QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

subilia mkuu naweka mambo sawa hapa .mzigo upo wa kutoshaa mwanzo mwisho ni mwendo wa bandika bandua mpaka kuchee.

manina wwe jamaaa nakuelewa mnoooo aiseeee
najuta kwanini nilichelewa kuyajua haya mabandiko yko ..nili ifuatilia mnooo PENIELA BUT alivyokuja kufa jaji elibarick siku taka tena kuisoma niliona kuwa muandishi hakumtendea haki yule Jamaa hakustahiki kifo kwa sabbu yeye ndiye aliyeuanzisha ule ufukunyuku wa udukuzi ..
 
Asipokubali Monica hii hadithi itakua haijasadiki kwa mabinti wa Kitanzani

Make familia nzima inawazaga tuuu mtu mwenye hela
hahaha wewe huoni ameshahamisha fikra zake kwa raisi ..yaani hata yule doctor ameacha kumfikiria kwa muda ..Manina wallahi
kwann sijazaliwa na bakhresa mimi ?? hahaa
 
Duh marcelo hakutendewa haki jamani ndo ilibid ammiliki Monica afu Daniel bhana sikujua special mission yake huko TISS ilikuwa nn nafurah amarachi alimpata Austin coz they match aisee then Ernest amekufa Kizembe sana aidha reward yake baada ya kuitokomeza Alberto had to be huge afu duh ule mradi wa monica ndo angekabidhiwa Austin akaanzia maisha Maskini Linda aliishia wapi afu ningepata raha Alberto mkuu angetokomezwa kabisa NAFIKIRIA KWA SAUTI WAKUU
 
Kongole kwako Mtunzi
QUEEN MONICA : FINAL SEASON
SEHEMU YA MWISHO

Saa kumi na moja za jioni dege la
kifahari la rais David Zumo likatua
katika uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere.David Zumo akalakiwa na rais
wa Zanzibar kisha wakaeleka moja kwa
moja ikulu.David Zumo alikuwa
ameongozana na Monica,Austin na
Amarachi bila kumsahau Job ambaye
walimkuta uwanja wa ndege
akiwasubiri.David Zumo aliomba
kuonana na rais wa Zanzibar kwa ajili
ya mazungumzo ya dharura yenye
umuhimu mkubwa.
“Mheshimiwa rais poleni sana kwa
matatizo makubwa
yaliyotokea.Tanzania na Congo ni nchi
ndugu na msiba wenu ni wetu
pia.Nimekuja mimi mwenyewe
kuwasilisha salamu za pole kutoka kwa
ndugu zenu wa Congo na pili
kuzungumza nawe kuhusu mambo
kadhaa ya muhimu yanayoihusu nchi ya
Tanzania.Naomba mimi nisiwe
mzungumzaji ila nitamuomba Austin
azungumze badala yangu” akasema
David Zumo na rais wa Zanzibar
akamkaribisha Austin.
Austin alianza kwa
kuwatambulisha wenzake
job,Amarachi na Monica halafu
akamueleza rais wa Zanzibar historia
yake na mambo yote aliyopitia hadi
alipoitwa na rais Ernest na kumtaka
amfanyia kazi yake.Alimsimulia kuhusu
Alberto’s chimbuko lao na namna
walivyokita mizizi yao nchini
Tanzania.Alimueleza kila kitu hadi pale
walipokuwa wamefikia.Maelezo yale
yalimuacha rais wa Zanzibar na
mshangao mkubwa.
“Mheshimiwa rais” Austin
akasema
“Mheshimiwa rais David Zumo
aliamua kutusaidia kwa kuwatafutia
makazi akina Yasmin na familia yake
ambao wanakwenda kuanza maisha
mapya nchini Australia .Kabla
hawajaondoka Yasmin alituelekeza
mahala alikoificha hati ya muungano na
tukamtuma Job aliyebaki hapa dar es
salaam aende mahala hapo na
athibitishe kama kweli hati hiyo ipo na
akaipata.Job naomba umkabidhi
mheshimiwa rais hati hiyo” akasema
Austin na Job akamkabidhi
mheshimiwa rais wa Zanzibar hati ile
ya muungabno akaifungua akaikagua
na kuhakikisha ni yenyewe.
