Propaganda za kidini zaanza Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Propaganda za kidini zaanza Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Phillemon Mikael, Nov 20, 2010.

 1. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #1
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Waraka maalum kwa Wakristo Zanzibar
  Wapendwa katika Bwana,
  NDUGU Wakristo umefika wakati tumeonelea kuwa ipo haja ya kuwaelezeni
  machache ili kuona maendeleo yetu na mafanikio tuliokwisha yapata hapa
  Zanzibar, yanaendelezwa na hayarudi nyuma kwa namna yoyote. Hapana
  shaka kuwa munaelewa kuwa idadi yetu hadi sasa ni ndogo sana na wengi
  wetu tungali katika kiwango na hadhi ya wahamiaji na sio Wazanzibar
  kama wanavyosema wenyewe.
  MAFANIKIO YETU
  KABLA kugusia yale ambayo tunahisi ndio lengo la waraka huu hapana
  budi kuwatajieni mambo machache ambayo tumefanikiwa kuyapata hadi
  sasa. Pamoja na jitihada zetu za muda mrefu bado tunapaswa tumsifu
  Bwana kwa msaada wake mkubwa kwetu dhidi ya maadui zetu. Tunaamini
  kuwa kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu, Bwana atatupa ushindi na
  mafanikio makuu zaidi ya haya na atawafumba macho maadui zetu wazidi
  kulala ili mipango yetu yote ya kuibadilisha Zanzibar kidemografia
  ifanikiwe katika kipindi kifupi kijacho. Mafanikio yetu yameenea
  katika kila upande – katika uchumi, siasa, huduma za jamii, umiliki wa
  ardhi, ujenzi, elimu na kadhalika ili kupata picha kamili ni vyema
  tuorodheshe kwa ufupi mafanikio hayo:
  Nafasi yetu kwa upande wa elimu imekuwa ya kuridhisha kupitia nafasi
  za serikali. Hivi sasa ni rahisi na limekua jambo la kawaida katika
  kila matangazo ya wito wa masomo kusikia majina ya Wakristo. Kati ya
  vijana 7 hadi 10 ni lazima upate vijana wawili hadi watatu kutoka
  katika makanisa yetu.
  Sambamba na matangazo ya elimu, vijana wetu wamekuwa wanapata nafasi
  nyingi za ajira katika serikali ya Zanzibar.
  Hali ya kutoelewana kisiasa baina ya Wazanzibari imetoa mwanya kwetu kuingiza vijana wa
  Kikristo wenye asili ya bara kwa wingi kwani wamekuwa wanaaminika
  zaidi kuliko vijana wa Zanzibar.
  Hali tulioieleza juu imetuwezesha kuwa na Wakristo wengi katika nafasi
  za juu serikalini na katika chama tawala. Hali hii ni lazima
  iendelezwe katika ngazi zote kwani ndiko kunako mambo mengi ya kila
  siku.
  Tumepata fursa ya kutumia Taasisi za serikali kwa uendeshaji wa ibada
  zetu. Hali hii imefanya tuzidi kukubaliwa na Waislamu na kuvumiliwa na
  inaweza kutupa nafsi ya kuwavuta katika NENO LA BWANA.
  Kwa upande wa mashamba (vijijini) tumepata wasaa mzuri wa kununua
  ardhi toka kwa Waislamu ambao hadi sasa bado hawajashtuka. Ardhi hizi
  zimetuwezesha kujenga makanisa kadhaa ambayo hapo awali hayakuwepo.
  Idadi ya skuli na vituo vyetu (ambavyo licha ya picha ya juu kuwa
  haviendeshwi kwa misingi ya Kikristo lakini kiukweli ni vituo vya
  kimisionari) vimeongezeka kwa hali ya kuridhisha. Skuli hizi ni
