Qatar ilipata utajiri kutokana na gesi. Kwanini Tanzania ilizuia miradi ya gesi?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,832
Leo hii Tanzania tungekuwa tunauza gesi yetu Ulaya kwa bei ya juuu baada ya Urusi kususiwa.😭😭

Tazama hiyo ni nchi ya Qatar
Kabla ya kugundua gesi mwaka 2002 uchumi wao ulikuwa dola bilioni 19 tu, baada ya kugundua gesi uchumi wao leo ni dola bilioni 220.

Screenshot_20230101-142406.png

Hii imeniuma sana kwa kuwa Magufuli alitupa kwenye pipa la taka mradi wetu wa gesi.

Akadanganya kuwa gesi yetu imetwaliwa na mabeberu, sasa kama ilitwaliwa aliwezaje kuisimamisha?

Na kama alikuwa Waziri mwandamizi kwenye serikali ya Kikwete kwanini hakulisema hilo au hata kujiuzulu kuokoa gesi isiende kwa mabeberu?

Samia anawezaje ku negotiate mkataba ya gesi na nchi nyingine hivi sasa?
 
Mfano wako haupo relevant mkuu kuicompare Qatar na nchi za kiafrica Tena Tanzania.

Sisi ngozi nyeusi hatuwezi kuzisimamia Mali zetu, tumejaa ufisadi. Angola ilitabiriwa uchumi ungepaa na maisha ya wananchi yangekuwa mazuri Kama ulaya baada ya kuanza kuuza mafuta lakini mambo yakaenda tofauti na matarajio ya wengi, nchi bado Ni masikini Hadi leo. Msumbiji wameanza kuuza gesi yao, wacha tusubiri Kama uchumi wao utabadilika.
 
Mkuu,ningekuwa na lugha chafu kidogo, ingeshanitoka.

Mikataba ya gesi, ya lazima, ilipitishwa bungeni usiku kwa usiku kwenye bunge lipi? Ni serikali ipi ilipeleka mikataba ile gesi bungeni kwa dharula?

Unajua chochote kuhusu mikataba hiyo? Kati yako wewe na Magufuli, ni nani aliyekuwa kwenye nafasi ya kuijua mikataba hiyo?

Mwisho, umeuliza, gesi imegunduliwa na kuanza kuchimbwa lini?
 
Thinking yenu huwa siielewi kabisa, mmekaa kimihemko na ushabiki sana, hamjui kufikiria vizuri kabisa, kwenu ni bora siku ipite kwa kumtaja Magufuli, ili mkila ugali upite vizuri kwenye koo.

Wewe unaamini tatizo la umasikini/poor decision nchi hii lililetwa na Magufuli, wala huoni kama ni la kimfumo, sasa mbona lilishakuwepo hata kabla ya ujio wa Magufuli?

Mbona hujiulizi, licha ya madini tuliyonayo, ikiwemo Tanzanite, yanayopatikana Tanzania pekee bado tuko nyuma kimaendeleo, kwanini uamini hiyo gesi inayopatikana maeneo mengi duniani ingetutoa kwenye umasikini? kwa usimamizi gani? wa CCM hii hii?!
 
Jibu zuri kabisaaa
 
Leo hii Tanzania tungekuwa tunauza gesi yetu Ulaya kwa bei ya juuu baada ya Urusi kususiwa.😭😭

Tazama hiyo ni nchi ya Qatar
Kabla ya kugundua gesi mwaka 2002 uchumi wao ulikuwa dola bilioni 19 tu, baada ya kugundua gesi uchumi wao leo ni dola bilioni 220.

View attachment 2465599

Hii imeniuma sana kwa kuwa Magufuli alitupa kwenye pipa la taka mradi wetu wa gesi.

Akadanganya kuwa gesi yetu imetwaliwa na mabeberu, sasa kama ilitwaliwa aliwezaje kuisimamisha?

Na kama alikuwa Waziri mwandamizi kwenye serikali ya Kikwete kwa nini hakulisema hilo au hata kujiuzulu kuokoa gesi isiende kwa mabeberu?

Samia anawezaje ku negotiate mkataba ya gesi na nchi nyingine hivi sasa?
Nyie mnages nyie
 
Yule bwana ukiacha kwamba alikuwa mtu wa mihemko Ila kwa sehemu kubwa hakuwa na akili na exposure ya Uchumi na biashara..

Ni ajabu Sana kina Kikwete waliacha Nchi ikaongozwa na bwana yule wakati wakijua historia yake sio mtu mzuri yaani Ni mtu wa kusimamiwa sio kujisimamia au kusimamia wengine..

Hata miradi aliyoiasisi ukiacha timing mbovu na mechanism aliyoitumia kuanza kuitekeleza Ila mingi ya hiyo miradi Ni tembo mweupe.Mda utasema.
 
Walisema kabla ya December kuisha watakuwa wameshamaliza majadiliano ya mkataba wa gas, kiko wapi.

Mama alipoingia aliamuru wamalize majadiliano ya bandari haraka na Kakoko akatolewa kwa sababu alionekana nuksi; kiko wapi.

Haya mambo ni raisi kulaumu mitandaoni tu, ila raisi akishapewa elimu na negotiators nini wanagawa wenyewe wanabaki kimya tu.

Isitoshe ata hao mabeberu wakifanikiwa hiyo gas wana mpango wa kupeleka soko la Asia, sio Europe.