“Mheshmiwa rais David
nimeishiwa maneno na sijui nizungume
nini kwa haya niliyoyasikia na
yaliyofanywa na hawa vijana.Nadhani
ninapaswa kumshirikisha pia jaji mkuu
wa Tanzania masuala haya mazito”
akasema rais wa Zanzibar na kuomba
jaji mkuu.Jaji mkuu akafika akaelezwa
kila kitu.Austin alimkabidhi pia kitabu
chenye orodha ya wauza dawa za
kulevya Tanzania vile vile akamkabidhi
na ile rekodi ya Irene aliyowarekodi
rais Ernest na Jenerali Lameck.
Pale pale bila kupoteza muda rais
wa Zanzibar akatangaza kumvua
madaraka mkuu wa majeshi na kuagiza
akamatwe mara moja.Rais pia
akawaomba Austin na wenzake
wakaonane naye kesho saa tano za
asubuhi ikulu.David Zumo na akina
Austin wakaondoka ikulu wakaelekea
nyumbani kwa wazazi wa Monica.Mara
tu baada ya kushuka garini mzee Ben
akamuwahi Austin akamuomba
wazungumze pembeni
“Austin nataka nitumie nafasi hii
kukupongeza binafsi kwa kazi kubwa
uliyoifanya.Sikuwa nikikufahamu wewe
ni nani na nini mchango wako kwa taifa
na baada ya kugundua umuhimu wako
nilijilaumu sana kwa kukuwazia
vibaya.Nilidhani ni mmoja wa wale
vijana ambao wanajaribu kuwa karibu
na Monica kwa malengo yao
binafsi.Hongera sana Austin.Hapa ni
nyumbani kwako unakaribishwa muda
wowote” akasema mzee Ben na Austin
akacheka kidogo
“Ahsante sana mzee ” akajibu
Austin kisha wakaelekea ndani.Wakati
maongezi yakiendelea Austin
akasimama na kusema
“Mheshimiwa rais David
Zumo,wazee wangu bwana na bi
Benedict mwamsole nimesimama kwa
heshima kubwa mbele yenu kwa ajili ya
jambo moja kubwa.Nyote mmesikia na
kufahamu mambo aliyoyafanya Ernest
Mkasa.Pamoja na mengi mabaya
aliyoyafanya lakini kuna jambo moja
kubwa amelifanya ambalo tunapaswa
kumpongeza nalo ni kuwaondoa
Alberto’s hapa nchini.Ingawa
hakutumia njia sahihi lakini
amewasafisha Alberto’s wote na nina
hakika hakuna tena Alberto’s hata
mmoja hapa nchini.Kwa hilo moja
kubwa alilolifanya kwa ajili ya nchi hii
anastahili pongezi za
kipekee.Tukiachana na hilo
nimesimama kwa heshima kubwa ili
kuwaomba wazee wetu mtumie fursa
hii kumueleza ukweli Monica
kuhusiana na Ernest Mkasa .Monica
anapaswa afahamu Ernest Mkasa ni
nani kwani ni haki yake kujua”
akasema Austin.Janet na mume wake
wakastuka na kutazamana.
“Wazee wangu,David Zumo bado
ana safari ya kurejea Congo kwa hiyo
tuokoeni muda.Tuweke mambo yote
wazi kwani jambo hili si siri tena kwani
sisi sote mtuonao hapa tunalifahamu
lakini hatujaweza kumwambia Monica
kwa sababu wenye jukumu hilo ni ninyi
wazazi wake kwa hiyo ingekuwa vyema
suala hili akaelezwa hapa mbele yetu ili
tunapoondoka hapa tuwe na uhakika
kwamba Monica tayari anaufahamu
ukweli”akasema Austin
Benedict mwamsole na mke wake
wakaomba watoke kidogo nje
wakajadiliane.Baada ya dakika tatu
wakarejea.Ben akasema
“Kama alivyosema Austin ni kwelu
kuna jambo ambalo Monica
hajafahamishwa na ni haki yake kulijua
ila hatukuwa tumepanga kumweleza
katika mazingira haya lakini kwa sasa
hatuna ujanja lazima afahamu ukweli.”
