Q-NET Company "biashara mtandao" ni utapeli unaoenea kwa kasi Tanzania. Serikali mko wapi?

Nami nilikuwa mpumbavu kama nyinyi mwanzoni. Mungu aliponipa nafasi ya kufanya utafiti hasa baada ya mwenzangu kujiunga Leo najuta kwanini sikujiunga mapema!!?

Siku IPO Mungu awatoe mawingu meusi yaliyozingira bongo zenu
Umejiunga kwenye utapeli subiri kulia
 
mimi kuna jamaa yangu mmoja aliniambia kuna fursa kesho twende ukasikilize, ila kwa vile mjini shule nikang'amua kuwa itakuwa ni moja ya hizi pyramids scheme maana mtu hawezi tu kuanza kukualika kwenye fursa yenye hela kizembe tu.

basi nikaenda mikocheni pale nafika nashangaa watu wanasalimiana good morning mchana, wakanieleza pale mambo meengi kweli kweli wakati naondoka nikawaahidi nitarudi :D:D:D:D

wakajua wamepata kichwa kumbe michezo hiyo naijua kitambo
Hahaha mimi pia niliwai kutana nao nikawasoma fasta nikaingia mitini
 
Mm nafikiri serikali iwapelekeni shule ili muachane na mawazo ya zamani, mjipange kuendana na ulimwengu wa Leo.

Net work ziko zaidi ya mia duniani. Hata huko zilikowahi pigwa marufuku nchi husika zilikuwa na mawazo ya zamani kama yenu. Leo hii nchi hizo ikiwemo India Q net inaendelea kwa mfano hadi Leo. Fanya tafiti.

Hii ni biashara kama biashara nyinginezo. Uvivu wa vijana wa Kitanzania kwanza wa kufikiri na kutendenda mnadhani mkiambiwa utapata ml.10 kwa mwezi basi nanyi mnaingia na akili za kuvuna kama ushirikina vile bila kujielekeza kupiga kazi.

Qi kampuni mama ya q net INA miaka zaidi ya 15, mafanikio ni mengi kuliko changamoto. Hii ni biashara.

Leo IPO Asia, ulaya, afrika nk. Watu wengi muno wanabadilika maisha yao kwa kila Mwaka. Biashara inalipa. Kama kuna wachache wasiobadilika, sababu zinaeleweka, uvivu, lengo la kujiunga na mengine. Hii ni biashara.

Kama biashara inakua kwa kasi basi inafanya vzr. Na mnaoandika negatively basi pengine ni washindani kwani biashara za mitandaoni ziko zaidi ya mia moja duniani.

Usidhani serikali haitambui uwepo wake. Naamini serikali inavyombo Vya kutosha Vya kujiridhisha.

Watu wanaobadilisha maisha ya q net kwa mfano, wanawashangaa. Na kuwahuzunikia kabisa. Mm nashauri Watanzania tujifunze kwenda kutafuta u kweli kwa tafiti nje ya google na jamii forum.
 
4f9b2655cb2bc87be1510fbd7ebc6cf2.jpg
 
Sasa kama bado mmefunga akili hiyo ni shida nyingine. Mm nimefanya kazi kubwa ya kizalendo kama mtanzania mwenzenu ninayeumizwa na umaskini wetu wa kiakili na kipato.

Mwenye macho...tazama
 
Jiunge Q net kwa mfano, ukiwa na akili ya kufanya kazi. Usijiunge Q net kwa akili ya kidesi na ufurimason. Kubali kuteseka kwa kujifunza sana. Kubali kukataliwa Mara nyingi. Hii ni biashara. Siku utawashangaza wengi pamoja na Hawa wanaoidiss mitandaoni. Lkn kuwa makini wengine ni washindani wanavutia upande wao kama forex nk
 
Tangulini MATAPELI WAKATANGAZWA KWENYE GAZETI KAMA HILO.. pitieni gazet la THECIZITEN la tarehe ya leo 30 may 2017. Mjionee ukweli kuhusu qnet.. WATANZANIA TUJIFUNZE KUPIMA MAMBO KWA FACTS na sio kukurupuka na kusikiliza kila opinions. Thanks.
QNet ni matapeli. Acha kutetea ujinga. Tangazo gazetini si linalipiwa tu. Na tapeli siku zote anacheza vizuri na sheria ukimfuatilia unakuta hakuna sheria aliyovunja.

Hawa QNet waliingia Tanzania toka 2004 enzi hizo wanaitwa Quest Net wakiwa wanauza biodisc (kipande cha glass wanachodai eti kina manufaa kibao ya kiafya).

Ni utapeli tu wa network marketing na pyramid scheme zenye product geresha ndani yake. Ila Watanzania wengi hawajui haya mambo na wanakuwa impressed na ndoto za kumiliki magari na kwenda nje ya nchi.

Nimesikitika kuona manetwork marketing mengi sasa hivi yanatarget watoto waliomaliza form six wakiingia chuo yanawakomba vibumu vyao.

Hawa ni watoto kibiashara maana hawajui lolote kuhusu biashara ndo wanakuja kudanganywa na hizi pyramid scheme zenye bidhaa-geresha ndani yake (aka network marketing companies).

QNet ni wabaya zaidi kutokana na pesa wanayotoza. Ila wako pia Forever Living Products (FLP), Oriflame, GNLD, Tianshi, D9 na Universal Plan B.
 
Acheni Muibiweee tuu yani Mnavyokazanaa Kujiunga hayo Maqnet ndo naona kilaa Watanzania Wa4 bhasi siku hizi Wa3 ni vichaaaa...!! Magu alegeze uzii jamanii...
 
mimi kuna jamaa yangu mmoja aliniambia kuna fursa kesho twende ukasikilize, ila kwa vile mjini shule nikang'amua kuwa itakuwa ni moja ya hizi pyramids scheme maana mtu hawezi tu kuanza kukualika kwenye fursa yenye hela kizembe tu.

basi nikaenda mikocheni pale nafika nashangaa watu wanasalimiana good morning mchana, wakanieleza pale mambo meengi kweli kweli wakati naondoka nikawaahidi nitarudi :D:D:D:D

wakajua wamepata kichwa kumbe michezo hiyo naijua kitambo
Nami nshaitwa kwenye semina, sasa hii salamu yao ilinipa ukakasi, "good morning" wakati ni saa tisa, nikaona haina uhalisia, na semina zao wanakupa dozi kidogo ukiwa na maswali wanakwambia hayo utajibiwa kesho!!!
 
Vyuma vikikaza sana ubongo huwa haushirikishwi sana kwenye kufanya maamuzi, hapo ndio jamaa kama Qnet hushika watu.
 
Mm siyo mtoto Mdogo wala mjinga. Keep your doubts, I keep money. Ok?
Raha yake utapeli wenu huwa haudumu ni suala la muda tu utalia mkishapewa semina mnakuwa kama machizi wa kuota utajiri baadae akiri itakurudi ukiwa ushachelewa.
 
Back
Top Bottom