QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEM YA 5

“ Daniel is a snake.!! Hafai kabisa
Yule kijana kuwa hata na ukaribu na
Monica.Baada ya kugundua ukaribu wake
na Monica nilimfanyia uchunguzi
nikagundua kuwa ni kijana mshenzi
sana.Ana tabia chafu mno.Ana wanawake
karibu kila kona ya jiji.Anawabadilisha
wanawake kama nini sijui.Daniel hafai
hafai kabisa tena nina mpango wa
kumuonya Monica aache kabisa kuwa
karibu naye” akasema Bi Janet huku sura
yake ikionyesha wazi alikwisha anza
kukasirika
“ Dah ! sikuwa nikifahamu tabia zake
kama ni hizo.Anyway tuachane na hayo
mambo tutazungumza siku nyingine
nataka tujadili namna ya kuandaa sherehe
ya kumpongeza Monica kwa mafanikio
haya
makubwa
aliyoyapata.Hiki
walichokifanya The Face kumtaja kuwa
ndiye mwanamke mrembo zaidi afrika ni
suala kubwa hii ni bahati kubwa kwa
familia yetu kwa hiyo lazima tufanye
sherehe kubwa ya kumpongeza”
“ Sawa ben niachie mimi suala hilo
nitalishughulikia” akasema Bi Janet
*****************
Monica aliwasili katika jengo zilimo
ofisi zake.Ni jengo la ghorofa mbili
analolimiliki yeye mwenyewe.Kama ilivyo
kawaida yake akasalimiana na walinzi
wake baada ya kushuka garini pamoja na
baadhi ya wafanyakazi waliokuwa nje
kisha akaingia ndani.Mapokezi hakukuwa
na mtu akapanda moja kwa moja katika
ghorofa ya kwanza ambako kazi zote za
ubunifu hufanyikia hapo lakini hakukuwa
na mtu ila kompyuta karibu zote
zilikwisha washwa .Monica akashangazwa
kidogo kwa hali ile
“ Where is everyone? akajiuliza na
kuchukua simu akataka kupiga mara
akatokea Jesica mmoja wa wafanyakazi
aliyekuwa akihema kwa kasi..
“Madam ..!! akaita Jessica
“ Jessica kuna nini mbona hivyo?
“ Madam its Linah ..!! akasema
Jessica na kumstua Monica
“ Linah ?? amefanya nini? Akauliza
Monica kwa wasi wasi
“ Ameanguka ghafla .Twende
ukamuone..” akasema Jessica na kugeuka
akaanza kutembea haraka haraka Monica
akiwa nyuma yake
“ nini kimemtokea Linah? Akauliza
Monica lakini Jessica hakumjibu
kitu.Walipanda hadi katika ghorofa ya pili
kulikokuwa na ofisi ya Monica pamoja na
ukumbi mdogo wa mikutano.Jessica
akaufungua mlango wa ukumbi ule mdogo
wa mikutano kwa kasi akaingia
ndani,Monica naye aliyekuwa amkimfuata
nyuma akaingia kwa kasi na mara
akakutana na kitu ambacho hakuwa
amekitarajia..
“ Surprise !!!!... ikasikika sauti kubwa
toka kwa wafanyakazi waliokuwa
wamekaa katika mojawapo ya kona ya
ukumbi ule wakiwa na nyuso zenye furaha
.Linah msaidizi wa Monica alikuwa
amesimama mbeye yao akiwa na maua
huku akiwa na tabasamu zito
“ Oh my Gosh !!..akasema Monica
kwa mshangao ..Taratibu Linah
akamsogelea Monica na kumpa maua
“Congraturations queen of Africa”
akasema Linah .Kwa mara nyingine
Monica
akajikuta
akimwaga
machozi.Alikuwa
na
furaha
iliyopitiliza.Wafanyakazi
wake
walimpongeza kwa kutangazwa kwake
kuwa ndiye mrembo kuliko wote
afrika.Baada ya pongezi Monica akaomba
aongee machache
“ Thank you..!! akasema Monica na
kufuta machozi
“ Thank you so much for this
wonderfull surprise.Nimefurahi kupitiliza
na ndiyo maana mnaona machozi
yananitoka.Ahsanteni sana ndugu zangu”
akanyamaza akafuta machozi na
kuendelea
“ Hiki kilichotokea kwa mimi
kutangazwa kuwa mrembo kuliko wote
Afrika ni mafanikio ya juhudi
zenu.Nimeonekana mimi kwa sababu
ninyi ndio mlioniinua na kunifanya
nionekane kwa hiyo ushindi huu ni wa
kwenu ninyi.Mnatakiwa mjipongeze papo
hapo napenda kuwaasa kuwa tunatakiwa
kuongeza bidii ya kazi ili tufike mbali zaidi
ya hapa tulipofika.Tutakaa pamoja na
kujadili namna tutakavyoweza kuitumia
fursa hii iliyojitokeza lakini kwa sasa
tufungue shampeni na tugonganishe glasi
tutakieni heri na kupongezana kwa
mafanikio haya makubwa” akasema
Monica.Shampeni ikafunguliwa wote
wakashangilia halafu kila mmoja akaenda
kuendelea na kazi.Monica aliingia ofisini
kwake akajiegemeza kitini hakuwa na
hamu ya kufanya kazi yoyote.
“ Why me Lord? Katika wanawake
wote hawa wa afrika wenye uzuri
usioelezeka why me? Akajiuliza Monica
akainuka na kuanza kuzunguka zunguka
mle ofisini na mara siku ya mezani ikaita
akaunyanyua mkono wa simu
“ Hallow “ akasema
“ Madam kuna wageni wako hapa
mapokezi”
“ Ni akina nani?
“ Ni Mr Daniel na mwenzake”
“ Ok waruhusu waje moja kwa moja”
akasema Monica halafu kwa haraka
akaingia katika kijichumba kidogo
kilichomo ndani ya ofisi yake ambacho
hukitumia kujirembea akarekebisha poda
usoni na kutoka tayari kuwapokea wageni
wake.Baada ya dakika kama nne hivi
mlango ukagongwa akaruhusu mgongaji

