zote huwa ni wasikilizaji, ukishindwa kuzingatia hilo basi! Ukiwa na wasikilizaji wengi hata matangazo mengi utayapata.
   
Loading...