  kuanzia kwa watoto wadogo hadi vituo kama hichi kilichopo mji mkongwe
  (Stone Town Youth Centre) na zinafanya kazi vizuri katika kupandikiza
  mila za Kikristo.
  Sera zilizopo hivi sasa kwa upande wa uingiaji na utokaji Zanzibar
  imetusaidia sana katika uingizaji wetu (Wakristo) kutoka Bara na hivyo
  kusaidia kufuta ile imani ya kuwa Zanzibar ni kisiwa cha Waislamu eti
  Wazanzibari kwa zaidi ya asilimia 99 ni Waislamu.
  Ujaji wa Wakristo kwa wingi kutoka Bara umewezesha kuongezeka kwa
  idadi ya mabaa na kilabu za pombe. Hivi sasa ni jambo la kawaida kuona
  magari ya aina mbalimbali yanayomilikiwa na eti Waislamu yamebeba
  kreti za bia na pombe kali.
  Kujiingiza kwetu katika taasisi za dola katika ngazi za mitaa
  kumetuwezesha kupata nafasi ya kutangaza Ukristo kwa njia ya mihadhara
  na wakati huo huo kudhibiti mihadhara ya wazi ya Waislamu kwa kutumia
  madai ya kashfa na kutatanisha maelewano mazuri baina ya watu wa dini
  tofauti.
  Tumefanikiwa kupata viwanja vingi katika maeneo ya mjini ambayo
  yangali mapya. Maeneo haya ni kama Tomondo, Mombasa, Mwanakwerekwe na
  kadhalika ambayo tayari tumeshajenga makanisa yetu ingawaje kwa sasa
  hayajawa na waumini wengi wa kuyatumia na bado yanaonekana ni matupu.
  Ndugu wapendwa katika Bwana,
  Mafanikio hayo yasitufanye tukalewa na kusahau jukumu la kanisa la
  kuona kuwa utawala wa Bwana unashuka Zanzibar haraka iwezekanavyo.
  Kosa lolote utakalofanya hivi sasa litaweza kuturudisha hatua kadhaa
  na huenda nafasi hii tuliyonayo hivi sasa tusiipate kwa karne mpya
  ijayo.
  Mambo ya kufanya yanayotukabili ili kuimarisha nafasi yetu ni kuona
  yale tuliyokwisha yapata hayatutoki na kuyafanya dira kwa karne ijayo
  ni haya yafuatayo:
  Tusahau tofauti zetu dhidi ya adui
  Ingawaje tupo madhehebu nyingi lakini tunawajibika kuelewa kuwa
  Waislamu na Uislamu wao ni adui yetu namba moja ambaye hatutofaulu
  kupambana nae mmoja mmoja. Uislamu hapa Zanzibar ni dini iliofungamana
  na mila na utamaduni hivyo kila itakavyowezekana tusahau tofauti zetu
  ndogo ndogo na hata kubwa kukabiliana nao, vingienvyo tutarudi kama
  wakati wa Karume.
  Tuhakikishe tunapata ardhi
  Hii ni mbinu kongwe katika usambazaji wa Ukristo. Wazee wetu
  walipoleta Ukristo Zanzibar na katika Afrika, jitihada waliyofanya ni
  kupata ardhi kuwa kwa ajili ya ujenzi wa maeneo yetu, majengo ya
  hospitali, shule, zahanati na vituo vya chekechea, makanisa na
  kadhalika. Tunahitaji ardhi kubwa ili kuziweka huduma hizo mahala
  pamoja kwa ajili ya kueneza injili ya Bwana na Muokozi wetu.
  Tununue nyumba na viwanja kwa ujenzi wa Makanisa
  Inaonekana Waislamu wenye siasa kali na baadhi ya watendaji kwenye
  serikali wameanza kushtuka na ongezeko kubwa la makanisa katika kisiwa
  cha Unguja. Kuna dalili kuwa tunaweza kupata ugumu katika kupata
  viwanja kwa ajili ya makanisa. Njia tunayoweza kuitumia kwa muda huu
  ni kununuwa viwanja vitupu au nyumba za Waislamu kwa bei kubwa
  itakayowashawishi kuziuza na baadaye tukaweza kuvijenga au kugeuza
