Fahamu Kuhusu Biashara ya Software na Programming

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,432
5,403
Habari za wakati huu,

Tujo katika karne ya 21 tukiwa tunaelekea kumaliza robo ya kwanza ya karne hii.Wakati karne hii inaanza kwa waliokuwepo tunakumbuka kamsemo maarufu kaliitwa Y2K najua kuna ambao mnakumbuka stori za mwisho wa dunia, kibwetere na kirusi cha Y2K na vinginevyo. Anyway Y2K sasa hivi tunajua maana yake. Kipindi kile huko bara amerika na ulaya kulikuwa na simulizi za maendeleo. Maendeleo ya Computer hasa ambapo vinara walikuwa ni Microsoft. Internet ilikuwa na umri mdogo bado na yahoo ndo ilikuwa habari ya mjini. Nakumbuka mitandao kama darhotwire ilikuwa maarufu miaka ya baada 2000 na internet cafe zilikuwa nyingi sana mijini. Watu walikuwa wanatumia flopy disk ukiwa na flash we mjanja. Siku hizi tunazungumzia habari za SSD ni miaka 20 tu imepita lakini tayari simu za mkononi zina storage capacity na processing power ambayo ni sawa na Pentium 1 ya kipindi hicho.Kwa kweli dunia inaenda kwa kasi. Nilikuwepo wakati haya yote yanatokea na kwa kweli nilikuwa mmoja kati vijana wachache ambao nilianza kumilika simu ya touch kipindi hicho zikiwa bado ni technolojia hafifu.

Hata hivyo leo sitaki kusimulia historia, nataka tujadili Fursa zilizopo katika technolojia.Katika safari yangu ya kutafuta maarifa nimebahatika kujifunza kuhusu teknolojia.Tena za aina tofauti na za kipekee. Moja katia ya eneo la teknolojia mbalo naona lina fursa na hazijatumika ipasavyo ni eneo la Programming katika upana wake. Bado wazazi hatujaona kama ni muhimu kuwafundisha watoto wetu Programming language angalau moja. Bado hata sisi wenyewe hatujaona umuhimu wa kujifunza programminga language angalau moja. Tusichokijua ni kwamba tutajikuta tunachelewe kama ambavyo tumekuwa tunachelewa. Programming knowledge kwa sasa hivi ni basic knowledge. Kama ambavyo ukienda kwenye vyuo vingi utakuta somo la Communication skills ni la wote au development studies basi nafikiri niwakati sasa wa kufanya somo la Computer Programming Skills liwe la wote.Ikiwezekana basi lifundishwe tangu ngazi za chini za elimu.

Sasa turudi kwenye Biashara. Moja kati ya biashara nyingi ambazo ni ndogo ambazo ninazifanya ni Biashara ya kutengeneza na kuuza mifumo ya Computer. Ndio natengeneza na kuuza mifumo ya aina mbalimba kama mifumo ya kiuhasibu, mifumo ya kusimamia biashara, michezo ya watoto, mifumo ya kufundisha watoto, mifumo ya kujifunza na kujisomea na kwa sasa hivi najifunza kutengeneza Operating Sytem ikiwezezekana niwe na ka operating system kangu kadogo tu kakuringishia washakaji hapa JF. Nakusudia kutumia Linux KERNEL kwa ajili ya hili lengo na Tayari nimeshajifunza 3% ya ufanyajai kazi wa Linux based systems ili niweze kutengeneza mfumo wenye TIJA. Lakini sio huko tu pia nimejifunza kuhusu PHP na Lugha nyingine za kutengeneza mifumo ya kompyuta kiasi kwamba naweza kusoma code na kuifanyia maboresha au mabadiliko kulinga na mahitaji yangu(Lazima nikiri kwamba Programming ni hobby tu ingawa nimeisomea na ninaifanyia kazi).

