Pumzika kwa Amani Dr Kabourou, mpinzani wa kweli na muasisi wa "UKAWA" katika siasa za vyama vingi Tanzania

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,820
image.jpeg
image.jpeg
image.png

Isingelikuwa umbali wa maili nyingi kufika nyumbani,ningefika kumpumzisha rafiki yangu na ndugu yangu Dr.Aman Walid Kabourou(digala).Huyu ni Alama ya siasa za mageuzi ndani ya mkoa wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla.Dr.Walid amelala,hataamka tena,Walid ameenda na hawezi kurudi tena.Pumzika kwa amani mpambanaji na mpigania haki wa zama zile.

Huyu Walid nilikutana naye kwa mara ya kwanza kati ya mwaka 1993 na 1994 (kama kumbukumbu zangu zinanisaidia vema) nikiwa katika kazi zangu pale mkoani Tabora,kwenye nyumba ya kulala wageni iliyokuwa kata ya Gongoni,mtaa wa Bhachu karibu na ilipo shule ya msingi maarufu kama "Town School",pale nyuma ya uwanja wa Vita-Tabora.

Dr.Walid na wanasiasa wenzake wa upinzani,walikuwa wamekutana kwa siri ili kujaribu kuunda "UKAWA" yao katika kuelekea kwenye siasa za vyama vingi 1995.Ile ilikuwa ndio "UKAWA" ya kwanza kabisa kutaka kuundwa na vyama vya upinzani Tanzania,lakini nafasi ya Mwalimu Nyerere katika siasa za 1995,zilibaini nguvu ya "UKAWA" na hivyo kulizuia jambo hili kwa njia ya "Kisheria" na baadae "Kijasusi".Hadi leo,mzimu huu wa "UKAWA" haujapata kukaa sawa ili kuunganisha nguvu za vyama pinzani Tanzania.Dr.Walid aliamini sana katika saisa za muungano ili kuiondoa au kupunguza nguvu za chama tawala bungeni.

CCM inajua nini maana ya sheria kuruhusu vyama pinzani kuungana,CCM inajua nini nguvu ya vyama pinzani pale vinapoamua kuungana na kuweka tofauti zao pembeni na kuamua kuwa kitu kimoja,ndio maana katika uchambuzi wa siasa za Tanzania,kila unapoweka sababu ya kwanini vyama mbadala vinapata shida ya kuingia Ikulu,moja ya sababu ni vyama hivi kutokuwa na "ushirikiano" wakati wa uchaguzi.Si ajabu,moja ya mikakati ya "Think Tank" ya CCM,ni kuhakikisha "muungano" wa vyama mbadala haupatikana au unavurugwa kwa nguvu zote.

Kwanini ilikuwa wakutane Tabora?Ilikuwa wakutane Tabora sababu hapa ndio kitovu cha harakati za siasa za vyama vingi Tanzania,hapa ndio walipotokea kina Mapalala na CUF,kina Fundikila na TADEA,NRA ya Malima ilikuwa na mizizi katika mkoa huu,na UMD ilijaa wanaharakati wengi wa Rufita,Gongoni,Kitete na Isevya.Tabora ilikuwa moto kuelekea uchaguzi wa 1995.

Siku kadhaa nilizotumia na Dr.Walid pale Tabora,zilifanya kuwa mwanzo wa ukaribu wetu.Siku hizo ndio zilinifanya kumfahamu haswa Dr.Walid na harakati zake,uwezo wake wa kujenga hoja na ujasiri wake katika siasa ngumu za upinzani katika nchi ya mfumo dola kama Tanzania.Achana na kina Dr.Slaa na Prof.Lipumba,achana na kina Lema na Freeman Mbowe,weka pembeni kidogo majina ya kina Zitto Kabwe na Mabere Marando,huyu mtu anaitwa Dr.Walid alikuwa mwanga na mfano mkubwa sana wa siasa ngumu za upinzani.

