Pumzika Kwa amani Mwalimu Yohana Seme, Mhadhiri wa sheria chuo kikuu Mzumbe, ndaki ya Mbeya.

Junior counsel

Senior Member
May 17, 2022
190
503
Habari za mapumziko Wana jamii forum.

Wiki hii imekuwa nzito sana kwa familia ya chuo kikuu Mzumbe hasa ndaki ya Mbeya. Hii ni baada ya kuondokewa na Mhadhiri mkongwe na nguli wa kitivo Cha sheria siku ya tarehe 4 March 2023.Chanzo Cha kifo hicho ni ajali iliyotokea maeneo ya simike -Mbeya siku ya tarehe 4 majira ya asubuhi.

Enzi za uhai wake, Mwalimu Yohana Seme ambaye pia alikuwa Wakili msomi wa mahakama kuu pamoja na mahakama za chini yake alikuwa ni kipenzi Cha wanajumuiya wote wa Mzumbe kuanzia wanafunzi, wafanyakazi wenzake na hata wadau wengine.

Mwalimu Seme ni miongoni mwa walimu wa mwanzo walioanzisha Mzumbe kampasi ya Mbeya miaka ya 2000 mwanzoni ikiwa na changamoto nyingi lakini alisimama imara kutatua changamoto hizo mpaka kufikia mazingira bora yaliyopo Sasa.

Enzi za uhai wake Mwalimu Seme alikuwa akifundisha kozi mbalimbali za sheria kama vile sheria za familia, sheria za makampuni na nyingine nyingi.

Mazishi ya Mwalimu Seme yanafanyika Leo tarehe 8 mkoani Mbeya. Kwa hakika wanafamilia wa Mzumbe tumepoteza mtu haswaaaa kwani alikuwa ni zaidi ya Mwalimu,zaidi ya Wakili kwani Kwa wanafunzi wengi walimuona kama mzazi

Poleni Wana Mzumbe, poleni mawakili wa chapter ya Mbeya.

Bwana ametoa, bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

FB_IMG_16809635570329509.jpg
FB_IMG_16809635873607140.jpg
 
Back
Top Bottom