Ziko kampuni nyingi sana za kitanzanaia ambazo zinafanya vizuri katika eneo hili la ICT na wako programmers wengi wazuri lakini pia lazima tukubali kwamba bado hatuipa TEHAMA uzito unaostahili ambao unaweza kuifanya iwe biashara kamili na lengo langu katika uzi huu ni kujaribu kuwapa mwanga wa namna ya kutumia FURSA katika eneo hili kujenga utajiri. Ukitaka kuingia katika sekta hii unaweza kuingia katika maeneo au njia tatu:
  1. Unaweza kuingia kama msambazaji/muuzaji wa mifumo na huduma za Tehama
  2. Unaweza kuingia kama mshauri/muelekezaji.mkufunzi wa mifumo ya TEHAMA
  3. Unaweza kuingia kama mzalishaji/mtengenezaji wa mifumo ya TEHAMA.
Unaweza pia kujikita katika maeneo yote matatu kwa kutegemea uwezo wako wa kifedha na kitaaluma.Sasa nitaeleza kila eneo kwa kina ili uelewe na uone kama una msuli na ujasiri wa kuingia humo.

Usambazaji na UUzaji wa mifumo ya TEHAMA

Hapa unachohitaji ni kuwa na mtaji na uwezo wa kuuza.Unaweza fanya kama mtu binafsi au kampuni. Unaweza fanya kama muuzaji aliyeidhinishwa, Wakala au White label (Hati miliki huru) Unapokuwa muuzaji aliyeidhinishwa maana yake ni kwamba unakuwa ni wakala rasmi wa bidhaa au huduma fulani kwa makubaliano maalum na wamiliki wa mfumo husika. Unapotaka kuingia kama wakala wa whitelabel hapa unakuwa unatumia jina lako na kuwajibika kwa wateja wako kama mmiliki wa huduma ile ingawa sio mmiliki,Faida hapa ni kuwa unakuwa na control ya biashara.

Katika eneo hili la kuwa msambazaji unawekeza zaidi katika kujitangaza na kutafuta wateja. Wateja unaowapata wanakuwa wateja wako na faida inakuwa ni ya kwako. Baadhi ya huduma na bidhaa unazoweza kuwa msambazaji na muuzaji ni pamoja na.
  1. Huduma za kuhost websites,System mbalimbali, hapa kuna makampuni mengi sana ambayo hufanya kazi kwa ada ndogo ya leseni kiasi cha Shilingi za Kitanzania 100,000 kwa mwaka ili wakupatie mfumo wa kisasa wa kuuza kwa wateja wako.Mimi ninafanya kazi ya kusambaza zaidi ya mifumo 18 kwa gharama ndogo tu TZS 100,000 kwa mwaka kwa mifumo yote.Biashara hii nilianza zaidi ya miaka 9 iliyopita ambapo nimeweza kuingiza PESA kwa kuuza domain names,kuuza hosting space,kuuza Email services ikiwamo huduma za email za google, nimeweza kuuza mifumo ya cloud server kwa ajili ya kampuni mbalimbali.Hii ina maana kwamba mimi ninauza bidhaa na huduma za makampuni mbalimbali kama namecheap, godady, bluehost, hostgator, freenom, inmotion google, mailchimp, wordpress, etc. Sizalishi wala similiki hata program moja kati ya hizi bali kazi yangu ni kutafuta wateja na kuwauzia mifumo hii na kuwapa support pale wanapohitaji.
  2. Wordpress ni eneo ambalo napenda nilieleze kidgo kwani ni teknolojia ambayo imeniwezesha kutengeneza faida.Kwa wasiojua wordpress in CMS(content management system) ambayo iko wazi(Open source) kutumiwa na kuendelezwa na mtu mwingine yeyote yule.Uzuri wa wordpress ni kwamba inakuwezesha kutengeneza website ndani ya muda mfupi sana.Kwa mfano mimi kwa kutumia wordpress naweza kumpatia mteja website ndani ya masaa 24 yaani process ya kutengeneza website imekuwa fupi kwa sababu wordpress in themes na plugins nyingi zinazorahisisha sana kazi yangu hii. Kwa kutumia wordpress na uzoefu wangu wa php, html na css naweza kumpatia mteja website yenye mfumo wa kusimamia biashara yake kwa gharama nafuu sana na muda mfupi. Kwa kupitia wordpress peke yake ninaweza kutengenza faida ya hadi milioni 20 kwa mwaka na kutengenza mifumo yenye kiwango kikubwa cha ubora na hapo bado najifunza vitu vingi ili niongeze uwezo wangu
Kuna mengi katika eneo hili la usambazaji na uuzaji wa huduma za TEHAMA lakini kwa leo inatosha nikwambie tu kwamba eneo hili huhitaji mtaji Mkubwa. Kama Uko serious na una kiasi kidogo cha PESA ambapo mimi nitakuongoza katika kusajili kampuni yako, kupata leseni, Kupata mfumo wa kuuza bidhaa za TEHAMA. Mafunzo ya jinsi bidhaa zilivyo na zinavyotumika. Support ya kufanya malipo nje ya nchi maana bidhaa hizi nyingi ni za nje ya nchi.Kwa ufupi unaweza kutengeneza brand kubwa ya kibiashara kwa kutumia tu Wordpress platform bila tatizo. Mwisho wa andiko hili nitaweka mawasiliano zaidi kwa ajili ya huduma nyinginezo.