Dr.Walid alisimika siasa za upinzani katika mikoa ya Magharibi,hasa Kigoma na Tabora,na baadae alifungua matawi katika mitaa mbalimbali ndani ya mkoa wa Tabora.Huyu ndiye alipeleka moyo wa siasa za CHADEMA pale Tabora mjini ambapo kulikuwa na nguvu ya CUF,TADEA na NRA.Nguvu ya CUF Tabora ilikuwa ni Mapalala,Lipumba na Dr Othman;TADEA sababu ya Mzee Chief Fundikira na NRA ilipata nguvu sababu ya Prof Malima na chanzo cha yeye kuondolewa wizarani,na tamko lake la kuondoka CCM alilitoa akiwa Tabora.Mambo haya yanafichwafichwa,lakini tuliokuwepo,pale Msikiti wa Ijumaa wa Gongoni,enzi hiyo 1990's za Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Sheikh Alli Salala,tunajua kwanini ilikuwa ngumu kwa CHADEMA ile ya kina Mtei na Marehemu Bob Makani kupenya kwenye mkoa kama wa Tabora.

Dr.Walid ndio alipeleka CHADEMA kufungua ofisi katika mkoa wa Tabora,ofisi hiyo ilikuwa kwenye nyumba ya mzee mmoja katika barabara ya Kitete,kwenye makutano ya Kitete na mtaa wa Rehani,mkabala na msikiti wa Kitete maarufu kama "Masjid Raudhwa".Ilikuwa ni nyumba dhaifu,yenye mbavu za mbwa,isiyo hata na umeme,lakini hapo ndio Walid alilala na kupanga mikakati yake katika kueneza CHADEMA mkoa wa Tabora miaka ile ya 1990's.Wakati huo hakukuwa na ruzuku,wala miamala ya simu,hata pesa ilipofika posta,ilicheleweshwa kutolewa ili kupunguza harakati.

Unapoizungumzia CHADEMA na waasisi wake,ni lazima umzungumzie Dr Walid,hawa kina Dr.Slaa walikuwa bado wapo CCM wakati Dr.Walid alipowekewa sumu kwenye chakula akiwa maeneo ya Kazura-Mimba,behewa la "Buffet" akielekea Kigoma baada ya kutoka kupanda mbegu ya upinzani mkoa wa Tabora.

Ni bahati mbaya Walid aliondoka katika chama alichokipenda sana,chama alichokiasisi kwa jasho na damu,Walid amelala umauti na atavikwa bendera ya chama ambacho hakukipigania kwa jasho na damu,na kuna wakati alikuwa akifikiri alipoitoa CHADEMA na leo hayupo nayo,alitokwa na machozi.Bendera anayozikwa nayo leo,haina alama ya jasho na damu ya Dr Walid,mwisho huu,sio mwisho ambao Walid aliutamani wakati ule akiwa mpinzani wa kweli.Kama wakati ungerudi nyuma,Dr Walid angeibasilisha historia hii anayoondoka nayo.

Dr.Walid hakuondoka CHADEMA kwa kupenda,Walid aliondoka CHADEMA kwa hasira,ni bahati mbaya Mungu amemchukua bila yeye kuandika kitabu ya nini kilitokea,hata alipokuwa CCM,Dr Walid hakuwahi kukashifu kule alipotokea,hakukashifu sababu ukweli wa nafsi yake ulikuwa katika siasa za harakati na ukombozi,aliondoka huku mapenzi yake kwa watu wake wa Kigoma yakiwa juu sana.

Dr.Walid anakumbuka vijana wengi waliofungwa na kuteswa sababu ya kumuunga mkono,Walid anakumbuka vijana wengi walivyojitoa katika kumlinda na kumpigania,anakumbuka alivyobebwa juujuu toka Stesheni mpaka Ujiji aliposhuka kwenye gari Moshi.

