Daaah kuna watu watata kuelewa,Mifuko yote unaijua imefutwa(kuunganishwa na kua kitu kimoja) na kuanza kwa Mfumo wa Hifadhi wa Watumishi wa umma,NSSF kwa sasa itahudumia wafanyakazi sekta binafsi tu.
Watumishi wote,wafaidika/warithi wa mafao wa mifuko iliyoundiwa PSSSF,wataendelea kufanya kazi PSSSF na kupokea stahiki zao kama kawaida kupitia huo mfuko mpya.
Madeni,mali,mikataba iliyokua chini ya iliyofutwa itahamia PSSSF. Hii ni kuanzia kesho 1 mwezi wa 8 2018.Ni NSSF tu imebakia ila sasa ni strictly sekta binafsi.