Song il gok
JF-Expert Member
- Feb 23, 2015
- 878
- 939
Kampuni bora inayoongoza kwa biashara Tanzania, Quality Group Limited (QGL) inatangaza kuwa imekusudia kuanzisha viwanda viwili vikubwa na vya kipekee vya sukari nchini.
Ujenzi wa viwanda hivyo ni hatua ya kampuni kuunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania, Dk John P. Magufuli za kusisitiza ujenzi wa viwanda ambavyo vitatoa ajira kwa Watanzania na kufikia ndoto ya kujitegemea pamoja na kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo 2025.
Viwanda hivyo viwili vitajengwa katika maeneo tofauti ambayo ni Pemba kwa Zanzibar na Mkundi mkoani Morogoro, na tayari kampuni imeshapata eneo lenye ukubwa wa ekari 20,000 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hivyo.
Mara vitakapoanza uzalishaji, viwanda hivyo vitakuwa vikizalisha tani za ujazo 100,000 kwa mwaka, ambazo zitasaidia kumaliza tatizo la uhaba wa sukari nchini na ziada itauzwa katika mataifa yote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Sanjari na uzalishaji wa sukari, kampuni itakuwa ikizalisha ethanol na umeme ambao utaunganishwa kwenye gridi ya umeme wa taifa katika mikoa husika na kupunguza tatizo la umeme.
Katika kuanzisha mradi huu, QGL imeingia ubia na kampuni kubwa za kimataifa ambazo zina ujuzi na uzoefu katika medani za uzalishaji wa sukari, ethanol na umeme.
Wataalam hao kwa muda mrefu wamekuwa wakitumika kushauri na kusimamia miradi kama hiyo, kwenye mataifa waliyopo kuboresha kilimo cha miwa na hadi sasa wameweza kuanzisha miradi zaidi ya 300 ya uzalishaji sukari duniani kote.
Wakati miradi mingine ikichukua zaidi ya miaka mitano (5) kukamilika na kuanza uzalishaji, mradi huu utaanza Desemba 2016 na utakamilika na kuanza kazi mwaka 2018 kwa ushirikiano baina ya Quality Group Limited na taasisi za Serikali kama Wizara ya Kilimo, Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na wadau wengine wa ndani ya nchi.
Mradi huo utagharimu dola za Marekani milioni 10 (sh bilioni 21.5) kwa kila kiwanda unatarajiwa kuzalisha nafasi za ajira 5000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. Ajira hizo zitahusisha wakulima wa miwa wadogo, ambao watanufaika kwa kuuza miwa kwenye viwanda hivyo.
QGL ni kampuni ambayo imekuwa ikijihusisha na biashara mbalimbali na kuajiri watu kutoka mataifa zaidi ya 12. Kupitia miradi hiyo, QGL inatarajiwa kuwa mwajiri mkubwa nchini na Afrika kwa mwaka 2017.