  nyumba hizo kuwa makanisa.
  Tujenge shule na hospitali kwa wingi
  Hizi ni taasisi ambazo tunaweza kueneza neno la Bwana kwa Waislamu
  walio wengi hapa Zanzibar. Kwa kutumia umaskini unaowakabili wengi ya
  Wazanzibari na uchache wa huduma hizo tunaweza kujitangaza vizuri,
  tujitahidi kutoa huduma nzuri kuweka vifaa vya kisasa kuweka bei
  ndogo, kuweka upendo ili vituo vya Waislamu au hata vile vya serikali
  visiweze kuvikaribia vyetu. Shule ni sehemu muhimu ya kupandikiza
  mafundisho yetu zaidi kwa watoto wadogo (Nursery).
  Tunadai muda zaidi katika vyombo vya habari (TV na Radio)
  Kwa muda mrefu sasa Uislamu na Waislamu wamehodhi vyombo hivi vya
  habari mbali na kuwa siku ya Ijumaa ambayo yote humilikiwa na vipindi
  vya Kiislamu vyombo hivyo hutenga siku nyingine kadhaa kwa vipindi vya
  Kiislamu na hata kuthubutu kutia adhana kila wakati wa sala hali hii
  inaudhi na inatoa picha ya wazi ya serikali kupendelea Uislamu
  ingawaje inadai kuwa haina dini. Wakati wa kusherehekea miaka 25 ya
  TVZ tulizungumzia suala hili lakini halikupata mtu wa kulifanyia kazi.
  Sasa tuhakikishe kuwa Ukristo unapata muda zaidi katika vyombo hivyo
  au Uislamu nao upunguziwe nafasi.
  Tuongeze mhadhara wa wazi
  Wakati Waislamu wamezuiliwa kufanya mihadhara ya wazi, sisi tujitahidi
  kuhakikisha kuwa mihadhara yetu inaongezeka kwa kiwango kikubwa. Kwa
  kuwa Waislamu hawahudhurii mihadhara hiyo, lazima tuone Wakristo wa
  mjini na mashamba wanahamasishwa na kupatiwa nyenzo ili kuhudhuria.
  Vipaza sauti vitumike kuhakikisha kuwa neno la Bwana linafika kila
  pahala. Mihadhara ifanyike karibu na nyumba, Misikiti na kwenye
  viwanja vya wazi.
  Tuendelee kutumia shule na sehemu za umma
  Ili kuwafanya Waislamu watuzoee na kuondosha chuki yao kwetu ni lazima
  kuendelea kutumia mashule na sehemu za umma zilizo wazi kwa mambo yetu
  ya ibada kwa kipindi kirefu hali hii inaweza kuwafanya washindwe kuona
  tofauti yetu na wao.
  Tufanye suala la uhamiaji Zanzibar kuwa jepesi
  Uzoefu unaonesha kuwa ni jambo gumu kuwabatiza Wazanzibari Waislamu.
  Hali hii inafanya ongezeko la Wakristo kuwa dogo au halipo kabisa
  ukitoa wale wanaozaliwa katika familia za Kikristo.
  Njia pekee ya kuhakikisha ongezeko la makanisa na taasisi zetu ni
  kuongezeka kwa Wakristo. Jambo hili litawezekana kwa kuingiza Wakristo
  wengi kutoka Tanzania Bara au wapagani ambao tutaweza kuwabatiza kwa
  kutumia udugu wetu wa kikabila au asili ya Bara. Kwa kuwatumia ndugu
  zetu waliomo serikalini (SMZ au SMT) tuhakikishe kuwa suala la
  uhamiaji linabakia wazi na rahisi na linaendelea kwa kila hali.
  Tuzuie jaribio lolote la kadi za uraia au vitambulisho
  Wakrsito tunapaswa kuelewa kuwa iwapo serikali ya Zanzibar itaamua
  kufanya chochote ili, kuwa na vitambulisho au kadi za uraia kwa
  Wazanzibari basi jambo hilo litaathiri sana mipango yetu ya muda mrefu
  kwa Zanzibar. Jitihada zozote za kuiimarisha Zanzibar kama Zanzibar na