Eneno Pili ni kama mshauri(Consultant) wa masuala ya IT

Katika eneo hili unafanya kazi na pande zote yaani wazalishaji na wasambazaji na wateja. Wazazlishaji unawasaidia kuelewa soko linataka nini. Wateja unawasaidi kuchagua huduma bora.Kwa kawaida unakuwa na ujuzi pia wa kufundisha watumiaji na hata kuwa support pale inapobidi.Wewe unakuwa ni kiungo.Eneo hili linahitaji uwe na utaalamu na uelewa mpana wa masuala ya TEHAMA na ufahamu mabadiliko na mambo muhimu katika TEHAMA.

Mimi pia hufanya kazi kama Junior consultant. Kwa mfano tangu mwaka 2018 nimekuwa nikifanya lobying kuhusu vfd (Virtual Fiscal Devices) kama mbadala wa EFD nilifurahi sana huduma hii ilipoanza kuwa maarufu na TRA walipoachili developers watumie API zao kwa ajili ya kuunganisha mifumo yao na mfumo wa risiti wa TRA. Kwa sasa hivi nazungumza na watoa huduma wa hizi vfd juu ya maeneo ambayo wanapaswa kufanya maboresho ili kufanya mifumo yao iwe na TIJA zaidi na ninazungumza na wateja ila nao wahamie katika mifumo hii na kwa mara ya kwanza kabisa na mimi nimeanza kufikiria kuanza kutoa risiti za efd kwa wateja wangu ninao wahudumia na ninaamini kwamba soon nitafanikisha hili. Soon pia nitaanza kuwa msambazaji wa hii mifumo na ninawakaribisha watengenezaji wa mifumo hio ili tuweza kuona namna tunaweza fanya kazi pamoja kufikisha huduma hii kwa wateja.

Kuwa consultant katika eneo la ICT kunahitaji uwe na uelewa mpana sana na ukiweza unaweza jisajili ICT commision na ukachukua kabisa leseni ya biashara ya ICT consultant.Hii itakusaidia kujenga uaminifu kwa wateja na zaidi itakuwezesha kuwa na uwezo wa kufanya kazi na taasisi kubwa za kimataifa.

ENEO la TATU ni la UTENGENEZAJI wa mifumo ya TEHAMA

Hili eneo ni pana unawezankuingia kama mtengenzaji kwa kutumia mfumo wa outsourcing ambapo unatumia wataalam wa ICT na kuwalipa kwa mkataba maalum kulinga na aina ya mfumo unaohitaji.Uzuri wa kazi za ICT unaweza fanya ukiwa popote cha muhimu ni kufahamu ni mfumo na utaalmu wa aina gani unahitajika.ENEO hlili ni lazima uwe na mtaji mkubwa kwani linahusisha TRIAL and ERRORS nyingi na kama hujui nini unataka unaweza kuingia gharama kubwa kutengeneza mfumo ambao hauna TIJA.

