Pumzika kwa Amani Dr Kabourou, mpinzani wa kweli na muasisi wa "UKAWA" katika siasa za vyama vingi Tanzania

barafu Heshima mbele sana Barafu na asante kwa andiko historia.

Mara kwa mara nikipita katikati ya maandishi yako yaliyojaa historia ya kina ya baadhi ya mambo ya nyuma, basi humkumbuka member mwenzetu hapa jamvini aliyelowea Amerika kwa kipindi sasa akitumia jina la Jasusi hapa jukwaani.
 
Hakuna kilichowahi kuletwa na Barafu hapa jamvini nikakipa kisogo. Huyu jamaa yuko SMART sana kwenye uwasilishaji wa mada zake. Kwa hakika zinavutia na utatamani urudierudie kuzisoma. Ahsante sana mkuu. Umetufungua macho tulio wengi.
Asante!!Tumshukuru Mungu na JF kwa kutuweka pamoja
 
Si mbowe tu, sema na mrema, kyara, mbatia nk. They all inherited sound economic bases.

Devilish ulterior motives.
of course, mfano mtu Kama KAFULILA ukitoa SIASA hana kitu chochote cha kumuingizia kipato, MKOSAMALI alitoka chuo tu na kugombea ubunge ukitoa siasa hana mradi wala biashara ya kumuweka mjini kwa miaka 10 hadi 20 so anaweza akawa yuko vizuri upstairs ila changamoto za kiuchumi zikamfanya asalimu amri
 
of course, mfano mtu Kama KAFULILA ukitoa SIASA hana kitu chochote cha kumuingizia kipato, MKOSAMALI alitoka chuo tu na kugombea ubunge ukitoa siasa hana mradi wala biashara ya kumuweka mjini kwa miaka 10 hadi 20 so anaweza akawa yuko vizuri upstairs ila changamoto za kiuchumi zikamfanya asalimu amri
Wewe ni mpumbavu. Unajua kafulila na mkosamali walilipwa kiasi gani kwa ubunge wao miaka 5?! Pesa waliyyolipwa haitoshi kufungua hiyo biashara unayoifikiria wewe jinga?
 
Wewe ni mpumbavu. Unajua kafulila na mkosamali walilipwa kiasi gani kwa ubunge wao miaka 5?! Pesa waliyyolipwa haitoshi kufungua hiyo biashara unayoifikiria wewe jinga?
Tujadiliane bila matusi na maneno ya kuudhi!!
 
Kabourou alikataa kutumiwa kama karai. Wakati anaipigania chadema, makamanda wa leo wengi walikwa na mrema nccr na baadaye tlp. Upepo ulipoelekea chadema wakamtosa mrema na kutimkia chadema.

Wapima upepo, wasivyo na soni leo wanathubutu kumwita Dr Walid msaliti.

Alikataaa kutumiwa kama karai ndio lakini mwisho wake ccm wamemtelekeza kwenye ugonjwa hadi Mauti hadi mazishi
Kaisaidia ccm kurudi Kigoma lakini wamempa hadhi gani katika umauti?
 
of course, mfano mtu Kama KAFULILA ukitoa SIASA hana kitu chochote cha kumuingizia kipato, MKOSAMALI alitoka chuo tu na kugombea ubunge ukitoa siasa hana mradi wala biashara ya kumuweka mjini kwa miaka 10 hadi 20 so anaweza akawa yuko vizuri upstairs ila changamoto za kiuchumi zikamfanya asalimu amri

Watu wa karibu na kafulila ni marafiki wanasema tayari anajutia Sana kurudi ccm Sema hana namna
“ .... huku shida tu na hata niliyoahidiwa sijatekelezewa Bora kule sikua na kitu lakini nyota yangu ilikua inavuma hata nikisimama natingisha na hata pesa napata japo kidogo, nilikua na mashabiki mimi wako wapi?”
Alinukuliwa kafulila karibuni na mtu wake wa karibu

Nadhani akitizama mwisho uliofika Kwa mfalme kabourou , ccm hata kutoa sanda , jeneza na usafiri imekua tabu hadi waliposikia Zitto katoa gari ataumia zaidi

Mwisho wa siku kila mtu anataka heshima na mwisho mwema
Ccm walivyomtelekeza Kabourou ni kama wamembagua
 
Alikataaa kutumiwa kama karai ndio lakini mwisho wake ccm wamemtelekeza kwenye ugonjwa hadi Mauti hadi mazishi
Kaisaidia ccm kurudi Kigoma lakini wamempa hadhi gani katika umauti?
Ndio kilema mlichonacho ...mnakosolewa nyie badala ya kukubali tatizo na kutafakari suluhisho mnakimbilia kusema ya CCM. Nina hakika hata Lissu atakuja kuondoka Chadema kama ilivyotokea kwa majabali wengine sababu hamjifunzi! Hamsemezani ukweli ili mpone ...
 
