PUGU: Maiti ya Mary Mkwaya Maramo, aliyekuwa afisa wa Wizara ya Nishati yafukuliwa na kuvuliwa nguo, yadaiwa kuingiliwa kimwili

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
754
3,097
Mwili wa aliyekuwa Afisa wa Wizara ya Nishati Mery Mkwaya Maramo aliyefariki mwanzoni mwa wiki hii na kuzikwa jana katika Makaburi ya Pugu Mwakanga jijini Dar es Salaam, Usiku wa kuamkia leo watu wasiojulikana wameufukua na kuutoa nje ya jeneza kisha kuuvua nguo .

Kaka wa Marehemu Mary, Deogratius Maramo amesema inasemekana mwili wa marehemu uliingiliwa kimwili lakini bado wanasubiri ripoti ya Polisi ili wajue kilichomtokea ndugu yao.

Kaka huyo wa marehemu amesema kuwa hakuna kitu chochote kilichoibiwa kaburini humo.

Marry.PNG

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mtaalam wa Afya wameufanyia Uchaguzi mwili wa Mary Maramo ambaye ni mtumishi wa Wizara ya Nishati na kukubaliana na ndugu wa marehemu kuwa mwili huo uhifadhiwe Tena.

Mwili wa Mary umevalishwa Nguo upya ukiwa ndani ya kaburi na kurudishwa kwenye jeneza na shughuli inayoendelea kwa sasa ni kulijenga kaburi mahala lilipobomolewa.
 
Ulozi at work!
May be mambo ya uchaguzi yamekaribia.
Waganga feki aanaotoa mashart magumu wakijua utashindwa kutimiza ili mwisho wa siku usipofanikiwa wanakua washajivua lawama kua ulishindwa mwenyewe masharti
Iam speechless....mhhh

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr
 
Back
Top Bottom