Kazi ya kutengeneza mfumo ni kazi onayofanywa natimu ya watu wenye skills za aina mbalimbali na utaalamu tofauti.Mara nyingi program inavohitaji mambo mengi ndo na utaalamu unavozidi kuhitajika.Utahitaji wataalm wa kutengeneza UI,wataalamu wa Database,wataalamu wa Backend wataalam wa testing etc .Kuunda timu ya aina hiyo kuna hitaji wewe mwenyewe kuwa na utaalmu na uwezo wa kifedha.Lakini pia unaweza kuunda timu ya wataalamu wa kujitolea na mkatenga muda mchache kuutuumia kwa ajili ya mradi wenu na kisha kuukamilisha mkauingiza sokoni.Cha muhijmu ni nyie kuwa na skill zinazohitajika pamoja na utayari wa kufanya kazi pamoja.

Kama nilivoeleza hapo juu SEKTA ya TEHAMA BADO ina FURSA nyingi na unaweza kuzitumia hata kama kiwango chako cha ujuzi ni kidgo.Hivyo basi iwapo unahitaji usaidizi wa kuanzisha biashara katika eneo moja wapo katika sekta ya TEHAMA basi unaweza kuwasiliana nasi.Kumbuka kwamba Biashara za TEHAMA zinahitajika kila siku na kila mahali.Iwapo unahitaji kujiingiza katika biashara kwenye sekta ya TEHAMA unaweza kuwasiliana nasi ili tufanye kazi pamoja.

Iwapo unahitaji huduma ya usajili wa Majina ya biashara,kampuni au unahitaji ushauri juu ya namna bora ya kuendesha biashara yako ikiwamo biashara ya TEHAMA basi unaweza kupata huduma hizo kwa gharama nafuu.Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na:
  1. Kwanza tutakushauri kuhusu muundo wa biashara yako faida na hasara pamoja fursa mbalimbali
  2. Pili tutakufanyia utafiti na ushauri wa Jina la Biashara yako kwa kuzingatia vigezo vya SOKO
  3. Tutakufanyia Taratibu zote za usajili kuanzia Uandaaji wa Nyaraka Mpaka Kukamilika kwa Usajili pamoja na leseni
  4. Tutakuandikia Company Profile ya Kisasa kwa Lugha ya Kiingereza na Kiswahili
  5. Tutakutengenezea Website ya kisasa kwa ajili ya Biashara na huduma zako.
  6. Tutakutengenezea, Logo, Business Card,Letter Head pamoja na Nyaraka nyingine za Kibiashara
  7. Tutakupatia Mfumo wa Kutunza kumbukumbu kwa njia ya Mtandao au kwenye Computer yako kwa ajili ya kusimamia Biashara yako
  8. Tutakufanyia Initial Marketing kwa Wateja wako (Inategemea aina ya biashara )wa Mwanzo ili kuwa na customer base ya kuanzia
  9. Pia tutakusaidia Mchakato wa Kufungua Bank Account kwa kutumia jina la Biashara yako (Deposit Ya Kwako)
Huduma hii ni designed and customized kwa ajili ya biashara Mpya kabisa.Iwapo biashara yako tayari ipo na unataka kupata huduma hii unaweza kuwasiliana nasi kw msaada zaidi.Gharama zetu ni Nafuu sana.Kwa mawasiliano,Whatsap 0710323060 Email: masokotz@yahoo.com

Karibuni Sana

Kuhusu SISI

Masoko Consulting ni Strategic Consulting Firm (Washauri waelekezi wa Kimkakati) ambao tunatumia mbinu za kisasa na utaalam wa kisasa katika kuwasaidia wateja wetu kutambua fursa na kuzitumia kwa ajili ya kukuza biashara zao na kukuza faida.Lengo letu ni kuwasaidi wafanyabiasha wadogo na wakati kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa biashara zao ili ziendani na dunia ya kisasa kwa kuwawezesha kufikia zana za kisasa,utaalamu wa kisasa na teknolojia katika kuendesha biashara zao.

Tulianza kutoa huduma Mwaka 2016 na tunafanya kazi kwa kutumia mbinu za kitaalamu na za kisasa.
 
Mawazo mema sana na umedadavua vyema...

Ila bwana masoko hivi serioua unawafanyia watu kazi ya kuhost website na domain email ila wewe huna website wala email binafsi na unatumia yahoo??? Serious? U need mtu wa marketing..
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom