tawijeusi
Member
- Mar 10, 2021
- 49
- 45
SEHEMU YA 90
Ninahisi hivyo kwani tukio hilo
limetokea baada tu ya kitabu hicho
kutoweka” akajibu Marcelo
“ Unamfahamu mtu mwenye hizo
namba alizokupa baba yako ? akauliza
tena Austin
“ Hapana simfahamu”
Austin na Ernest wakatazamana
kisha Austin akasema
“ Suala hili linaonekana si suala
dogo.Ninasita kujiingiza huko kwa sababu
tayari kuna masuala mazito
yanayotukabili.Kwa kuwa tayari suala hili
liko katika mikono ya polisi basi hatuna
budi kuwaacha waendelee na uchunguzi”
akasema Austin
“ Uko sahihi Austin.Nitaweka mkazo
pia kwa jeshi la polisi wahakikishe
wanawasaka na kuwapata watu hao
waliotaka kukuua.Kwa sasa hadi hapo
tutakapopata maelekezo mengine toka
kwa David Zumo utaendelea kukaa hapa
pamoja na Austin.Hii ni sehemu salama
sana kwako kwa sasa.Utafuata yale yote
utakayoelekezwa na Austin”
“ Ahsante mheshimiwa rais.Mungu
awabariki sana” akasema Marcelo.Ernest
na Austin wakatoka mle chumbani
“ Suala la Dr Marcelo linaonekana ni
suala tata sana.David zumo ameingiaje
katika suala hili? Hicho kitabu alichopewa
na baba yake kina nini ndani yake?
Maswali haya yanalifanya jambo hili kuwa
gumu” akasema Ernest
“ Ni kweli mheshimiwa rais.Suala hili
linaoneana si suala jepesi.Ni suala pana
.Lazima kuna kitu kimejificha hapa na
ndiyo maana Marcelo anataka
kuuawa.Nahisi labda yawezekana ukawa
ni mtandao wa mambo haramu kama vile
madawa ya kulevya n.k Lakini hata mimi
uhusika wa David Zumo katika jambo hili
unanila akili sana.Anamfahamu Marcelo
lakini
Marcelo
hamfahamu
David.Inakanganya kidogo.Mheshimiwa
rais naomba tusiumize vichwa vyetu kwa
suala hili.Tuwaachie jeshi la polisi
watafanya uchunguzi wao na kupata
ukweli” akasema Austin wakaagana Ernest
akaondoka.
********************
Wakati rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Ernest Mkasa
akiondoka katika nyumba anayoishi
Austin,ukumbi mmoja mdogo wenye
kuweza kuchukua watu zaidi ya hamsini
uliopo ndani ya jumba moja kubwa la
kifahari lililoko kandoni mwa bahari
,kikao kizito kilikuwa kinafanyika
kilichowakutanisha watu zaidi ya
arobaini.Katika ukumbi huo kulikuwa na
luninga nne kubwa ambazo kulikuwa na
watu wakionekana waliokuwa nje ya nchi
wakiunganana wenzao wa hapa Tanzania
katika kikao kile.Kikao kile kilihudhuriwa
na makamu wa rais wa Tanzania,waziri
mkuu aliyevuliwa madaraka pamoja na
baadhi ya viongozi na wafanya biashara
wakubwa ambao ni wajumbe wa kamati
kuu ya Alberto’s Tanzania.
“ Kabla ya kiongozi wa kikao
kuwasili kulikuwa na minong’ono ya hapa
na pale na wajumbe wakijadiliana hili na
lile.Kiongozi wa kikao kile aliyevaa suti
nyeusi mfanya biashara tajiri mtanzania
mwenye asili ya Ghana,Obi Ochukwu
akatokea akiwa ameongozana na wajumbe