Ni kweli kabisa mfuko wa PSPF una hali mbaya kifedha. Nimethibitisha hili hivi karibuni, baada ya kuwasiliana nao ili nijue kwanini wamekua wakimzungusha mzee wangu katika kupata mafao yake, baada ya kuwa amestaafu kwa muda mrefu sasa!
Bila kutafuna maneno, nilijibiwa kwamba fedha hakuna, wanasubiri hazina itakapopeleka makato ndipo waweze kulipa. Na kwamba haijulikani ni lini, ila niendelee tu kuwasiliana nao kila nitakapopata nafasi.
My take: Kwa kweli hali ni mbaya, Serikali inabidi ichukue hatua haraka iwezekanavyo, ili kunusuru wazee wetu hawa!
Labda niongezee au nifafanue pale ulipoishia. Kwa PSPF Kuna Matatizo mawili, ambayo yote chanzo ni Serikali yetu iliyoko madarakani, na nitaelezea kama ifuatavyo;-
1) Pre-'99
Mwaka 1999 serikali iliuomba huu mfuko kuwachukua staff wake wengi tu na kuwasajili kwenye mfuko kana kwamba walikuwepo toka zamani (kabla ya (1999). Hivyo basi mfuko huu uliamua kuwaingiza kwenye database yake hata wale ambao hawakua wamechangia. Yaani mfano mtu kaanza kazi Serikalini tuseme mwaka 1985 na akachangia mafao yake hazina Mpaka mwaka 1998, mtu huyu alihamishiwa PSPF mwaka 1999 na labda kama atastaafu mwaka 2000, PSPF watamlipa mafao ya kuanzia mwaka 1985 ingawa kwao kachangia kuanzia 1999 tu.
Makubaliano haya yalikua kama ni Mkopo ambao hazina/serikali ingedaiwa na huu mfuko sababu mfuko unalipa mafao ambayo makato yake haukuyapokea, na toka ahadi au makubaliano hayo ya deni yafikiwe huo mwaka 1999, serikali haijawahi kuilipa huu mfuko ingawa mfuko umeendelea kuwalipa wastaafu mafao yao yote pamoja na pensheni Mpaka mwaka jana.
2) Monthly Salary Deductions
Hapa napo Kuna delays. Toka January mwaka huu, serikali imeshindwa kupeleka makato inayowakata wafanyakazi wake kwenye mishahara yao. Wewe ukipokea Pay slip yako inaonesha umekatwa PSPF ila in actual sense hiyo hela haijaenda bado kwa watu PSPF.
Deni la kwanza ambalo ni historical linatokana na fact kwamba ni kubwa mno, zaidi ya 1 trillion, hivyo serikali inayolia deficit kwenye bajeti yake kuondoa hela kama hii ni tatizo. Deni hili aliliacha mkapa, na dalili zote ni kua JK nae ataliacha, ingawa likiwa limeongezeka.
Na deni la pili nalo ni hiyohiyo deficit ya serikali, maana hata mishahara yenyewe ni kwa manati ingawa inalipwa.
Data hizi ni kutoka Hazina ambao ndio wadaiwa, hivyo hazina shaka kabisa