Quality Mall inasikitisha, maduka mengi yamefungwa

menny terry

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
506
646
Habarini wadau,

Leo nilitembelea Quality Centre Mall kwa ajili ya manunuzi ya hapa na pale aisee nilicho kukuta kimenishtua sana. Ni miaka sijaenda pale hivyo picha niliyokuwa nayo ilikuwa ni ile ya enzi zile pakiwa pamoto balaaa! Hakika panasikitisha mno.

Vyoo ni vibovu, maduka mengi yamefungwa, jengo asilimia kubwa ni giza. Kwakweli hali ya Quality Centre Mall inasikitisha sana.
Kwa taarifa nilizopata nikuwa jengo liko sokoni linauzwa.
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
11,488
23,966
watanzania wenyewe walikuwa wanamlalamikia Manji alivyokuwa anatupiga kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, akaja jamaa na kuamua kusikiliza kilio cha watanzania na kumfix "gabachori", leo hii watanzania walewale wanalalama huku..
 

Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
12,626
11,311
Manji mwenyewe ambaye ni mmiliki kaitelekeza

Hiyo mali yote Manji aliyotumia kujenga hapo alichukua kutoka NSSF enzi ya Ramadhani Dau; sina hakika kama huo mkopo ulirudishwa. Kama haukurudishwa maana yake hiyo mali iliyopo hapo inaoza ni ya wafanyakazi waliowekeza makato ya mishahara yao hapo NSSF. Wafanyakazi hawapati mafao yao kwasababu ya ufisadi kama huu uliofanywa na Ramadhani Dau na rafiki yake CAG mstaafu ASSAD wakati huo akiwa Mwenyekiti wa AUDIT committee ya board ya NSSF!
 

Mayotte

Senior Member
Nov 19, 2021
160
404
Manji mwenyewe ambaye ni mmiliki kaitelekeza.

Nakumbuka mwaka 2012 hapo palikuwa patamu kuliko mliman city.

Kuna kijiwe cha bata kiliitwa savanah ilikuwa balaa sana weekend
Baasii usimalize kusemaa,kwani ukiendelea moyo wangu unauchomaa..
Story hiizi,Ndio mana unaona nimeshika tamaa..kama kifaranga aliekosa mamaa..
R.I.P Savanna Lounge we miss you..
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
11,609
15,201
Hiyo mali yote Manji aliyotumia kujenga hapo alichukua kutoka NSSF enzi ya Ramadhani Dau; sina hakka kama huo mkopo ulirudishwa. Kama haukurudishwa maana yake hiyo mali iliyopo hapo inaoza ni ya wafanyakazi waliowekeza makato ya mishahara yao hapo NSSF. Wafanyakazi hawapati mafao yao kwasababu ya ufisadi kama huu uliofanywa na Ramadhani Dau na rafiki yake CAG mstaafu ASSAD wakati huo akiwa Mwenyekiti wa AUDIT committee ya board ya NSSF!
Haya ndiyo mambo natakaga kuyasoma humu mkuu siyo zile ngonjera mara marehemu, mara tuliumizwa, mara unapigwa mwingi.

Kumbe hao hao wanavaa gauni alafu wanaibuka wamevaa suruali au kanzu aseee..!
 
5 Reactions
Reply
Top Bottom