Akasema mzee Ben na kumfahamisha
Monica kwamba Ernest Mkasa alikuwa
ni baba yake mzazi.Monica alipigwa na
butwaa akabaki anawatazama wazazi
wake kwa zamu
“Mbona sikuelewi baba? Ni kitu
gani hiki unachonieleza? Akauliza
Monica
“Monica suala hili si suala rahisi
na ndiyo maan hata sisi wenyewe
tumeshindwa kukueleza .Ni suala gumu
hata kwetu sisi lakini ukweli ni
kwamba Ernest Mkasa ndiye baba yako
mzazi” akasema mzee Ben.Monica
akamtazama kwa hasira na kusema
“Kama Ernest ni baba yangu na
wewe ni nani?
“Monica sipati neno zuri la
kulielezea suala hili.Tunahitaji kupata
muda na utulivu wa kutosha ili
kulifafanua suala hili” akasema Ben na
Monica akamgeukia mama yake
“mama suala hili analolisema baba
ni la kweli? Akauliza Monica.
“Ni kweli Monica” akajibu mama
yake kwa sauti ndogo
“Oh my God !! akasema Monica na
kutoka mbio pale sebuleni akaelekea
chumbani kwake
“Let me handle this” akasema
Austin na kumfuata Monica ambaye
aliingia chumbani kwake na kujifungua.
“Open the door Monica its me
Austin” akasema Austin huku akigonga
mlango lakini Monica
hakufungua.Austin akasikia vitu
vikiangushwa na kutupwa mle
chumbani,akarejea sebuleni kwa
wazazi wa Monica na kuomba apatiwe
funguo ya akiba.Akaongozana na David
Zumo hadi chumbani kwa Monica
wakaufungua mlango wakaingia na
kumkuta Monica amekaa chini
akilia.David akamfuata
“Malaika wangu
imetosha.Nyamaza kulia” akasema
David huku akipiga magoti na
kumkumbatia akamfuta machozi
“David nimeumia sana kwa taarifa
hii.Kwa nini wananifanyia hivi?
akauliza Monca,akainua kichwa na
kukutanisha macho na Austin
“What are you doing here?Stay far
away from me!! Akafoka Monica
“What kind of a friend are you?
You knew about this and you didn’t tell
me?!!
“Monica samahani sana kwa kwa
hilo” akasema Austin
‘Sitaki kusikia kitu chochote toka
kwako Austin.Wewe ni sawa na hao
wazee walionificha jambo hili kwa
miaka hii yote na wananiambia wakati
Ernest amefariki dunia.Hata hivyo
Ernest hawezi kuwa baba yangu
kamwe.Nimewakosea nini wazazi
wangu kiasi cha kuniumiza namna hii??
Akauliza Monica
“Monica naomba nipe muda
nikueleze jambo muhimu..” akasema
Austin
“Austin sitaki kuiona sura yako
humu ndani.Toka na usijaribu kuwa
karibu yangu tena !! akafoka Monica
“Monica mpenzi ,mpe nafasi
Austin ajieleze.Punguza hasira.Jambo
hili limetustusa wote lakini tunapaswa
kuwa watulivu .Naomba umsikilize
Austin anachotaka
kukwambia”akasema David na
kumfanyia ishara Austin aendelee
“Nilitwa na rais Ernest Mkasa”
akasema Austin na Monica akainua
kichwa kumtazama na kumsikiliza
“Aliniambia kuwa amefahamishwa
kwamba wewe ni mwanae lakini hana
uhakika kama kweli wewe ni mwanae
kwa hiyo kazi anayotaka kunipa ni
kumsaidia kupata sampuli toka kwako
ambazo angeweza kuzitumia kwa ajili
ya kipimo cha vinasaba ili awe na