Ndio kilema mlichonacho ...mnakosolewa nyie badala ya kukubali tatizo na kutafakari suluhisho mnakimbilia kusema ya CCM. Nina hakika hata Lissu atakuja kuondoka Chadema kama ilivyotokea kwa majabali wengine sababu hamjifunzi! Hamsemezani ukweli ili mpone ...
Kwa hiyo hutaki watu waseme ukweli kwa kuwa tu hata wao wana makengeza? Acha mambo yako weye
 
View attachment 708656 View attachment 708655 View attachment 708648


Isingelikuwa umbali wa maili nyingi kufika nyumbani,ningefika kumpumzisha rafiki yangu na ndugu yangu Dr.Aman Walid Kabourou(digala).Huyu ni Alama ya siasa za mageuzi ndani ya mkoa wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla.Dr.Walid amelala,hataamka tena,Walid ameenda na hawezi kurudi tena.Pumzika kwa amani mpambanaji na mpigania haki wa zama zile.

Huyu Walid nilikutana naye kwa mara ya kwanza kati ya mwaka 1993 na 1994 (kama kumbukumbu zangu zinanisaidia vema) nikiwa katika kazi zangu pale mkoani Tabora,kwenye nyumba ya kulala wageni iliyokuwa kata ya Gongoni,mtaa wa Bhachu karibu na ilipo shule ya msingi maarufu kama "Town School",pale nyuma ya uwanja wa Vita-Tabora.

Dr.Walid na wanasiasa wenzake wa upinzani,walikuwa wamekutana kwa siri ili kujaribu kuunda "UKAWA" yao katika kuelekea kwenye siasa za vyama vingi 1995.Ile ilikuwa ndio "UKAWA" ya kwanza kabisa kutaka kuundwa na vyama vya upinzani Tanzania,lakini nafasi ya Mwalimu Nyerere katika siasa za 1995,zilibaini nguvu ya "UKAWA" na hivyo kulizuia jambo hili kwa njia ya "Kisheria" na baadae "Kijasusi".Hadi leo,mzimu huu wa "UKAWA" haujapata kukaa sawa ili kuunganisha nguvu za vyama pinzani Tanzania.Dr.Walid aliamini sana katika saisa za muungano ili kuiondoa au kupunguza nguvu za chama tawala bungeni.

CCM inajua nini maana ya sheria kuruhusu vyama pinzani kuungana,CCM inajua nini nguvu ya vyama pinzani pale vinapoamua kuungana na kuweka tofauti zao pembeni na kuamua kuwa kitu kimoja,ndio maana katika uchambuzi wa siasa za Tanzania,kila unapoweka sababu ya kwanini vyama mbadala vinapata shida ya kuingia Ikulu,moja ya sababu ni vyama hivi kutokuwa na "ushirikiano" wakati wa uchaguzi.Si ajabu,moja ya mikakati ya "Think Tank" ya CCM,ni kuhakikisha "muungano" wa vyama mbadala haupatikana au unavurugwa kwa nguvu zote.

Kwanini ilikuwa wakutane Tabora?Ilikuwa wakutane Tabora sababu hapa ndio kitovu cha harakati za siasa za vyama vingi Tanzania,hapa ndio walipotokea kina Mapalala na CUF,kina Fundikila na TADEA,NRA ya Malima ilikuwa na mizizi katika mkoa huu,na UMD ilijaa wanaharakati wengi wa Rufita,Gongoni,Kitete na Isevya.Tabora ilikuwa moto kuelekea uchaguzi wa 1995.

Siku kadhaa nilizotumia na Dr.Walid pale Tabora,zilifanya kuwa mwanzo wa ukaribu wetu.Siku hizo ndio zilinifanya kumfahamu haswa Dr.Walid na harakati zake,uwezo wake wa kujenga hoja na ujasiri wake katika siasa ngumu za upinzani katika nchi ya mfumo dola kama Tanzania.Achana na kina Dr.Slaa na Prof.Lipumba,achana na kina Lema na Freeman Mbowe,weka pembeni kidogo majina ya kina Zitto Kabwe na Mabere Marando,huyu mtu anaitwa Dr.Walid alikuwa mwanga na mfano mkubwa sana wa siasa ngumu za upinzani.

