Rweye
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 16,958
- 7,512
Ni wananchi wanaopatikana ndani ya mkoa wa Pwani, Kibaha mji katika mtaa wa Viziwa ziwa. Hari si shwari hasirani, unyanyasaji huu na tamaa za viongozi huko chini inawahangamiza wananchi wa Tanzania na raia pasipo kuwepo na mhamiaji.
Ni kaeneo kadogo kakiitwa "VIMISA". Hapa ndo panapoongelewa haswa, watu wametakiwa kulipia square meter moja kwa sh6,000/= Ili kufidia kile eti kinachoitwa fidia kwa aliyekuwa muwekezaji miaka 30 iliyopita na hata leo hajulikani ni nani na wala wananchi hawajawahi kumuona kwa macho.
Kuna vitisho, ulaghai na ghiliba za kila aina kutoka kwa viongozi wa mtaa mpaka wilaya na lao wote ni moja kuwabomolea wananchi ama walipe hiyo pesa haraka sana iwezekanavyo ndani ya miezi sita. Wameenda mbali hawaruhusu hata wananchi hao kupata huduma muhimu za kijamii ndani ya hilo eneo.
Swali hapa ni, kwanini 6,000 kwa sqmt1 eneo kama lile bei ambayo ni kama ya kukomoa tena haraka haraka ndani ya miezi 6 tu?
Ni kwanini mbali ya wananchi kukubali kulipia Ili kutii amri ya kibabe hiyo bado watishiwe kubomolewa?
Ni kwanini pamoja na kulipia bado hao wananchi wametengwa Ili wasipate huduma muhimu za kiraia kama raia wa nchi hii na hata umeme wanaambiwa wao hawastahili REA wakati maeneo jirani yao wanawekewa umeme wa REA?
Yako mengi lakini mamlaka tajwa hapo juu ndo wenye kuweza kusaidia wananchi hawa Ili wapatiwe na wao haki zap maana inaonekana kuna genge kubwa nyuma ya hili na wakubwa wengi wamo na wengine wananufaika nalo.