uhakika kama wewe ni mwanae.Siku ile
ulipokutana na rais kwa chakula cha
usiku tulikuwekea dawa ya usingizi
katika kinywaji na ukalala kisha mbele
ya rais tukachukua sampuli
zinazohitajika tukazipeleka maabara
kwa vipimo na majibu yakaonyesha
kwamba Ernest Mkasa ni baba
yako.Nilimpigia simu nikamtaarifu
kuhusu majibu yale lakini kwa bahati
mbaya sikuweza kumkabidhi ile ripoti
kwani tayari mimi na yeye tulikuwa
tumeingia katika mgogoro lakini
majibu hayo ninayo na
nitakukabidhi.Nadhani mpaka hapo
nitakuwa nimelijbu swali lako
ulilowahi kuniuliza kwamba kwa nini
kila utakachomuomba Ernest
anakupatia?Alifahamu wewe ni
mwanae na ndiyo maana kila
ulichokitakatoka kwake ulikipata.Hayo
ndiyo ninayofahamu kwa upande
wangu.Masuala mengine ni wazazi
wako ndio watakaokueleza.Ahsante
sana Monica kwa kila kitu.Wewe ni
sababu kubwa ya sisi
kufanikiwa.Ulijitoa kuhakikisha
kwamba tunafanikiwa.Mungu akipenda
tunaweza kuonana tena hapo siku za
usoni.” Akasema Austin halafu
akamfuata David Zumo
“Mheshimiwa rais ahsante sana
kwa msada wako mkubwa uliotusaidia
hadi tumefanikiwa kuimaliza salama
operesheni yetu.Pamoja na kuwa
katika wakati mgumu wa kuondokewa
na mkeo lakini bado umesimama nasi
na kuhakikisha nchi yetu inabaki
salama.Ni heshima kubwa sana kwangu
kufahamiana nawe.Ahsante sana
mheshimiwa rais” akasema Austin na
kumpa mkono David Zumo
“Hata mimi ni heshima kubwa
kwangu kukufahamu kijana shupavu
kama wewe .Naionea wivu Tanzania
kwa kuwa na vijana wenye ujasiri kama
wewe na wenzako.Kundi dogo
limepambana na kuiweka nchi yao
mbele na hatimaye mmefanikiwa
kuikomboa.Afrika nzima inastahili
kuwafahamu kwa uzalendo huu
mkubwa mlio nao.Nini mipango yako
baada ya kuimaliza operesheni hii?
Akauliza
“kazi yetu mimi na wenzangu
imekwisha na majukumu yaliyobaki
tumeyakabidhi kwa uongozi wa nchi
kwa hiyo sisi tunaendelea na maisha
yetu ya kawaida.Sifahamu nini
nitafanya lakini nataka nijaribu kwa
mara nyingine tena kuachana na kazi
hizi na kutafuta maisha mapya”
“Kutokana na umahiri
wako,nimefikiria kama utakuwa tayari
nikuajiri kama mkuu wa idara ya siri
ya ujasusi ninayotarajia
kuiunda.Unasemaje kuhusu hilo?
Akauliza David
“Ahsante sana mheshimiwa rais
kwa kuniamini lakini kwa sasa sihitaji
tena kufanya kazi hizi .Nataka kuanza
maisha mapya”
“Tafadhali Austin naomba
ulifikirie hilo suala na utakapokuwa
tayari utanijulisha” akasema David
wakaagana na Austin akaondoka
akaenda sebuleni wakagana na wazazi
wa Monica wakaondoka zao.
“Namuonea huruma sana
Monica.Alimchukia mno Ernest na hata
kutamka maneno makali dhidi yake
bila kujua kama ni baba yake mzazi”
akasema Amarachi
“Inauma sana lakini lazima
akubaliane na ukweli huo kwamba yule
ni baba yake hata kama alikuwa na
roho ya kikatili” akasema Austin halafu
akamgeukia Job
‘Job vipi kuhusu Mukasha?