Dr.Walid alitengeneza taswira chanya juu ya haki za kisiasa kupiganiwa mahakamani.Kesi yake na Premji ilikuwa ya kuvutia sana.Nakumbuka kuifuatilia sana katika vyombo vya habari na wakati mwingine moja kwa moja.Kesi ile ilikuwa chini ya Jaji Mfalila,Samatta na Jaji Lubuva.

Ilivutia watu wengi,Premji akiongozwa na mawakili wake walimlalamikia Dr.Walid na wafuasi wake kutumia kauli za kibaguzi katika kampeni zake,Premji alilalamika kuitwa "Ponjoro".Ilikuwa ni kesi tamu na ya kuvutia.Ilistajabisha watu pale Bob Makani alipokuwa anaomba "pumziko" ili akavute Mkambadoti wake.Zilikuwa ni nyakati za kusisimua na kupandwa kwa mbegu ya upinzani Tanzania.

Nimeangalia katika maktaba yangu,nimekuta sehemu ya mahojiano ya mawakili ktk kesi hii maarufu jinsi ilivyokuwa ikichapishwa magazetini,nimeweka kipande cha sehemu ya taarifa ya hukumu ya kesi ya Premji na Dr.Walid.Mungu ampumzishe rafiki yangu Walid.

Bahati mbaya nyakati hizo hakukuwa na magazeti mengi wala mitandao kama leo,bila shaka ingalikuwepo,basi Dr Walid angekuwa ni moja kati ya wanasiasa maarufu wa upinzani zaidi ya hawa tunaowataja leo.Wakati na teknolojia,havikumtendea haki digala Dr.Walid Kabourou.

Alipokuwa akiongea Dr.Walid,kama ukimsikiliza,basi baada ya mkutano unaweza kubeba mawe na kuanza kutafuta ofisi za serikali zilipo.Dr Walid alikuwa "eloquent",aliweza kushawishi na alijua kujenga hoja.Kila alipounguruma Ujiji,basi Ikulu ya Dsm ilitikisika.

Ilikuwa ni ushindi mkubwa sana kwa CCM baada ya kuona ndani ya chama alichokuwepo Walid wametofautiana.Walitumia nafasi hii kumvuta Walid na kumuahidi vyeo na mazingira salama ya kuishi,hili linaweza kuwa hakina tofauti na lile la balozi wetu wa Sweden.

Pengine hata Zitto isingekuwa ACT,labda angekuwa upande wa pili.Kupitia Dr Walid,Zitto na Slaa,vyama vya upinzani,vijifunze kumaliza migogoro yake ya ndani,kutunza hazina ya viongozi aina ya Kabourou ambao hukata tamaa na kuamua kuungana na adui baada ya kuona kama wanaonewa.

Vijana walio katika vyama pinzani,wajifunze kuwa na adabu,na wajue kuwa hapo vilipo vyama vyao,kuna watu huko nyuma walilipa kwa gharama ya uhai na damu.

Kuna mengi ya kumzungumzia Dr.Walid,ninashindwa kuandika yote sababu Walid amekata kauli na pumzi,hawezi tena kujizungumzia na kujitetea,si haki kuandika mengine ambayo angelikuwa hai,angeweza kupata nafsi ya kuyasemea.Ila kubwa kuliko yote,Walid alikuwa ni "mpinzani" mpaka mauti inamkuta.Si ajabu katika uongozi wake,mkoa wa Kigoma ulikuwa na wabunge wengi wa upinzani kuliko CCM.Walid aliamini katika siasa za ushindani na upinzani,hakuona tabu kwa kijana wake Zitto kushinda jimbo la Kigoma Mjini sababu aliamini umuhimu wa upinzani katika mkoa wake wa Kigoma.

Pumzika kwa Amani Digala Dr Walid Aman Kabourou...Tutaonana tena katika ulimwengu wa pili.
 
Asante Mungu ampumzishe kwa amani.
Siasa za upinzani ndio zishazikwa mpaka 2030 kwa watakaokuwa hai.
 
