PSRS mtaua vijana mtaani, toeni ajira

PSRS mtaua vijana mtaani, toeni ajira

Timoth1234

Member
Joined
Mar 13, 2025
Posts
5
Reaction score
5
Yaani kuna Uzi nimepitia humu Jobless wapo tayari kutoa 20% ya mshahara wake kwa miaka 2 ili tu apate kazi, daah jamani mtatua jobless tupeni kazi jamani daah Utumishi mtaua vijana mtaaani. Mitaji ya Biashara hatuna umri unaenda dira hakuna
 
Psrs hawatoi ajira.

Waajiri ndio wanatoa ajira.
 
PSRS wameweka pamba kwenye masikio. Next week nawindana nao, ama wanikande au niwavue msuli.
 
Nini kitatuhakikishia kuwa watatoa hiyo hela tena kwa miaka miwili isije baadae unaanza kuleta ujeuri.
 
Yaani kuna Uzi nimepitia humu Jobless wapo tayari kutoa 20% ya mshahara wake kwa miaka 2 ili tu apate kazi, daah jamani mtatua jobless tupeni kazi jamani daah Utumishi mtaua vijana mtaaani. Mitaji ya Biashara hatuna umri unaenda dira hakuna
Jiajirini wenyewe.
 
Hakuna simu iliyopigwa mkuu. Nilijaribu kuulizia tena wakaniambia niendelee kusubiri watanijulisha mchakato wa kuhakiki vyeti ukikamilika, hivyo bado nipo mtaani tu.
Eeh kuhakiki vyeti tena aah...mimi nlijua ukiitwa kazini imeisha hiyo na mshahara unaanza
 
Kila mchakato ni stress ndugu yangu. Ukishaenda kuripoti kazini na barua yako pale masjala unakutana na HR anakwambia ukatoe copy ya vyeti na uache namba ya simu watakupigia simu baada ya kumaliza uhakiki. Mshahara mpaka upate check number ni process ndefu yaani lazima uwe mvumilivu tu.
 
Hakuna simu iliyopigwa mkuu. Nilijaribu kuulizia tena wakaniambia niendelee kusubiri watanijulisha mchakato wa kuhakiki vyeti ukikamilika, hivyo bado nipo mtaani tu.
Ndio utaratibu upo hivyo ?
 
Ndio utaratibu upo hivyo ?
Ndio utakuwa hivyo. Kwa hiyo tangia utume ombi la ajira, usaili mpaka kuanza kazi rasmi ni mchakato wa zaidi ya nusu mwaka. Jobless hatuna namna, ni kuwa watulivu tu na kuvumilia.
 
Back
Top Bottom