Tunatakiwa tumkabidhi naye kwa
vyombo husika kwani naye ni mshirika
mkubwa wa Ernest”akasema Austin
“It’s too late.Mukasha tayari
ameondoka”
“Ameondoka?? Austin akauliza
“Ndiyo ameondoka.Nimemuacha
akaondoka.Mimi na yeye tulikuwa na
makubaliano kwamba akinisaidia
kumpata mwanangu Milleen basi na
mimi nitamsaidia kuondoka
nchini.Alitekeleza sehemu yake ya
makubaliano na nikafanikiwa kumpata
Millen hivyo ikanilazimu na mimi
nitekeleze sehemu yangu.Mchana wa
leo ameondoka nchini”akasema Job
“Ndugu zangu leo nina furaha ya
ajabu mno ambayo siwezi hata
kuieleza.Nimeonana tena na
mwanamngu Millen.Nawashukuruni
mno nyote kwa ushirikano wenu
mkubwa hadi nimelifanikisha
hili.Austin sina cha kukulipa kaka
yangu kwani bila wewe hadi sasa bado
ningeendelea kuishi maisha yale ya
uwenda wazimu.Wewe ndiye uliyekuja
kunitoa katika maisha yale kwa hiyo
nina deni kubwa la shukrani
kwako.Amaraci kwako sina cha
kusema.Umekuwa nami toka siku ya
kwanza niliyoyaanza maisha yale ya
ukichaa.Kwa miaka hii yote
umesimama nami na kuna nyakati
ulifanya hata mambo ya hatari kwa ajili
yangu.Nashukuruni sana nyote”
akasema Job
“Nini mipango yako mipya?
Utaendelea na kazi ya awali Austin
akauliza
“Hapana.Kwa sasa nataka kuishi
maisha mapya.I want to be a father to
my daughter.Ninataka kujikita zaidi
katika kilimo na ufugaji.Nitanunua
nyumba mpya nitakayoishi na
mwanangu Millen na nitafungua pia
mashamba makubwa” Akasema Job
‘What about her mother? Akauliza
Amarachi
“It’s over.Yule mwanamke hana
nafasi tena katika moyo wangu.Kitu
pekee nilichokuwa nakihitaji toka
kwake ni kumpata mwanangu na kwa
kuwa tayari nimempata sina haja naye
tena.Ila kuna kitu nataka mnishauri
ndugu zangu.Mnamuonaje Julieth
anaweza kunifaa? Akauliza Job
“What do you think? Austin
akamuuliza
“I think she’s good.Japokuwa bado
sijamfahamu vizuri ila ni mzuri na
kikubwa zaidi anaelewana sana na
Millen” akasema Job
“Job sisi hatuwezi kukushauri
chochote kuhusu suala hilo kwani ni
suala la ndani ya moyo wako.Kama
umeona Julieth anakufaa basi fungua
ukurasa mpya naye” akasema Austin
Kabla ya kuelekea nyumbani
wakapita kwanza hospitali kwa
Marcelo kumjulia hali mzee maboko
baba mzazi wa Irene ambaye Marcelo
alimpeleka pale ili kumuandaa kwa ajili
ya safari ya kuelekea Ujerumani siku
inayofuata kutibiwa.
Ilikuwa ni furaha kubwa kwa
Irene kuwaona tena akina Austin na
kuwashukuru kwa kumsaidia
kuwakomboa wazazi wake na sasa
familia yao iko salama.Austin na akina
Job wakarejea nyumbani
BAADA YA MIEZI SITA
Uwanja wa taifa ulifurika maelfu
ya watanzania waliokwenda
kushuhudiwa kuapishwa kwa rais
mpya wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dr.Hebron Donald mpare
aliyeibuka kidedea kwa kura nyingi
baada ya uchaguzi kufanyika kufuatia
kifo cha rais Ernest Mkasa.
Sherehe hizi zilihudhuriwa pia na
viongozi mbali mbali wa kimataifa na
miongoni mwao alikuwepo mfalme wa
kwanza wa Congo David Zumo
aliyeambatana na mke wake ambaye ni
malkia wa Congo Monica Benedict
mwamsole ambaye sasa anajulikana
kama Monica David Zumo.Walikuwepo
pia wawakilishi wa marais na mabalozi
mbali mbali walioziwakilisha nchi
zao.Katika jukwaa kuu la viongozi
walikuwepo pia wageni maalum wa
heshima walioalikwa kuhudhuria
sherehe zile ambao ni Austin January
akiwa na mke wake Amarachi
Austin,Job Israel akiwa na mke wake
Julieth Israel na hakusahaulika Dr
Marcelo Richard akiwa na mchumba
wake Irene maboko.