Dr. Apumzike kwa Amani, Suala la watu wengi kutotimiza malengo yao ni kutokana na ngazi ya familia kuwa duni na kutokuwa stable kiuchumi, Mbowe anaweza survive kwa sababu kwao aliachiwa msingi kidogo ila hawa wenzetu kina Machali, Fubusa, Mchange, Kafulila, Kaborou unakuta familia nzima ni yeye tu ndiye anategemewa akishayumbishwa sana ndugu wa karibu watamlilia arudi CCM ili aweze kuwafanya wa survive
 
Makala nzuri!
Kwa nini hamkutafuta enzi za uhai wake kumshauri aandike historia ya maisha yake kwenye harakati?

Je mpaka anaaga dunia hii alikuwa bado anaamini kwenye chama tawala ama alikuwa huko tu kwa kuwa....
 
Hakuna kilichowahi kuletwa na Barafu hapa jamvini nikakipa kisogo. Huyu jamaa yuko SMART sana kwenye uwasilishaji wa mada zake. Kwa hakika zinavutia na utatamani urudierudie kuzisoma. Ahsante sana mkuu. Umetufungua macho tulio wengi.
 
Mwisho mzuri ndio kila kitu..... Yote aliyofanya kaborou hayawezi kuheshimika sasa kwa sababu mwisho wake aliumalizia pabaya

Huyu alishiriki kuchakachua kura za upinzani kigoma na kuhakikisha majimbo yote ya NCCR yanarudi CCM na akafanikiwa!!! Yaani ameua upinzani aliouasisi!!

Na ili kuonyesha alijikwaa ilisababisha wananchi wamkatae hadi akaangushwa na ''MTOTO'' wake kisiasa Mhe Zitto kwa kura nyingi sana

Anyway pamoja na mwisho wake mbaya ila tuliokulia kigoma tutamkumbuka huyu mwamba ila liwe funzo tujenge mwisho mzuri kuliko mwanzo maana unapokufa mwisho wako ndio una determine ukumbukwe kwa lipi

RIP kaborou
 
View attachment 708656 View attachment 708655 View attachment 708648

Isingelikuwa umbali wa maili nyingi kufika nyumbani,ningefika kumpumzisha rafiki yangu na ndugu yangu Dr.Aman Walid Kabourou(digala).Huyu ni Alama ya siasa za mageuzi ndani ya mkoa wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla.Dr.Walid amelala,hataamka tena,Walid ameenda na hawezi kurudi tena.Pumzika kwa amani mpambanaji na mpigania haki wa zama zile.

Huyu Walid nilikutana naye kwa mara ya kwanza kati ya mwaka 1993 na 1994 (kama kumbukumbu zangu zinanisaidia vema) nikiwa katika kazi zangu pale mkoani Tabora,kwenye nyumba ya kulala wageni iliyokuwa kata ya Gongoni,mtaa wa Bhachu karibu na ilipo shule ya msingi maarufu kama "Town School",pale nyuma ya uwanja wa Vita-Tabora.

Dr.Walid na wanasiasa wenzake wa upinzani,walikuwa wamekutana kwa siri ili kujaribu kuunda "UKAWA" yao katika kuelekea kwenye siasa za vyama vingi 1995.Ile ilikuwa ndio "UKAWA" ya kwanza kabisa kutaka kuundwa na vyama vya upinzani Tanzania,lakini nafasi ya Mwalimu Nyerere katika siasa za 1995,zilibaini nguvu ya "UKAWA" na hivyo kulizuia jambo hili kwa njia ya "Kisheria" na baadae "Kijasusi".Hadi leo,mzimu huu wa "UKAWA" haujapata kukaa sawa ili kuunganisha nguvu za vyama pinzani Tanzania.Dr.Walid aliamini sana katika saisa za muungano ili kuiondoa au kupunguza nguvu za chama tawala bungeni.

