Prove me wrong Hakuna fundi tajiri.

Basi mafundi wa miaka hii hawataki mchakato kabisa.
 
 
Nionyeshe fundi tajiri nikupe ten.
Unamjua Thomas Lyimbo aliyekuwa anagawa maziwa shule za msingi maeneo ya Kimara na Ubungo mojawapo Ubungo Msewe?
Kiwanda chake Cha welding and metal fabrication kipo Kimara Korogwe pale?
Yule ambae alijikuta kwenye anga za FBI sababu ya kuwauzia gesi Al Qaida waliolipua ubalozi wa Marekani Dar Tanzania?
Huyo mmoja tu Ila wapo wengi.

Kaka yangu tumbo moja fundi magari alifanikiwa kujipata akamiliki gari na viwanja kadhaa, gari ya watalii cruiser extended body maarufu War bus.
Ghorofa, dula jumla kubwa la vinjwaji, duka la spare za gari, Car Wash, Bar, n.k.

Mwinge fundi maarufu wa kufunga sound system kwenye magari kule Arusha? Naye kajipata.

Nenda Gerezani Kariakoo kakutane na mafundi tajiri.
Kutoboa na utajiri inategemea juhudi zako na bahati yako.

Kuna matajiri mafundi body za gari na rangi waswahili, wachina, waarabu, na wahindi matajiri sana Dar na Arusha. Bado hujaenda Nairobi.
Kuna fundi electronics , computer n.k. ambao Ni matajiri Tena baadhi Ni authorized dealers wa brand kubwa Kama Dell, HP, Sony, Samsung n.k.
Mtazamo wako dhidi ya mafundi ni wa mafundi wale wa chini ya mwembe ambao wanajitafuta.
 
Mwambie akawatafute akina Motech au East cars....vijana kama hao wapo wengi wana maisha mazuri kwa ufundi tu. Tatizo yeye anafikiri fundi ni wale waliochafuka na grease tu.
 
Kijana hana exposure. Yupo ndani ya box.
 
Kweli itabidi nibadilishe mtazamo, mimi naowaona circle yangu ni mafundi wa chini ya muembe ambao ni 95% ya mafundi wote.
 
Mwambie akawatafute akina Motech au East cars....vijana kama hao wapo wengi wana maisha mazuri kwa ufundi tu. Tatizo yeye anafikiri fundi ni wale waliochafuka na grease tu.
Nimebadilisha mtazamo mkuu mimi nilikuwa naongelea mafundi wa chini ya muembe ambao ni 95% ya mafundi wote, ila ninachokiona kila fundi anaweza kuwa na Maisha mazuri endapo akitumia platform vizuri kujitangaza na kuaminika.
 
Kwani hapa bongo matajiri kwa jumla ni asilimia ngapi?
Kwa mujibu wa statistics ni asilimia 0.003% labda sikuweka vizuri au kuonesha utajiri wa namna gani, nachomaanisha ni mtu kuwa na standard ya kawaida ya maisha, nyumba, viwanja, asset mbalimbali, ambapo mimi cycle yangu sioni mafundi wakimiliki asset.
 
Kweli itabidi nibadilishe mtazamo, mimi naowaona circle yangu ni mafundi wa chini ya muembe ambao ni 95% ya mafundi wote.
Kila kitu hata kama utakua unalipwa milions of money kama huna akili ya kujiongeza ni bure....ninaye jamaa angu tulisoma wote afya ila mshikaji kabla hatujasoma baba ake ni fundi cherehani na yeye mshikaji alikua anajifunza kushona hivi ninavyokuambia mshikaji alipiga chuo chini now ni fundi mkubwa ana miliki duka la jumla la vifaa vya ushonaje na kwasasa ana agiza vitu kutoka china... Yeye anachukua tenda za mauniform nk now ana kaniacha mbali sana ana usagiri kajenga ana biashara zingine bajaji nk na hii nakuambia ni miaka 7 iliyopita tangu aanze jiatfuta.
 
Ishu nyingine kuna mama tunakaa nae mtaa mmoja yeye anatengeneza crisp za ndizi oya yule mama yuko njema kishenzi mzee na yeye crisp anauza kwa jumla akitengeneza hazikai zishabebwa zote kaajiri vijana anatengeneza usiku kucha...ana nyumba kadhaa na mafanikio kadhaa kasomeshaw awatoto mpaka chuo na wanajitegemea. Hivyo acha dharau kwakua wewe pengine una miliki pesa ya kula na kubadilisha nguo ..Maisha yana njia nyingi za kupiga hatua kwa mtu mwenye juhudi,uvumilivu ,bahati na anayejua kucontrol tamaa yake.
 

Maisha haya tabiriki mkuu. Huwezi kujua mtu ana asset kiasi gani, au huduma anayotoa inagusa watu wangapi.
 
Kazi ni mbaya au haina faida na wewe ukiwa tu huna malengo yako,

Unaweza hata ukawa unafagia barabara ila kama una malengo yako,utafika tu mbali,mfano unaweza kujipa 3 years unakua una save kiasi fulani kisha unaangalia ustaarabu mwingine,

Pia unaweza ukawa unalipwa mamilioni ila kama hujajiwekea mipango na kua na nidhamu ya fedha,huwezi kua na maendeleo,

Maisha yanahitaji nidhamu ya hali ya juu sana,pamoja na kujiwekea malengo.
 
Maisha ni akili yako tu babu bila mahesabu ya kuchambua venye utamiliki hela kaz yako tuh nikutumia tuh hela alafu unatarajia uwe tajiri utoke wap
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…