  nje ya Utanzania ni lazima tuelewe kuwa Uislamu utapata nguvu na kuwa
  tishio kwa hapa Zanzibar na hata Bara. Iwapo tutawajibika kuunga mkono
  ni kadi za Uraia na vitambulisho vya Watanzania kwa ujumla na sio
  Zanzibar peke yake.
  Tujipenyeze na kushika nafasi muhimu
  Lazima tuelewe kuwa chama chochote cha siasa kinalenga kukamata
  serikali ili kiweze kutekeleza yale yanayoaminika kuwa mazuri kwa
  chama hicho. Tunapozungumzia vyama vya siasa kwa Zanzibar tunahusisha
  zaidi kwenye CCM na CUF. Watu wetu wamefaulu kuingia kwa wingi katika
  chama tawala na katika jumuiya zake.
  Tuunge mkono sera za utalii
  Hadi sasa wengi wa watalii wanaoingia Zanaibar hutokea nchi za
  Kikristo. Desturi za watalii hupingana na zile za Kizanzibari na hata
  za Kiislamu. Watalii wanasaidia kuongezeka kwa mabaa na vivazi ambavyo
  Waislamu wanataka visivaliwe hasa na wanawake.
  Tujenge mabaa na kuongeza pombe
  Waislamu wengi huchukia pombe na huweza kuhama iwapo duka la pombe au
  baa ipo karibu nao. Waislamu hatari ni wale wanaosoma na kupata muda
  wa kujishughulisha na dini yao.
  Pombe ni kitu ambacho humtoa Muislamu katika Uislamu wa vitendo na
  kumkaribisha na Ukristo.
  Uwafuate Wakristo waliosilimu ili warudie Ukristo
  Watu wa aina hii wanakuwa bado hawajatulia na mara nyingi huwemo
  katika matatizo. Pana haja ya kuwalenga watu hawa ili kuwarudisha
  kabla hawajatulia au kupata elimu nzuri. Matatizo yao ndipo mahala pa
  kuanzia ili Bwana atawateremshie roho ya utulivu. Uzima wa Ukristo ni
  kuwa na wafuasi wengi kadiri iwezekanavyo.
  Tuwafuate wanawake kwa misaada
  Jumuiya zisizo za kiserikali zinaungwa mkono duniani kote na hasa zile
  za wanawake na watoto tujiweke pamoja ili tuweze kuwavutia kwa jina la
  kuwasaidia.
  Tuongeze vituo vya mafunzo ya Kikristo
  Kituo cha vijana cha mji mkongwe (Stone Town Youth Center) kimekuwa
  kikifanya kazi yake vizuri kwani hadi sasa lengo lake la ndani bali
  halijaeleweka na vijana wanaohudhuria hapo kwa shughuli mbalimbali,
  jitihada zifanyike ili kuwa na vituo vya aina hii katika maeneo
  mengine. Lengo kuu liwe ni vijana na wanawake bila ya kuonesha dalili
  za kidini.
  Tuwaoe wanawake wao kwa kusilimu kimajina
  Jitihada za makusudi zifanyike ili kila itakapowezekana kuwaoa
  wanawake wa Kiislamu ili tuweze kuwabatiza baadae, njia nzuri iwapo
  patakuwa na ugumu ni kusilimu kiuongo ili kuruhusiwa kuwaoa wanawake
  wao.
  Tuanzishe NGOs na sisi tuwe viongozi
  Kwa kuwa hivi sasa wafadhili wengi wameonesha hamu ya kuzisaidia NGOs
  moja kwa moja badala ya serikali ni lazima tujitahidi kuunda jumuiya
  zetu ambazo zitawashirikisha Waislamu lakini uongozi wa juu ni lazima
  uwe mikononi mwetu. Hii itatuwezesha kuona sera zetu na malengo
  yanatelekezwa kwa kivuli hicho.
  Tujenge ukaribu na viongozi ili kuwadhibiti Waislamu
  Mambo yetu mengi yamekuwa yanakwenda vizuri katika maeneo mbalimbali
  baada ya wenzetu kuwemo katika kamati za masheha, na matawi ya vyama,
  na kamati za maendeleo za maeneo mbalimbali. Hali hii ni lazima
  iongezeke ili udhibiti wa shughuli za Waislamu uwe mzuri zaidi na
  wakati huo huo kuona kuwa mambo yetu yanakwenda yakiwa na baraka ya
  vyombo vya dola na vyama vya siasa.
  Tuwachonganishe Mashehe wenye msimamo mkali
  Mashehe wenye misimamo mikali wamekuwa ni tatizo kwa Ukristo kwani
  wana wafuasi wengi na wamekuwa wakisema wazi na kushutumu maendeleo
  yetu. Mashehe hao ni lazima wachonganishwe na serikali ili hali
  ikiruhusu wazuiliwe kuendesha shughuli zao. Wakati tukifanya hivyo
  hatuna budi kuwaunga mkono Mashehe wote ambao wamekuwa wakitusaidia
  kwa njia mbalimbali.
  Tulenge kuifuta Tabligh
  Pamoja na kuwa na Tabligh sio hatari moja kwa moja kwa Ukristo lakini
  bado inastahili kupigwa vita kwa sababu ina aina pekee ya mihadhara ya
  Waislamu inayoruhusiwa humu Zanzibar. Tabligh inaweza kuwazindua
  baadhi ya Waislamu ambao ni vema kubaki bila ya kuzinduliwa.
  Tudai turudishiwe taasisi zetu
  Serikali ya Zanzibar bado inaonekana kuwa ngumu katika milki ya
  makanisa, ardhi na taasisi zetu. Dalili za huko nyuma zilionekana
  nzuri kwani tulifanikiwa kupata hospitali yetu Walezo na eneo la
  Kiugani hata hivyo panakuwepo na ugumu wa kurudishwa shule zetu. Kwa
  kuwatumia wenzetu waliomo serikalini na baraza la wawakilishi
  tuzidishe harakati na madai ya taasisi zote zilizobaki.
  Tulete waumini kutoka mashamba kuanza makanisa
  Hivyo sasa pameibuka wasi wasi kuhusiana na wingi wa makanisa ambayo
  hayajapata waumini wa kuyajaza. Ili kuficha dosari hii na hoja kadhaa
  utaratibu uliopo hivi sasa chini ya baadhi ya makanisa ni lazima
  uungwe mkono. Wakristo wahamiaji wengi hufikia mashamba hivyo pawekwe
  na utaratibu wa kuwaleta mjini ili kujaza makanisa.
  Neno la mwisho
  Wapendwa katika Bwana.
  Miongozi hii ni mikubwa na inaweza kuwatisha baadhi ya waumini wa
  Kikristo hasa wale ambao bado hawajampokea Roho Mtakatifu vizuri. Hata
  hivyo, kwa uwezo wa Bwana Mungu wetu ni mpango rahisi. Suala la muhimu
  ni haya kufahamika na kila Mkristo apendae kumtumikia Bwana. Pia
  hatuna budi kuishukuru awamu ya nne ya serikali ya Mapinduzi ambao
  imefungua milango kwa Ukristo na kushuhudia ongezeko la makanisa.
   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Huu ndiyo ujinga mtupu wala aliyeandika hizi habari si Mkristo kwasababu aliyoandika si ya kweli. Tatizo la elimu ndogo ya zanzibar huwezi kusingizia udini wakati 99% ya wananchi wa zanzibar ni waislam. Vivilevile je ni kiongozi gani wa zanzibar mkristo anayejulikana?? hivyo hizo habari za viongozi si za kweli. Zanzibar hata kazi hakuna uchumi unategemea mgao wa 10% kutoka bara na Wanzanzibar wengi wanaoishi nchi za ulaya na marekani kutuma pesa. Kama mnatakaka kukuza elimu basi punguzeni ukubwa wa serikali na tumieni kiasi kikubwa cha 10% mnayopata kuendeleza elimu. Visingizio vya kidini havitafanya kazi na hii hoja inaonyesha ni jinsi gani wenzetu wanavyofikiria kama usikopata elimu nzuri.
   