Dr.Walid alisimika siasa za upinzani katika mikoa ya Magharibi,hasa Kigoma na Tabora,na baadae alifungua matawi katika mitaa mbalimbali ndani ya mkoa wa Tabora.Huyu ndiye alipeleka moyo wa siasa za CHADEMA pale Tabora mjini ambapo kulikuwa na nguvu ya CUF,TADEA na NRA.Nguvu ya CUF Tabora ilikuwa ni Mapalala,Lipumba na Dr Othman;TADEA sababu ya Mzee Chief Fundikira na NRA ilipata nguvu sababu ya Prof Malima na chanzo cha yeye kuondolewa wizarani,na tamko lake la kuondoka CCM alilitoa akiwa Tabora.Mambo haya yanafichwafichwa,lakini tuliokuwepo,pale Msikiti wa Ijumaa wa Gongoni,enzi hiyo 1990's za Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Sheikh Alli Salala,tunajua kwanini ilikuwa ngumu kwa CHADEMA ile ya kina Mtei na Marehemu Bob Makani kupenya kwenye mkoa kama wa Tabora.

Dr.Walid ndio alipeleka CHADEMA kufungua ofisi katika mkoa wa Tabora,ofisi hiyo ilikuwa kwenye nyumba ya mzee mmoja katika barabara ya Kitete,kwenye makutano ya Kitete na mtaa wa Rehani,mkabala na msikiti wa Kitete maarufu kama "Masjid Raudhwa".Ilikuwa ni nyumba dhaifu,yenye mbavu za mbwa,isiyo hata na umeme,lakini hapo ndio Walid alilala na kupanga mikakati yake katika kueneza CHADEMA mkoa wa Tabora miaka ile ya 1990's.Wakati huo hakukuwa na ruzuku,wala miamala ya simu,hata pesa ilipofika posta,ilicheleweshwa kutolewa ili kupunguza harakati.

Unapoizungumzia CHADEMA na waasisi wake,ni lazima umzungumzie Dr Walid,hawa kina Dr.Slaa walikuwa bado wapo CCM wakati Dr.Walid alipowekewa sumu kwenye chakula akiwa maeneo ya Kazura-Mimba,behewa la "Buffet" akielekea Kigoma baada ya kutoka kupanda mbegu ya upinzani mkoa wa Tabora.

Ni bahati mbaya Walid aliondoka katika chama alichokipenda sana,chama alichokiasisi kwa jasho na damu,Walid amelala umauti na atavikwa bendera ya chama ambacho hakukipigania kwa jasho na damu,na kuna wakati alikuwa akifikiri alipoitoa CHADEMA na leo hayupo nayo,alitokwa na machozi.Bendera anayozikwa nayo leo,haina alama ya jasho na damu ya Dr Walid,mwisho huu,sio mwisho ambao Walid aliutamani wakati ule akiwa mpinzani wa kweli.Kama wakati ungerudi nyuma,Dr Walid angeibasilisha historia hii anayoondoka nayo.

Dr.Walid hakuondoka CHADEMA kwa kupenda,Walid aliondoka CHADEMA kwa hasira,ni bahati mbaya Mungu amemchukua bila yeye kuandika kitabu ya nini kilitokea,hata alipokuwa CCM,Dr Walid hakuwahi kukashifu kule alipotokea,hakukashifu sababu ukweli wa nafsi yake ulikuwa katika siasa za harakati na ukombozi,aliondoka huku mapenzi yake kwa watu wake wa Kigoma yakiwa juu sana.

Dr.Walid anakumbuka vijana wengi waliofungwa na kuteswa sababu ya kumuunga mkono,Walid anakumbuka vijana wengi walivyojitoa katika kumlinda na kumpigania,anakumbuka alivyobebwa juujuu toka Stesheni mpaka Ujiji aliposhuka kwenye gari Moshi.

Dr.Walid alitengeneza taswira chanya juu ya haki za kisiasa kupiganiwa mahakamani.Kesi yake na Premji ilikuwa ya kuvutia sana.Nakumbuka kuifuatilia sana katika vyombo vya habari na wakati mwingine moja kwa moja.Kesi ile ilikuwa chini ya Jaji Mfalila,Samatta na Jaji Lubuva.

