Hapa hatuangalii suala la UZINZI pekee; Private life ya mtu ina mambo mengi yakiwemo kwa uchache amesoma nini na kwa kiwango gani; utajiri/umasikini wake ameupataje; udini au ukabila wake ni wa kiwango gani; anakamata vipi hasira, chuki, husda, wivu vinapomvaa; anapenda kwa kiwango gani nafsi yake, watu wengine (hasa wenye mawazo na misimamo huru). Vipi katika kutafuta MALI ana simile kidogo? anapenda kuambiwa yale tu anayotaka kuyasikia? n.k...Sisemi yupo aliyekamilika kwa yote haya ila kwa viwango vinavyoridhisha kidogo.