Hakuna nchi ya ulaya yenye shida na gas ya Tanzania it’s too expensive to ship liquified gas. Ukijumlisha na lead time ya kupata volume capacity wanayotaka ata kwa nchi yenye GDP ndogo inventory will make that gas too expensive kwenye soko lao. .

Haya mambo ni rahisi kuropoka na kulaumu kwa watu wasio elewa how the industry work ata huyo J.K mwenyewe akutaka ku sign mkataba wa LNG baada ya kuonywa lawama za mbeleni ata akiwa kaburini, akikurupuka bila kuweka maslahi ya nchi mbele.
 
Gesi ina expire date kuwa imeoza baada ya JPM kuiweka pending? Kama haipo basi hakuna tatizo itatumika.

Umeuliza swali la kidwanzi!! Ninajua hufahamu “game of timing”. Sisi tuna makaa ya mawe (yasiyo na expiry date kama unavotaka). Kama tungeyachimba miaka iliyopita ingesaidia. Sasa hatuwezi kuyachimba kwa sababu yanapigwa vita kwa uharibifu wa mazingira!! Shida iko hapa - tumechelewa kuingiza gesi sokoni na tutaowakuta sokoni tayari, wataathiri mapato yetu!!

Ni akili hii ya vijana wakumbafu* imelifikisha taifa hapa. Kudhani muda mara zote uko upande wetu. Kijana ww hovyo sana.
 
Utajiri huanzia mtu mmoja, familia, mtaa, Kijiji, kata, wilaya, mkoa na mwisho taifa.

Hawezekani taifa au nchi kuwa tajiri bila kwanza kuwa na sera za kuwawezesha wananchi wake kuwa matajiri.

Kosa kubwa la nchi za Afrika ni fikra potofu kuwa serikali inaweza kufanya nchi tajiri wakati wananchi ni masikini.

Ni lazima serikali iweke mazingira ya watu binafsi kuwa matajiri (mara nyingi utajiri hutoka nje, unahifadhi ulichonacho na kukusanya kutoka kwa wengine zaidi).

Utumwa, ukoloni mkongwe na mamboleo unathibitisha hilo.
Fikra potofu za kimasikini za kuwakamua wananchi Kodi na tozo huku tukiongeza taasisi za udhibiti/kuzuia ubunifu haziwezi kuondoa umasikini kamwe.
 
Leo hii Tanzania tungekuwa tunauza gesi yetu Ulaya kwa bei ya juuu baada ya Urusi kususiwa.😭😭

Tazama hiyo ni nchi ya Qatar
Kabla ya kugundua gesi mwaka 2002 uchumi wao ulikuwa dola bilioni 19 tu, baada ya kugundua gesi uchumi wao leo ni dola bilioni 220.

View attachment 2465599

Hii imeniuma sana kwa kuwa Magufuli alitupa kwenye pipa la taka mradi wetu wa gesi.

Akadanganya kuwa gesi yetu imetwaliwa na mabeberu, sasa kama ilitwaliwa aliwezaje kuisimamisha?

Na kama alikuwa Waziri mwandamizi kwenye serikali ya Kikwete kwa nini hakulisema hilo au hata kujiuzulu kuokoa gesi isiende kwa mabeberu?

Samia anawezaje ku negotiate mkataba ya gesi na nchi nyingine hivi sasa?
Mjinga tu. Wewe una chuki tu na magufuli. Sasa hapo Magufuli anahusika vipi na gesi kuuzwa Ulaya? Kinachojulikana priority ilikua gesi izalishe umeme, hatua inayofuata ya kuuza nje ndio itafuata.
 
Umeuliza swali la kidwanzi!! Ninajua hufahamu “game of timing”. Sisi tuna makaa ya mawe (yasiyo na expiry date kama unavotaka). Kama tungeyachimba miaka iliyopita ingesaidia. Sasa hatuwezi kuyachimba kwa sababu yanapigwa vita kwa uharibifu wa mazingira!! Shida iko hapa - tumechelewa kuingiza gesi sokoni na tutaowakuta sokoni tayari, wataathiri mapato yetu!!

Ni akili hii ya vijana wakumbafu* imelifikisha taifa hapa. Kudhani muda mara zote uko upande wetu. Kijana ww hovyo sana.
Kwamba tumechelewa kuingiza gesi sokoni. Hahaha Kazi ipo.
 
Thinking yenu huwa siielewi kabisa, mmekaa kimihemko na ushabiki sana, hamjui kufikiria vizuri kabisa, kwenu ni bora siku ipite kwa kumtaja Magufuli, ili mkila ugali upite vizuri kwenye koo.

Wewe unaamini tatizo la umasikini/poor decision nchi hii lililetwa na Magufuli, wala huoni kama ni la kimfumo, sasa mbona lilishakuwepo hata kabla ya ujio wa Magufuli?

Mbona hujiulizi, licha ya madini tuliyonayo, ikiwemo Tanzanite, yanayopatikana Tanzania pekee bado tuko nyuma kimaendeleo, kwanini uamini hiyo gesi inayopatikana maeneo mengi duniani ingetutoa kwenye umasikini? kwa usimamizi gani? wa CCM hii hii?!
Mifumo ya ccm ni ya wizi mtupu. Sema jpm analaumiwa kwa sababu aliongeza tatizo kipindi watu walitarajia yeye angekuwa mkombozi
 
Back
Top Bottom