Ilivutia watu wengi,Premji akiongozwa na mawakili wake walimlalamikia Dr.Walid na wafuasi wake kutumia kauli za kibaguzi katika kampeni zake,Premji alilalamika kuitwa "Ponjoro".Ilikuwa ni kesi tamu na ya kuvutia.Ilistajabisha watu pale Bob Makani alipokuwa anaomba "pumziko" ili akavute Mkambadoti wake.Zilikuwa ni nyakati za kusisimua na kupandwa kwa mbegu ya upinzani Tanzania.

Nimeangalia katika maktaba yangu,nimekuta sehemu ya mahojiano ya mawakili ktk kesi hii maarufu jinsi ilivyokuwa ikichapishwa magazetini,nimeweka kipande cha sehemu ya taarifa ya hukumu ya kesi ya Premji na Dr.Walid.Mungu ampumzishe rafiki yangu Walid.

Bahati mbaya nyakati hizo hakukuwa na magazeti mengi wala mitandao kama leo,bila shaka ingalikuwepo,basi Dr Walid angekuwa ni moja kati ya wanasiasa maarufu wa upinzani zaidi ya hawa tunaowataja leo.Wakati na teknolojia,havikumtendea haki digala Dr.Walid Kabourou.

Alipokuwa akiongea Dr.Walid,kama ukimsikiliza,basi baada ya mkutano unaweza kubeba mawe na kuanza kutafuta ofisi za serikali zilipo.Dr Walid alikuwa "eloquent",aliweza kushawishi na alijua kujenga hoja.Kila alipounguruma Ujiji,basi Ikulu ya Dsm ilitikisika.

Ilikuwa ni ushindi mkubwa sana kwa CCM baada ya kuona ndani ya chama alichokuwepo Walid wametofautiana.Walitumia nafasi hii kumvuta Walid na kumuahidi vyeo na mazingira salama ya kuishi,hili linaweza kuwa hakina tofauti na lile la balozi wetu wa Sweden.

Pengine hata Zitto isingekuwa ACT,labda angekuwa upande wa pili.Kupitia Dr Walid,Zitto na Slaa,vyama vya upinzani,vijifunze kumaliza migogoro yake ya ndani,kutunza hazina ya viongozi aina ya Kabourou ambao hukata tamaa na kuamua kuungana na adui baada ya kuona kama wanaonewa.

Vijana walio katika vyama pinzani,wajifunze kuwa na adabu,na wajue kuwa hapo vilipo vyama vyao,kuna watu huko nyuma walilipa kwa gharama ya uhai na damu.

Kuna mengi ya kumzungumzia Dr.Walid,ninashindwa kuandika yote sababu Walid amekata kauli na pumzi,hawezi tena kujizungumzia na kujitetea,si haki kuandika mengine ambayo angelikuwa hai,angeweza kupata nafsi ya kuyasemea.Ila kubwa kuliko yote,Walid alikuwa ni "mpinzani" mpaka mauti inamkuta.Si ajabu katika uongozi wake,mkoa wa Kigoma ulikuwa na wabunge wengi wa upinzani kuliko CCM.Walid aliamini katika siasa za ushindani na upinzani,hakuona tabu kwa kijana wake Zitto kushinda jimbo la Kigoma Mjini sababu aliamini umuhimu wa upinzani katika mkoa wake wa Kigoma.

Pumzika kwa Amani Digala Dr Walid Aman Kabourou...Tutaonana tena katika ulimwengu wa pili.
Sahihisho dogo : TADEA ilikuwa na KASANGA TUMBO , chief ABDALLA FUNDIKIRA alikuwa na UMD
 
Ndio kilema mlichonacho ...mnakosolewa nyie badala ya kukubali tatizo na kutafakari suluhisho mnakimbilia kusema ya CCM. Nina hakika hata Lissu atakuja kuondoka Chadema kama ilivyotokea kwa majabali wengine sababu hamjifunzi! Hamsemezani ukweli ili mpone ...

Ccm wamembagua kaborou aliyerudisha uhai Kigoma
Wenzake wanawapeleka India yeye hata Muhimbili hadi ndugu wamechanga
Haya hata msiba wameshindwa kuubebaa?
 
Back
Top Bottom