 3. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Kuna kazi kubwa sana kuweza kumpropagate tai. Na mkristo halisi amefananishwa na tai. Hili bandiko linaloitwa waraka lina mkono wa wahadhiri wa kiislamu wale wanaoendesha mihadhara ya kukashifu ukristo. Propaganda hizi wanazotumia hapa ni za zamani sana japo wengine wataziona mpya. Poleni mujahidini wa kiislamu huko zenj.
   
 4. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,521
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Hujaeleweka vizuri
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,205
  Trophy Points: 280
  TISS at work huu ni upuuzi na aliyeandika ni mpuuzi kapoteza muda wake bure, huwezi kukuza ukristo kwa kuanzisha mabaa mengi na pombe nyingi au kuoa wanawake wa kiislamu. Huu ni mwendelezo wa Kikwete type emails na messages zenye kupandikiza sumu ya udini ili kuonyesha aliyoyazungumza juzi yana support, Kikwete aelewe kama aliruhusu mambo haya yafanyike kumsaidia wakati wa kampeni yataendelea kumla mwenyewe taratibu, mimi naelewa hakuna kitu kama hiki kinaweza kufanywa na mkristo kamili.
   
 6. Omukuru

  Omukuru JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Source please.
   
 7. R

  Rugemeleza Verified User

  #7
  Nov 20, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huu ni mwendelezo wa kampeni chafu za kutaka kuwagawa Watanzania. Ni lazima zilaaniwe kwa nguvu zote.Watu wanaoandika upuuzi kama huu ni lazima wafichuliwe na kuanikwa hadharani ili jamii iwajue. Wataalamu wetu wa teknolojia ya habari tusaidie tuweze kuwapata.
   
 8. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,205
  Trophy Points: 280
  Wafuchuliwe mara ngapi wakati baadhi ya wanaohusika kwenye propaganda ni kampuni ya mtoto wake.
   
 9. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Huu ni upuuzi ulioandaliwa na kikundi cha waislam uchwara kwa lengo la kuamsha hisia za kibaguzi Zanzibar. Mwislam wala mkristo wa kweli hawezi kuandika utumbo huu. Hivi inakuwaje mtu mwenye akili timamu akatulia na kuandika 'utumbo mrefu' kiasi hicho!!!! Ndiyo maana nchi hii haiendelei. Badala ya watu kufanya kazi za maana, wanatumia muda wao kuandika mambo yasiyo na mbele wala nyuma.

  Invisible, tafadhali tuondolee kiumbe huyu humu jf.
   
 10. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  kwanza natoa pongezi kwa PHILEMON MICHAEL kwa kuweza kutuletea waraka huu......mimi ni mkristo....lakini ndani ya ukristo hamna chuki kma zilizoandikwa humu...naungana na wachangia mada hapo juu kuwa HAUKUANDIKWA NA WAKRISTO bali WALETA UBAGUZI WA DINI NYINGINE.....!
  .."THE FAILED PROPAGANDA"........ mbona wanashindwa kueneza nyaraka halali za makanisa kama vile.."waraka kuhusu uchaguzi mkuu"
  WASHINDWE KWA JINA LA YESU.... YESU WETU SI WA VITU VYA DUNIANI.... SISI TU-WASAFIRI,MAKAO YETU NI MBINGUNI,HATUHANGAIKII YA DUNIANI, NA WALA VITA VYETU SI JUU YA DAMU NA NYAMA
   
 11. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #11
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280

  Huu ni waraka ambao unazunguka zanzibar..wenye lengo la kuibua chuki dhidi ya wakristo wachache ili watendeewe kama wanavyotendewa wakristo wachache wa IRAQ.........ni wazi haukuandikwa na mkristo...bali ni aya za kufikirika za wachochezi.

  Kuna chama ambacho wafuasi wake walipania kuwa wakishika dola watatekeleza yaliyomo humo ikiwamo kuchoma makanisa ,baa na kuwafukuza watanganyika.....sasa kwa kuwa hakikushika dola wafuasi wake wamekuja na mbinu hii ya kuibua hasira miongoni mwa wananchi ili waamke wenyewe kuyatekeleza hayo maudhui........

  kwa kuwa sherehe za harusi ya kishoga zinaendeelea TISS hawawezi kuamka kuyashughulikia haya zaidi ya mkuu wa nchi kulalama tu majukwaani!!!
   