CCM inajua nini maana ya sheria kuruhusu vyama pinzani kuungana,CCM inajua nini nguvu ya vyama pinzani pale vinapoamua kuungana na kuweka tofauti zao pembeni na kuamua kuwa kitu kimoja,ndio maana katika uchambuzi wa siasa za Tanzania,kila unapoweka sababu ya kwanini vyama mbadala vinapata shida ya kuingia Ikulu,moja ya sababu ni vyama hivi kutokuwa na "ushirikiano" wakati wa uchaguzi.Si ajabu,moja ya mikakati ya "Think Tank" ya CCM,ni kuhakikisha "muungano" wa vyama mbadala haupatikana au unavurugwa kwa nguvu zote.

Kwanini ilikuwa wakutane Tabora?Ilikuwa wakutane Tabora sababu hapa ndio kitovu cha harakati za siasa za vyama vingi Tanzania,hapa ndio walipotokea kina Mapalala na CUF,kina Fundikila na TADEA,NRA ya Malima ilikuwa na mizizi katika mkoa huu,na UMD ilijaa wanaharakati wengi wa Rufita,Gongoni,Kitete na Isevya.Tabora ilikuwa moto kuelekea uchaguzi wa 1995.

Siku kadhaa nilizotumia na Dr.Walid pale Tabora,zilifanya kuwa mwanzo wa ukaribu wetu.Siku hizo ndio zilinifanya kumfahamu haswa Dr.Walid na harakati zake,uwezo wake wa kujenga hoja na ujasiri wake katika siasa ngumu za upinzani katika nchi ya mfumo dola kama Tanzania.Achana na kina Dr.Slaa na Prof.Lipumba,achana na kina Lema na Freeman Mbowe,weka pembeni kidogo majina ya kina Zitto Kabwe na Mabere Marando,huyu mtu anaitwa Dr.Walid alikuwa mwanga na mfano mkubwa sana wa siasa ngumu za upinzani.

Dr.Walid alisimika siasa za upinzani katika mikoa ya Magharibi,hasa Kigoma na Tabora,na baadae alifungua matawi katika mitaa mbalimbali ndani ya mkoa wa Tabora.Huyu ndiye alipeleka moyo wa siasa za CHADEMA pale Tabora mjini ambapo kulikuwa na nguvu ya CUF,TADEA na NRA.Nguvu ya CUF Tabora ilikuwa ni Mapalala,Lipumba na Dr Othman;TADEA sababu ya Mzee Chief Fundikira na NRA ilipata nguvu sababu ya Prof Malima na chanzo cha yeye kuondolewa wizarani,na tamko lake la kuondoka CCM alilitoa akiwa Tabora.Mambo haya yanafichwafichwa,lakini tuliokuwepo,pale Msikiti wa Ijumaa wa Gongoni,enzi hiyo 1990's za Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Sheikh Alli Salala,tunajua kwanini ilikuwa ngumu kwa CHADEMA ile ya kina Mtei na Marehemu Bob Makani kupenya kwenye mkoa kama wa Tabora.

Dr.Walid ndio alipeleka CHADEMA kufungua ofisi katika mkoa wa Tabora,ofisi hiyo ilikuwa kwenye nyumba ya mzee mmoja katika barabara ya Kitete,kwenye makutano ya Kitete na mtaa wa Rehani,mkabala na msikiti wa Kitete maarufu kama "Masjid Raudhwa".Ilikuwa ni nyumba dhaifu,yenye mbavu za mbwa,isiyo hata na umeme,lakini hapo ndio Walid alilala na kupanga mikakati yake katika kueneza CHADEMA mkoa wa Tabora miaka ile ya 1990's.Wakati huo hakukuwa na ruzuku,wala miamala ya simu,hata pesa ilipofika posta,ilicheleweshwa kutolewa ili kupunguza harakati.

