Racism ndani ya Call of Duty Black OPS 2

Racism ndani ya Call of Duty Black OPS 2

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Kilio cha majonzi kimeibuka katika jumuiya ya wachezaji wa Call of Duty baada ya kitendo cha kipuuzi na cha kibaguzi kufanyika ndani ya mchezo wa Black Ops 2.
images - 2025-12-17T124511.175.jpeg

Yaan kuna majamaa mapuuzi yaliobeba chuki za kijinga yakabadilisha mhusika maarufu wa ramani ya Tranzit, Gremlin, na kuweka sura ya George Floyd — jambo lililowaacha wachezaji wengi wakiwa na hasira, huzuni na mshtuko mkubwa.
1765964657983.jpg

George Floyd si mhusika wa mchezo. Ni alama ya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, ukatili wa polisi, na dhuluma kwa watu weusi duniani. Kumtumia kama chombo cha dhihaka katika video game ni jeraha jipya kwa familia yake, jamii ya watu weusi, na kila anayepinga chuki.
maxresdefault.jpg

Swali kubwa linaibuka: inawezekanaje kampuni ya mabilioni ya dola kama Activision kuruhusu mazingira yao ya michezo kutumiwa kueneza chuki ya wazi namna hii?
images - 2025-12-17T124451.911.jpeg

Mashuhuda wanasema baadhi ya wachezaji walilia walipoingia mtandaoni na kukutana na picha hiyo ya kuchukiza. Huu si “utani wa mtandaoni” — ni sumu ya kijamii.
images - 2025-12-17T124511.175.jpeg

Jamii ya michezo inapaswa kuwa salama, ya heshima na ya burudani, si uwanja wa majeraha ya kihisia.
 
Back
Top Bottom