Sherehe za kumuapisha rais mpya
zilifana sana na kila mtu alizifurahia na
mwisho rais mpya akapewa fursa ya
kusalimia watanzania na kusema
machache
“Ndugu wageni waalikwa mabibi
na mabwana sipati maneno mazuri ya
kuwashukuruni nyote kwa kufika kwenu
katika tukio hili muhimu na la kihistoria
kwa nchi yetu.Itoshe tu kusema kwamba
Ahsanteni sana nyote kwa kufika”
‘Ndugu zangu watanzania siku ya
leo si siku yangu ya kutoa hotuba lakini
niruhusuni nitumie dakika hizi chache
kusema mambo machache
muhimu.Kwanza kabisa napenda
kuwashukuruni sana kwa kunichagua
kwa kura nyingi ili niwe rais wenu na
ninawaahidi nitawatumikia kwa nguvu
zangu zote na ninathubutu kusema
kwamba hamkukosea kuchagua”
uwanja wote ukalipuka kwa kelele za
kushangilia
“Miezi takribani sita sasa imepita
toka nchi yetu ilipokumbwa na giza nene
baada ya kutokea kwa tukio la
kusikitisha sana ambalo ni nadra sana
kutokea duniani.Tulipoteza karibu
viongozi wote wa juu.Tulimpoteza
rais,makamu wa rais, wabunge wote
.Tukio hili bado litaendelea kukaa katika
vichwa vyetu kwa miaka mingi ijayo
kutokana na uzito wake.Namshukuru
sana,makamu wa pili wa rais ambaye
pia ni rais wa Zanzibar na mwenyekiti
wa baraza la mapinduzi kwa
kutuongoza vyema katika pindi hiki cha
mpito hadi hii leo tunaposhuhudia
kuapishwa kwa rais mpya ambaye ni
mimi.Katika kipindi hiki cha mpito
mmekuwa mkishuhudia safisha safisha
kubwa.Kilichotokea miezi sita iliyopita
kimetupa mafunzo makubwa na
hatutaki kitu kama kile kitokee tena
nchini kwetu.Wote waliohusika na
mambo yale yote maovu tayari
wamefikishwa mbele ya sheria na
wengine tayari wamehukumiwa.Pamoja
na kazi kubwa aliyoifanya rais
aliyetuongoza kipindi cha mpito lakini
bado nitaendelea kusafisha na nitaanzia
pale alipoishia mwenzangu na
nitaendelea kusafisha hadi nihakikishe
nchi hii inakuwa safi kama ilivyoachwa
na waasisi wetu.Ninapenda nichukue
fursa hii kuwatambulisha kwenu watu
muhimu sana kwa taifa hili ambao
wengi wenu hamuwafahamu.Naomba
Austin January na wenzako msimame ili
watanzania wawafahamu”akasema rais
na akina Austin wakasimama
isipokuwa Monica aliyekuwa amekaa
pembeni ya David Zumo
“Vijana hawa waliosimama
mkawaona ni mashujaa wanaopaswa
kutambuliwa na kupewa heshima ya
pekee kabisa.Hawa ndio waliopambana
kufa na kupona kuhakikisha kwamba
wanawaondoa watu waliotaka
kutuharibia nchi yetu kwa kutuletea
tamaduni za kigeni.Vijana hawa
wamepambana kuhakikisha kwamba
nchi yetu inabaki salama na inabaki
moja kwani tayari hadi hati ya
muungano wetu ilikwisha tolewa ikulu
na kupewa watu wasioitakia mema nchi
hii.Haikuwa rahisi kwa vijana hawa
lakini walipambana kufa na kupona na
baadae wakisaidiwa na rais David zumo
walifanikiwa kushinda mapambano yao
na nchi yetu ikawa salama
tena.Tanzania itawaenzi na
kuwakumbuka daima Austin na
wenzako.