Unapoizungumzia CHADEMA na waasisi wake,ni lazima umzungumzie Dr Walid,hawa kina Dr.Slaa walikuwa bado wapo CCM wakati Dr.Walid alipowekewa sumu kwenye chakula akiwa maeneo ya Kazura-Mimba,behewa la "Buffet" akielekea Kigoma baada ya kutoka kupanda mbegu ya upinzani mkoa wa Tabora.

Ni bahati mbaya Walid aliondoka katika chama alichokipenda sana,chama alichokiasisi kwa jasho na damu,Walid amelala umauti na atavikwa bendera ya chama ambacho hakukipigania kwa jasho na damu,na kuna wakati alikuwa akifikiri alipoitoa CHADEMA na leo hayupo nayo,alitokwa na machozi.Bendera anayozikwa nayo leo,haina alama ya jasho na damu ya Dr Walid,mwisho huu,sio mwisho ambao Walid aliutamani wakati ule akiwa mpinzani wa kweli.Kama wakati ungerudi nyuma,Dr Walid angeibasilisha historia hii anayoondoka nayo.

Dr.Walid hakuondoka CHADEMA kwa kupenda,Walid aliondoka CHADEMA kwa hasira,ni bahati mbaya Mungu amemchukua bila yeye kuandika kitabu ya nini kilitokea,hata alipokuwa CCM,Dr Walid hakuwahi kukashifu kule alipotokea,hakukashifu sababu ukweli wa nafsi yake ulikuwa katika siasa za harakati na ukombozi,aliondoka huku mapenzi yake kwa watu wake wa Kigoma yakiwa juu sana.

Dr.Walid anakumbuka vijana wengi waliofungwa na kuteswa sababu ya kumuunga mkono,Walid anakumbuka vijana wengi walivyojitoa katika kumlinda na kumpigania,anakumbuka alivyobebwa juujuu toka Stesheni mpaka Ujiji aliposhuka kwenye gari Moshi.

Dr.Walid alitengeneza taswira chanya juu ya haki za kisiasa kupiganiwa mahakamani.Kesi yake na Premji ilikuwa ya kuvutia sana.Nakumbuka kuifuatilia sana katika vyombo vya habari na wakati mwingine moja kwa moja.Kesi ile ilikuwa chini ya Jaji Mfalila,Samatta na Jaji Lubuva.

Ilivutia watu wengi,Premji akiongozwa na mawakili wake walimlalamikia Dr.Walid na wafuasi wake kutumia kauli za kibaguzi katika kampeni zake,Premji alilalamika kuitwa "Ponjoro".Ilikuwa ni kesi tamu na ya kuvutia.Ilistajabisha watu pale Bob Makani alipokuwa anaomba "pumziko" ili akavute Mkambadoti wake.Zilikuwa ni nyakati za kusisimua na kupandwa kwa mbegu ya upinzani Tanzania.

Nimeangalia katika maktaba yangu,nimekuta sehemu ya mahojiano ya mawakili ktk kesi hii maarufu jinsi ilivyokuwa ikichapishwa magazetini,nimeweka kipande cha sehemu ya taarifa ya hukumu ya kesi ya Premji na Dr.Walid.Mungu ampumzishe rafiki yangu Walid.

Bahati mbaya nyakati hizo hakukuwa na magazeti mengi wala mitandao kama leo,bila shaka ingalikuwepo,basi Dr Walid angekuwa ni moja kati ya wanasiasa maarufu wa upinzani zaidi ya hawa tunaowataja leo.Wakati na teknolojia,havikumtendea haki digala Dr.Walid Kabourou.

Alipokuwa akiongea Dr.Walid,kama ukimsikiliza,basi baada ya mkutano unaweza kubeba mawe na kuanza kutafuta ofisi za serikali zilipo.Dr Walid alikuwa "eloquent",aliweza kushawishi na alijua kujenga hoja.Kila alipounguruma Ujiji,basi Ikulu ya Dsm ilitikisika.

