Kuingia kwa majukwaa ya uuzaji wa mtandaoni ya China barani Afrika ni fursa mpya kwa biashara na uchumi

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,000
1,019
Na Ronald Mutie

VCG111175877098.jpg


Mwaka 2020 mwezi Mei, takriban tani 1.5 za kahawa ya Rwanda ziliuzwa ndani ya dakika moja tu wakati wa tukio la uuzaji wa moja kwa moja mtandaoni lililolenga kutangaza kahawa ya Rwanda kwenye soko na wateja wa China.

Uuzaji huo ulikuwa umeandaliwa na kampuni kubwa zaidi duniani ya mauzo ya mtandaoni Alibaba.

Mwaka 2018 Rwanda na Alibaba zilitia saini makubaliano ambayo yalifungua milango kwa wafanyabiashara wadogo barani Afrika kushiriki katika biashara ya kielektroniki kwa kupeleka bidhaa zao kwenye soko la China kupitia Jukwaa la Biashara la Kielektroniki la Dunia eWTP.

Ujio wa Alibaba barani Afrika wakati huo uliashiria mwanzo mpya wa ufanyaji biashara na kufungua fursa mpya kwa bidhaa za Afrika.

Na sasa kwa mara ya kwanza, kampuni nyingine kubwa ya kuuza bidhaa mtandaoni ya China JD.com ambayo ni mojawapo ya masoko yenye ushawishi mkubwa mtandaoni nchini China imekuja kutoa jukwaa hilo kwa Waafrika .

Kwa mujibu wa taarifa ya ubalozi wa Tanzania nchini China iliyosainiwa na balozi Mbelwa Kairuki hatua ya kuuza bidhaa hizo kwenye jukwaa hilo inafuatia makubaliano kati ya ubalozi huo na kampuni ya China ya Prestige inayoendesha jukwaa hilo.

Baadhi ya bidhaa ambazo zimechaguliwa kuuzwa kupitia jukwaa la biashara ya mtandaoni ni pamoja na madini na bidhaa za vyakula ambazo ni korosho, kahawa na chai.

Hatua hii mpya imekaribishwa na wadau wa bidhaa zinazolengwa.

Haika Kimaru anajishugulisha na biashara ya kukusanya korosho kutoka kwa wakulima wadogo na baadaye kuuza kwenye miji mingine kama vile Dar Es Salaam, Arusha na Dodoma.

Akiwa anatokea mkoa unaolima korosho kwa wingi anaona kuwa kuwepo na aina mpya ya soko kutasaidia kupanua mauzo ya zao hilo.

“Kuna wakati mwingine siuzi kabisa kwa mwezi mzima, lakini miezi mingine Napata oda za karibu kilo 200, hivyo kukiwa na soko la mtandaoni ambalo linalenga wateja wa China, mahitaji yataongezeka na nitapata oda zaidi za hapa na pia waagizaji”, anasema Kimaru.

Ni kweli, biashara ya mtandaoni nchini Tanzania bado iko katika hatua ya maendeleo, hata hivyo bila shaka ina uwezo wa kukua haraka.

Lakini kuingia kwa kampuni ya Jd.com nchini humo kutachochea hamu ya kampuni za ndani kujiunga kwenye mnyororo wa biashara.

Kupitia biashara ya mtandao, wafanyabiashara wanapata fursa ya kuuza na kuongeza mauzo ya bidhaa zao na kuwafanya wanunuzi kupata huduma kwa viwango vya kimataifa.

Manufaa ya kuwepo majukwaa makubwa kama vile Alibaba na Jd.com barani Afrika ni kwamba wafanya biashara watapata bei za kimataifa kwa bidhaa zao bila kujiweka kwenye hatari za kusafiri au vikwazo vingi.

Kwa mfano “Bei ya jumla ya kahawa ya Rwanda ikiuzwa mtandaoni nchini China ni ya juu ambayo ni kati ya asilimia 30% na 40% kuliko inayouzwa katika soko la jadi la Marekani na Ulaya. Hivyo ni soko lenye faida zaidi kwa wakulima na wafanyabiashara wa Rwanda,” anasema Mshauri wa Uchumi na Biashara katika ubalozi wa China nchini Rwanda Wang Jiaxin.

Kupenya kwa kasi kwa Mtandao kupitia simu katika muongo mmoja uliopita kwa kiasi kikubwa kulichangia ukuaji wa biashara ya mtandaoni barani Afrika.

Takwimu za shirika la Biashara la Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa Nigeria, Afrika Kusini na Kenya zinaongoza kwenye aina hiyo ya Biashara.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom