Quick Reminder: Ewe Shabiki wa Simba na Yanga punguza matarajio

Best Daddy

JF-Expert Member
Apr 2, 2019
759
1,280
Yakiwa yamebaki Masaa yasiyozidi therathini kwa Timu zetu za Kariakoo kurusha karata zao katika mashindano ya kimataifa, ghafla nazinduka usingizini baada ya kuyakumbuka maneno ya mzee mmoja mwenye busara aliyesema;

"SON, Football can kill you, A real death. Don't settle for less but lower your expectations"

Matarajio, Matarajio, Matarajio. Hayo matarajio makubwa uliyonayo. Je, yanaendana na ubora wa kikosi chako?

Hii ndiyo ile miezi ya Nongwa pale Jangwani. Why?, Tunaaminishwa tena na viongozi wetu kabisa, Yanga ni timu bora sana, like hakuna timu ya kuizuia. So kama mashabiki matarajio yetu yapo juu, Inafika wakati unawaza ubingwa kabisa. Mambo yakiwa tofauti ni disappointments na Vilio. Punguza matarajio wewe sio mkubwa kama unavyofikiri.

Hii ndiyo ile miezi ya manung'uniko pale msimbazi(Hawa jamaa hawana kelele sana kama wananchi). Naamini utakubaliana na mie, Simba linapokuja suala la kimataifa mentality yao ni kama Real Madrid, yaani ligi ya ndani anaweza kuwa wa kawaida ila kimataifa wana-spirit moja ya ajabu sana. Timu nyingi zina mengi ya kujifunza kutoka kwa Simba. Simba ikija kupata wachezaji bora, Nawaona fainali kabisa.

Sasa Simba yupo kwenye Kundi gumu sana maybe zaidi hata ya lile la Al-ahly na Vita. Raja si mwepesi hata kidogo(hata hapa kwa mkapa), Vipers atatupa pia mechi moja ngumu sana(Mark my words), Horoya si wepesi pia pale kwao. Nitakua mtu wa mwisho kuamini simba atapata 7+ points kwenye group lake. Punguza matarajio.

Ni vizuri ukawa positive kuhusu timu yako, pia kama shabiki unaweza tamba na timu yako ila ni vyema ukatengeza mazingira ya kuto-jidanganya(Jiambie ukweli). Otherwise, vile vilio vitarejea tena. Zile ngonjera za atuachie timu yetu....sijui hatumtaki huyu na yule tuzisikia sana.

Yaani Mnyama unafungwa na Raja unalia? Una-andamana? Wewe Mnyama wa wapi buana?

Mwanachiii. Punguza matarajio.

Nasema haya sababu najali. Tupunguze matarajio.

All in all, Kila lenye Kheri Mwananchi.
All the best, Mnyama.
 
Wakati Yanga inafanya usajili nyinyi mlikuwa mnazurura tu na kupiga Picha na Manzoki, Sasa kila mtu atavuna alichopanda.
 
kwahio imani yako uto yupo njia salama kama mleta uzi alivotahadhalisha kwamba vinyesi mnajiamini sana na kwamba hakuna mtu wa kuwazuia kwenye kundi lenu? Na unaamini makolo hawana kabisa kikosi cha kupambana na kuvuka kundi lao kisa hawakusajili vizuri si ndio uto? Ila kumbuka mbumbumbuni kumeongezeka
Chama
Phili
Ntibanzokinza
Baleke na wengine wazuri ambao hawakuwepo last czon, na unakumbuka wazi simba ile ya kina sako na kibu denga ilivowatoa kamasi bingwa mtetezi berkane na orlando pirates kwa kikosi kile tu, je uto huoni kama ngada fc wana advantage kuliko hata wewe? Ukiangalia hata bettings wamewapa makolo odds zinazokaribiana na za timu mwenyeji leo hii! Ila uto sioni hili, by the way tupunguze matarajio sana.
 
Kuna watu eti baada ya Vipers kufungwa 5 na Raja casablanca jana basi eti wameshajihesabia wana points zao sita toka kwa vipers. Lol.
Kwani wao wamesahau walivyokuwa wanapigwa hamsa na jamaa za Kinshasa na Cairo?

Kilichowakuta Vipers ni karibu Mgeni, Sasa wamekaribishwa rasmi ligi ya makundi, na ile timu ni ukanda mwingine, lakini mechi yao na Simba ni ya kawaida sana kwao kwani ni ukanda mmoja timu zote mbili kila timu INA uwezo wa kupata matokeo iwe Kampala au Dar es salaam.
 
Wakati Yanga inafanya usajili nyinyi mlikuwa mnazurura tu na kupiga Picha na Manzoki, Sasa kila mtu atavuna alichopanda.
Yanga yupo safe group. Ila kile alichopanda bado hakiridhishi hata kidogo. Punguza matarajio.
 
kwahio imani yako uto yupo njia salama kama mleta uzi alivotahadhalisha kwamba vinyesi mnajiamini sana na kwamba hakuna mtu wa kuwazuia kwenye kundi lenu? Na unaamini makolo hawana kabisa kikosi cha kupambana na kuvuka kundi lao kisa hawakusajili vizuri si ndio uto? Ila kumbuka mbumbumbuni kumeongezeka
Chama
Phili
Ntibanzokinza
Baleke na wengine wazuri ambao hawakuwepo last czon, na unakumbuka wazi simba ile ya kina sako na kibu denga ilivowatoa kamasi bingwa mtetezi berkane na orlando pirates kwa kikosi kile tu, je uto huoni kama ngada fc wana advantage kuliko hata wewe? Ukiangalia hata bettings wamewapa makolo odds zinazokaribiana na za timu mwenyeji leo hii! Ila uto sioni hili, by the way tupunguze matarajio sana.
Tupunguze matarajio.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom