PSPF yashindwa kuwalipa wastaafu

PSPF yashindwa kuwalipa wastaafu

wao ndo wana mkataba wakudaiama mi huwa nikichukua statement zangu pesa haichelewi zaidi ya 3months
 
Pesa ktk kampeni tena hao wastafu ndio wengi walewale sasa hii nI tiba mbadala wengine waishobokee ssm ccm. Ndio wajue ccm wameshindwa kazi
 
Huu mfuko uko taabani sana kwa sasa, kuna jamaa yangu kaomba mkopo wa nusu pension tangu mwezi wa Tisa mwaka Jana. Kila siku anaambiwa hundi iko tayari lakini hakuna pesa. Ananiambia wako wengi kweli hadi imebidi wasitishe maombi mapya.


Kitu ambacho bado najiuliza, ni kwa nini hii pesa ya nusu pension wanaifanya mkopo tena inarudishwa kwa riba ya asilimia 13?

Imagine, mko watu wawili na wote mmefikisha umri wa miaka 55, wote mmepata sifa ya aidha kistaafu kwa hiari au kupokea nusu pension. Mmoja akisema anastaafu kwa hiari analipwa mafao yake yote kama kawaida. Mwingine akisema mi bado namalizia hii miaka 5 iliyobakia, ila naomba nusu yangu nijiandae, anaambiwa utapata lakini ni mkopo na tutakata asilimia 13 katika iliyobaki. Utakuwaje mkopo wakati ni fedha yangu, na nimechukua tu nusu nimewaachia nusu yangu mzalishie kwa miaka hii 5 ijayo? Si ningeichukua yote kama ningesema nastaafu kwa hiari?

Kwa maelezo mengine, anayakataa kustaafu kwa hiari, lakini akaona achukue nusu pension tu na aendelee kutunisha kiasi atakachopata pension kwa miaka 5 ijayo, hakuna anachoongeza kwani chochote kitakachoongezeka ndo hicho kitawarudia tena kama riba ya asilimia 13 kwa mwaka kwa hela yako mwenyewe uliyopewa kama mkopo.
 
Mashirika ya kijamii yamekuwa yakijitangaza kuwa yana huduma bora sana,mashirika haya ikiwa ni pamoja na PSPF.

Shirika hili lilikuwa linasifiwa kuliko mashirika yote ya huduma za kijamii.

Hata hivyo tumeona katika siku hizi za karibuni huduma za shirika hili zikidorora kwa kiwango kikubwa.

Kwa mfano wastahafu ambao walipaswa kulipa pension zao za kila mwezi angalau ilipofika tarehe moja ya mwezi wa nne mpaka leo hawajalipwa stahili yao.

Mashirika haya yakumbuke kwamba wastahafu hawa wanategemea pension hizi kwa kiwango kikubwa kama vile wafanyakazi wanavyotegemea mishahara yao. Na wakumbuke pia kwamba wastahafu hawa wameneemesha sana mashirika haya.

Ni swala la kiutu tu na uungwana kwamba inabidi watambue mchango wao na shirika hili liwe na mpango thabiti wa kuwalipa wazee hawa mapema. Ni watu waliolitumikia shirika hili kwa siku nyingi kwa hiyo ni vema wakaheshimiwa.

Tukiandika andika hivi mwishoni watapoteza wateja.

Wajirekebishe na watekeleze wajibu wao ipasavyo.

Kuna wazee nawafahamu wamestaaft mwaka jana ila mpaka leo hawajalipwa mafao yao. Hapo jaribu kupata picha ni namna gani pspf walivo wakatili. Wao wakistaafu wanalipana hapohapo ila wananchi maskini wakistaafu wanaanza kuwazungusha
 
Mimi sio kibarua wa NSSF.Kwanza NSSF ndiyo mbaya kuliko.Ila uache kudakia mambo usiyo yajua.Ni kweli PSPF haijawalipa wastahafu kwa kipindi cha April,May na Juni.Kama si kweli waje hapa wakanushe.Hii imewaweka wastahafu kwenye hali ngumu zaidi ya maisha,kwa vile hali yao tayari ni mbaya.Wewe nadhani ndiye kibarua wa PSPF kwa vile inaonekana unaipigia kifua PSPF.

Kazi nzuri ya ccm au wameshakopa sana huko nakukimbia

Pspf bana cjui tatzo ni nini pale ila naskia serikali imekopa sana hii mifuko

Serikali sikivu lazima imehakopa huko kwa ajili ya kununulia BVR

Nakumbuka CAG alishasema linaweza shindwa kulipa mafao.Pia trillioni 6 wanazolidai serikali sijui Kama zimerudi.

Haya Mashirika YANA pumulia Mashine ...Serikali inayakopa Sana ....na Zaidi wakuu wa haya mashirika ni Wezi Wezi Wezi .....wanabuni miradi ambayo ni white elephant ......na wana exaggerate gharama Za ujenzi ...sijui SSRA wanangoja nini au hawana Nguvu ....

Chakulia mfano ....shirika linaenda kujenga Jengo ILALA KWA Bilioni 76 ...Wakati Jengo Kama Hilo Hilo watu wanajenga kwa Bilioni 35
Ghorofa pale Moshi ambalo partition watafanya wapangaji ...unaambiwa limejengwa kwa Bilioni 70

Jengo ambalo limejengwa pale Makumbusho ..na lile la Ilala ...kwa kuangalia lipi imara na zuri na lenye facilities nyingi ....lakini Jengo la Ilala ( mzizima towers )eti ni la gharama kuliko la makumbusho

Unakuta Jengo Lina Majengo yako tupu ...lakini wakurugenzi au watu wao wa karibu ....wanajenga maghorofa Binafsi na Kupandisha makampuni wanayoyaongoza ....

Mtandao wa kulinda huu uovu ni Mpana Sanaa ..na Hilo mtaliona muda sio mrefu .

Ni kweli kuhusu uzuri wa formula ya tofauti za pensheni wanazotumia PSPF LAKINI formula hiyo hiyo ndiyo imeuchosha mfuko wa PSPF ndio maana sasa wanahaha kuwalipa wastaafu.....na kimahesabu(kwa uelewa wangu mdogo) walijipanga vizuri ila kuna factors mbalimbali hazikukaa sawa kama vile kukopwa na serikali fedha nyingi sana bila kulipwa nk (na siasa ndani yake)..hivyo ndio maana sasa wanayumba yumba sana!

Ni kweli kabisa mfuko wa PSPF una hali mbaya kifedha. Nimethibitisha hili hivi karibuni, baada ya kuwasiliana nao ili nijue kwanini wamekua wakimzungusha mzee wangu katika kupata mafao yake, baada ya kuwa amestaafu kwa muda mrefu sasa!

Bila kutafuna maneno, nilijibiwa kwamba fedha hakuna, wanasubiri hazina itakapopeleka makato ndipo waweze kulipa. Na kwamba haijulikani ni lini, ila niendelee tu kuwasiliana nao kila nitakapopata nafasi.

My take: Kwa kweli hali ni mbaya, Serikali inabidi ichukue hatua haraka iwezekanavyo, ili kunusuru wazee wetu hawa!

Hatima ya haya matatizo ni ipi? Wahusika naona kama wameziba masikio!

Hili ndo shirika lililochoka hasa. Mm nasikitikia wazee bora mm nliyeenda kutaka mkopo wa masomo nkaambiwa riba ni 7. 5asilimia huko mza nikaenda msoma wakasema sio hiyo ni 14%kwa mwaka wakacalculate na makato nikalinganisha na crdb yenye 18% tofauti ni ndogo sana. PSPF hawana nia ya dhati kutusaidia Bali kutuibia funny enough wanakwambia benki ya posta ndo inakupa mkopo haijalishi makato yako yanatosha kukukopesha .kumbe PSPF ni bankrupt kwa mujibu wa report ya CAG nadhani hela zimebebwa na serikali kwenye uchaguzi jamani jamani.

Ha ha ha Mama samia si ana matrillioni ya kugawa vijijini mwambieni awakopeshe PSPF
Sasa hizi ahadi zamagufuli anategemea kuzitimiza na nini ilihali JK ashakopa mpk mifuko ya ndani imeisha

Labda niongezee au nifafanue pale ulipoishia. Kwa PSPF Kuna Matatizo mawili, ambayo yote chanzo ni Serikali yetu iliyoko madarakani, na nitaelezea kama ifuatavyo;-

1) Pre-'99
Mwaka 1999 serikali iliuomba huu mfuko kuwachukua staff wake wengi tu na kuwasajili kwenye mfuko kana kwamba walikuwepo toka zamani (kabla ya (1999). Hivyo basi mfuko huu uliamua kuwaingiza kwenye database yake hata wale ambao hawakua wamechangia. Yaani mfano mtu kaanza kazi Serikalini tuseme mwaka 1985 na akachangia mafao yake hazina Mpaka mwaka 1998, mtu huyu alihamishiwa PSPF mwaka 1999 na labda kama atastaafu mwaka 2000, PSPF watamlipa mafao ya kuanzia mwaka 1985 ingawa kwao kachangia kuanzia 1999 tu.

Makubaliano haya yalikua kama ni Mkopo ambao hazina/serikali ingedaiwa na huu mfuko sababu mfuko unalipa mafao ambayo makato yake haukuyapokea, na toka ahadi au makubaliano hayo ya deni yafikiwe huo mwaka 1999, serikali haijawahi kuilipa huu mfuko ingawa mfuko umeendelea kuwalipa wastaafu mafao yao yote pamoja na pensheni Mpaka mwaka jana.

2) Monthly Salary Deductions
Hapa napo Kuna delays. Toka January mwaka huu, serikali imeshindwa kupeleka makato inayowakata wafanyakazi wake kwenye mishahara yao. Wewe ukipokea Pay slip yako inaonesha umekatwa PSPF ila in actual sense hiyo hela haijaenda bado kwa watu PSPF.

Deni la kwanza ambalo ni historical linatokana na fact kwamba ni kubwa mno, zaidi ya 1 trillion, hivyo serikali inayolia deficit kwenye bajeti yake kuondoa hela kama hii ni tatizo. Deni hili aliliacha mkapa, na dalili zote ni kua JK nae ataliacha, ingawa likiwa limeongezeka.

Na deni la pili nalo ni hiyohiyo deficit ya serikali, maana hata mishahara yenyewe ni kwa manati ingawa inalipwa.

Data hizi ni kutoka Hazina ambao ndio wadaiwa, hivyo hazina shaka kabisa

Ahsante kwa ufafanuzi wa kina mkuu, kuna watu humu wamezoea kupotosha kila ukweli kwa maslahi yao binafsi na waliowatuma. Bila kupima kwanza hasira wanazoweza kuziibua kutoka kwa wengine, ambao kimsingi ndio wahanga wa haya mambo!

Nafikiri sote kwa pamoja tuendelee kuisihi Serikali yetu ifanye linalohitajika kwasasa, ili kuwaondolea adha hii wazee wetu. Kwa kweli inatia uchungu sana, mzee anapoishi kwa matumaini, asijue ni lini hasa atafanikiwa kupata haki yake. Bado tuna imani na Serikali yetu, na kwakua imekua ikijitambulisha kwamba ni SIKIVU, MAHILI NA MAKINI, huu ndio wakati sasa wakudhihirisha hayo kwa vitendo.

Fedha za wastaafu ndo zinajenga maghorofa yaoo!!!

Pesa ktk kampeni tena hao wastafu ndio wengi walewale sasa hii nI tiba mbadala wengine waishobokee ssm ccm. Ndio wajue ccm wameshindwa kazi

Serikali ndio inakopa kutoka mifuko hii .
Ukopaji bila malipo unaweza ukafilisi mifuko ya jamii. Pia kuletea wastaafu kutokupata mafao yao.

Mpaka sasa serikali inadaiwa zaidi ya trilioni 1, Na bado inaendelea kukopa. Mikopo hii inaathiri uchumi wa Taifa, Je serikali itazilipaje fedha hizo?

Kwa bahati mbaya serikali inayokopa na kushindwa kulipa madeni Ñî serikali ya CCM.

Je utaipigia kura CCM?

Tafakari, chukua hatua. Ñî wakati wa madiliko.
 
Hapa mtoa mada wastaafu wanapata stahiki zao kila Mara kwa wakatii....
Tena kila ikifika wakati wa kupewa bila shida wanachukua nimekaa pale wazee wanasifia ule mfuko

Hahaha, watu kama ninyi hamuwezi kukosekana, hasa katika nyakati hizi..
 
PSPF wameshindwa kulipa mafao kwa wastaafu wa mwaka 2014, kiasi cha kusababisha wastaafu kuishi kwa shida sana, jamani PSPF lipeni mafao watumishi wa umma, wanapata shida sana.
 
CAG ishawahi sema pspf ni mfuko unaofilisika kwa kasi. Sababu serikali imekopa sana huko. Juzi rais kasema atalipa madeni yote ya pspf kabla ya kuondoka madarakani. Rais kabakiwa na kama mwezi mmoja hivi.
 
mabadiliko ni muhimu wakati huu... serikal kujenga maghorofa kwa penshen za watu wakati wenye hela wanashinda njaa
 
Pspf sio mfuko tena ni shati Tu. Ushafilisika na CAG na mkurugenzi wao Bwn. Adam mayingu alishasema hatua madhubuti isipochukuliwa utashindwa kumeet operation zake. Mfuko ni Lapf ndio mfuko bora kwa sasa na wenye asset za kutosheleza kulipa wanachama wake na kuwekeza. Ongera Bwn. Sanga kwa utendaji Wako uliotukuka ata kufanya wanachama kma Mimi kujivunia kuwa eneo salama na uhakika.
 
PPF mm nafuatilia mafao yangu mwezi wa pili sasa pale kinondon branch....wafanyakaz wako hovyo sana pale....hawajui wanachofanya ...
 
Oi wamekopwa na serikali wako hoi 😱😱
 
Back
Top Bottom