 12. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  This is stupid! It reflects the level of understanding of the composer of ths episode.not a single christian can do ths.ukristo sio dini ya chuki na wakristo ni wastaarabu.Pamoja na wingi wa madhehebu ya kikristo,yet hakuna hata mojawapo laweza kuandika upuuzi huu.hii ni roho ya uchochezi inayotoka kwa shetwani.mnakera sana.ningekuwa na uwezo watu wa namna hii ningewahamishia kwenye sayari ya mars dunia yetu iendelee kubaki na amani.nawalaani watu wa jinsi hii1
   
 13. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 594
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60
  i dont buy it .....its 100 percent nonsense, yaani mtu kwa akili zake akae chini na kuanza kufikiri hayo maupuuzi;;; huyo aliyeandika hayo kwanza inaonyesha hajui hata misingi ya kikristo;;;;kweli mungu atuhurumie siamini kama naishi na kiumbe huyu nchi moja na namuita mwanainchi mwezangu.
   
 14. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 742
  Likes Received: 349
  Trophy Points: 80
  WOO si mchezo... Mbona jamii forums imechelewaaa sana hapa huo waraka siyo wa sasa hivi na wala siyo matokeo ya kampeni za kikwete hapa namtetea. huo waraka umeanza kutambaa katika mitaa ya znz naona mwishoni mwa 1999 au mwanzoni mwa 2000 na ninavyokumbuka ni mrefu sana lakini naona hapo umeekwa page kidogo. na nakumbuka hiyo NGO inayoitwa Stone Town Youth Centre ndiyo kwanza ilikuwa inaanzishwa miaka hiyo na ilikuwa maarufu sana na vijana wengi sana wakati huo walikuwa wanaenda hapo na ilikuwa na kiongozi wake alikuwa GOA lakini sasa hivi hiyo NGO haipo tena na miaka mingi sana imepotea.sasa huo waraka kusudio lake kwa vijana wa kiislamu wasiende pale.. sasa nashanga pale mnapomuhusisha kikwete na waraka huo.. tutajidi fitna za kidini katika jamii yetu ya kitanzania ingeneral lakini tusimsingizie mtu kama ni sababu au ni matokeo ya kampeni zake... kama kweli huo waraka ungekuwa na umesababishwa na chuki kwa nini kuanzia hapo 2000 idadi ya makanisa ZNZ yameongezeka mara 10 zaidi na mtu anipe ushahidi kama kuna kanisa lililochomwa moto?....
   
 15. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ushenzi huuu!
   
 16. shungurui

  shungurui JF-Expert Member

  #16
  Nov 20, 2010
  Joined: Sep 1, 2008
  Messages: 1,592
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Kipindi cha kuwadanganya watanzania kimeshapita,

  unataka watanzania waache kujadili maada zenye kujenga na kuendeleza taifa letu ,ili wajadili huo upuuzi wako.
   
 17. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #17
  Nov 20, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Nikuhakikishie mkuu kuwa hakuna mkristo mpuuzi wa kuandika kitu kama hicho. Hii imeandikwa na wapagani wanaotaka kuleta fujo za kidini visiwani.
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Nov 20, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  Wazanzibara ndiyo wameshika utamu huko Zenji na wale wazenji wao walie tu.....................na hawa wazanzibara ni kama sisi tu huku hawasumbuliwi sana na dini za watu na ndiyo maana kuanzia 1999 hadi leo hakuna vurugu za kidini huko........................pamoja na Mujahedina kuandika waraka huo wakijifanya ni wakristu..............................wakati siyo..................................mkristu hawezi kuandika propaganda siziso na mashiko kama huo waraka bomu kabisa.........................
   
 19. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #19
  Nov 20, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280


  umeadika vizuri sana kwa kueleza ukweli, lakini hapo kwenye nyekundu nadhani umesahahu kuwa kwenye miaka hiyo ya mwisho ya 90 na mwanzo wa 2000 kanisa lililipuliwa na bomu huko zanzibar, vuta kumbukumbu ama fatilia vizuri
   
 20. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #20
  Nov 20, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naona kuna watu wana hamu ya kuona Tz tunazichapa
   
Loading...