MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,643
- 33,439
Wakuu,
Kama mnavyojua JF ni kisemeo chetu na imesaidia kuleta mabadiliko mengi. Niliwahi kuanzisha uzi hapa kushauri radio za Kikatoliki na kupitia uzi ule kuna mabadiliko yamefanyika na moja wapo ni kurasa za mitandao ya kijamii ya radio Tumaini ku improve! Kasi bado ni ndogo kulinganisha na Radio Maria lakini kuna mwendo.
Leo nimeona nishauri mambo mengine kuboresha radio Tumaini. Kwasasa kuna kampeni ya kuchangia radio/TV Tumaini na nimesikiliza father Massenge akifafanua changamoto za uendeshaji hadi nikajisikia vibaya! Tujitahidi kuchangia kurahisisha uinjilishaji.
Lakini ni muhimu radio Tumaini wabadilike pamoja na vipindi vingi vizuri lakini bado wanafanya vipindi kama radio Tanzania! Hivi nani zama hizi anasikiliza vipindi vya salamu tena usiku? Nani anasikiliza ngoma za asili zama hizi? Hayo achieni idhaa ya Taifa wanaoishi kwa ruzuku.
Radio Tumaini kuna asilimia ya vipindi vya kijamii sio dini tu lakini kwa hizo asilimia ndogo fanyeni vipindi ambavyo hata idara yenu ya marketing wanaweza kutafuta sponsors.
Usiku watu wamelala kama hakuna mahubiri basi wekeni hata nyimbo za dini kuliko kutuma salamu mambo ambayo hata radio zingine walishaacha!Karistimatiki chini ya utume wa walei mnaweza kuwapa wafanye night shift itaongeza wasikilizaji.
Vipindi vya kijamii visivyo na tija ni mzigo tu bora iwe radio ya dini fully kuliko hivi! Sponsors zimejaa shule na vyuo vya ufundi sababu ya jinsi mnavyoendesha vipindi kizamani na hambadiliki.
Ushauri, Kanisa limejaa manguli wa kuendesha radio na social media kwa mafanikio mf Millard Ayo, Sebastian Maganga, Francis Chiza n.k. Waiteni muwape kazi ya kusikiliza na kuwashauri hasa uendeshaji wa vipindi vya kijamii na mitandao ya kijamii ili vivutie sponsors otherwise mtakuwa mnalipia leseni bure!
Nimemsikia Basil Mbakile kwenye habari, mtumieni vizuri kwenye maboresho ni fundi aliyefanya kwenye radio za kisasa ikiwemo East Radio na Tv.
Mwisho kwa waamini Wakatoliki, tujitahidi kuchangia media zetu kazi ya injili isonge mbele! Ni wajibu wetu.
Mwenye access na father Massenge Mkurugenzi wa Radio Tumaini amfikishie hii.
Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app