 
kwa mwenye soft copy ya hiki kitabu, ikiwa kwa PDF itapendeza zaidi, naomba tuwasiliane maana mpangilio wa humu nimeshindwa kuuelewa kabisa, unatia uvivu kutafuta pages zenye mwendelezo wa stori
 
Najua nimechelewa ila nitarudi tu baadae kikubwa kabisa naomba kwanza Lege unihakikishie usalama wangu kuwa sitakuwa teja kwa simulizi zako.
 
Hii ni bonge ya story na inamafundisho pia... Ikulu ikipata kichaa si tu taifa liko hatarini Bali hata watuzungukao....mojawapo ya dhima ya mwandishi katika literature ni kuangalia jamii na ku bashiri au kutoa bunio ya mambo yajayo.... Kwanye PENIELA & QUEEN MONICA mwandishi amejikita ktk hujuma katika ofisi ya RAIS& SERIKALI kwa ujumla... Hii ni wake-up call kwa viongozi kuishi katika viapo vyao..na kutanguliza uzalendo na utaifa katika kila jambo..na kwa wananchi tuwaangalie viongozi wetu kwa jicho la tatu, tusikubali kila watuambialo bila kuchunguza.. Kwa kuwa we hiyo wao wako radhi nchi iteketee wao waneemeke.. ALBERTOS Kwa wingi wao bungeni na jinsi walivyokuwa watumika kupitisha mishwaada na sheria BUNGENI ni sawa na Wabunge wa CCM sasa bungeni wanavyotumika kupitisha mishwaada kandamizi na isiyo na tija kwa taifa hili..PONGEZI kwa Mwandishi na kwa LEGE & wenzake kwa kuileta
 

Similar Discussions

51 Reactions
Reply
Back
Top Bottom