Ilikuwa ni ushindi mkubwa sana kwa CCM baada ya kuona ndani ya chama alichokuwepo Walid wametofautiana.Walitumia nafasi hii kumvuta Walid na kumuahidi vyeo na mazingira salama ya kuishi,hili linaweza kuwa hakina tofauti na lile la balozi wetu wa Sweden.

Pengine hata Zitto isingekuwa ACT,labda angekuwa upande wa pili.Kupitia Dr Walid,Zitto na Slaa,vyama vya upinzani,vijifunze kumaliza migogoro yake ya ndani,kutunza hazina ya viongozi aina ya Kabourou ambao hukata tamaa na kuamua kuungana na adui baada ya kuona kama wanaonewa.

Vijana walio katika vyama pinzani,wajifunze kuwa na adabu,na wajue kuwa hapo vilipo vyama vyao,kuna watu huko nyuma walilipa kwa gharama ya uhai na damu.

Kuna mengi ya kumzungumzia Dr.Walid,ninashindwa kuandika yote sababu Walid amekata kauli na pumzi,hawezi tena kujizungumzia na kujitetea,si haki kuandika mengine ambayo angelikuwa hai,angeweza kupata nafsi ya kuyasemea.Ila kubwa kuliko yote,Walid alikuwa ni "mpinzani" mpaka mauti inamkuta.Si ajabu katika uongozi wake,mkoa wa Kigoma ulikuwa na wabunge wengi wa upinzani kuliko CCM.Walid aliamini katika siasa za ushindani na upinzani,hakuona tabu kwa kijana wake Zitto kushinda jimbo la Kigoma Mjini sababu aliamini umuhimu wa upinzani katika mkoa wake wa Kigoma.

Pumzika kwa Amani Digala Dr Walid Aman Kabourou...Tutaonana tena katika ulimwengu wa pili.
Kabourou alikataa kutumiwa kama karai. Wakati anaipigania chadema, makamanda wa leo wengi walikwa na mrema nccr na baadaye tlp. Upepo ulipoelekea chadema wakamtosa mrema na kutimkia chadema.

Wapima upepo, wasivyo na soni leo wanathubutu kumwita Dr Walid msaliti.
 
Barafu leo umenirudusha nyumbani Tabora kwa jinsi. Shukran kwa tanzia hii ya mwamba huyu nadhani kuna mengi yabkujifunza hasa kw wapinzani ili kuleta siasa zenye weledi na mizani isiyo na shaka, kuna shida sana linapokuja swala la uongozi na kutofautiana mawazo kwenye vyama vya upinzani. Mie kwasababu ya Tabora always huwa najiona mpinzani hata kama sina chama
 
Hata Mungu sio wote wanaoridhika nae
Si ajabu kwa wewe na kwangu!!Sisi ambao uwepo wetu ni matokeo ya uchafu wa manii wa watu wawili....Relax and take life easy!!
Unapoita manii uchafu unamkufuru mwenyezi Mungu. Usirudie tafadhali.
 
Tulikuwa na Wimbo Wetu wa:

Aifora Aifora, Aifora mwenda salama!

Nikija ntampata nani, utampata mjinga mwenzako!

....

Kila nikilisikia hili jina naikumbuka Aifora Beach.

RIP
 
Dr. Apumzike kwa Amani, Suala la watu wengi kutotimiza malengo yao ni kutokana na ngazi ya familia kuwa duni na kutokuwa stable kiuchumi, Mbowe anaweza survive kwa sababu kwao aliachiwa msingi kidogo ila hawa wenzetu kina Machali, Fubusa, Mchange, Kafulila, Kaborou unakuta familia nzima ni yeye tu ndiye anategemewa akishayumbishwa sana ndugu wa karibu watamlilia arudi CCM ili aweze kuwafanya wa survive
Si mbowe tu, sema na mrema, kyara, mbatia nk. They all inherited sound economic bases.

Devilish ulterior motives.
 
Back
Top Bottom