Nataka nitumie dakika hizi chache
kufikisha ujumbe kwa yale mataifa
makubwa kwamba Tanzania sisi tuna
tamaduni zetu na tunaomba
ziheshimiwe.Hatuhitaji tamaduni za
kigeni wala misaada yenye
mashart.Ninatoa onyo kwamba
taasisi,au nchi yoyote itakayothubutu
kutaka kuingilia mambo yetu ya ndani
na kutuletea taratibu za kigeni kama
vile mapenzi ya jinsi moja,utoaji mimba
n.k hatutasita kuchukua hatua kali na
za haraka sana za kuvunja mahusiano
na taifa hilo bila kujali ukubwa wake.
Kwenu watanzania
ninawakumbusha tuzienzi tamaduni
zetu tulizorithi toka kwa mababu zetu
kwa ajili yetu na vizazi
vyetu.Tusikumbatia tamaduni za kigeni
ambazo zitatuharibia kizazi
chetu.Nitakuwa mkali sana katika hilo.
Ndugu zangu maneno hayo
machache yanatosa kwa leo.
Ahsanteni sana na Mungu
awabariki
Watu wakamshangilia rais na
hakukuwa na shughuli nyingine
iliyokuwa inaendelea hapo uwanjani
hivyo wageni wote waalikwa
wakaelekea ikulu kulikoandaliwa
chakula maalum kwa ajili yao na akina
Austin wakapata nafasi ya kukutana
tena na Monica na David Zumo
“Nimefurahi sana kuonana nanyi
tena” Monica akawaambia akina Austin
“Hata sisi tumefurtahi sana
kuonana nanyi tena.kwanza hongereni
sana kwa kufunga ndoa ingawa
hamkutualika” akasema Austin na wote
wakaangua kicheko
“Mtatusamehe sana kwa kuwa
hatukujua wapi tungewapata kwani
mara ya mwisho tuliachana bila hata ya
kuagana vizuri.Kwa sasa mnaishi wapi
Austin?Unafanya kazi gani? Akauliza
Monica
“Kwanza kabisa mimi na Amarachi
tulifunga ndoa” akasema Austin
“Wow ! hongereni sana.Niliona
jambo hili mapema na nikakutaarifu
kwamba Amarachi ndiye mwanamke
anayekufaa” akasema Monica
“Kwa sasa tunaishi afrika
kusini..Tunalima matunda na tuna
kiwanda chetu cha kusindika mvinyo
unaouitwa Amarachi.Ni mvinyo mzuri
unapendwa sana na una soko kubwa
nchi za ulaya.Job yeye amewekeza
katika kilimo na ufugaji.Ana kiwanda
chake cha kutengeneza maziwa.Dr
Marcelo yeye bado yuko kwenye fani
yake ya udaktari na wana mipango ya
kufunga ndoa na Irene.Operesheni ile
imetusaidia tukakutana na wenzi wetu”
Akasema Austin na wote wakacheka
“Nimefurahi sana kuonana nanyi
tena.Karibuni sana Kinshasa.Mimi kwa
sasa ni malkia wa Congo naitwa Queen
Monica wa kwanza.Nitafurahi sana
endapo tukitoka hapa tutaongozana
wote kwenda Congo” Akasema Monica.
“Ahsante sana Monica lakini mimi
na mke wangu Amarachi tunaondoka
na ndege ya saa mbili za usiku kurejea
Afrika ya kusini.Tutapanga siku
nyinginetutakuja uwatembelea.Ahsante
sana Queen Monica kwa msaada wako
mkubwa kwani bila wewe hivi sasa
tusingekuwa na nchi inaitwa
Tanzania.Mungu akitujalia tukipata
mtoto wa kike tutamuita Monica kwa
heshima yako Queen Monica wa
kwanza.Inawezekana labda siku moja
naye akawa malkia” Akasema Austin na
wote wakacheka
TAMATI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kaeni mkao wa kula story nyingine toka kwa mtunzi yule yule aliyetunga peniela now kaja na kitu kiitwacho queen monica. kutana na kijana AUSTIN JANUARY mtanashati na jasusi hatari anafanya mambo makubwa sana.

ALBERTOS kundi hatari linalotaka kuitawala dunia limeingia pia tanzania
Mkuu Lege kimya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom