Propaganda Chafu za CHADEMA juu ya Rose Kamili, je wanajua madhara yake?

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau, hakika nimesikitishwa sana na huu upotoshwaji unaofanywa na vijana wa Kinondoni, dhidi ya mke wa Dr Slaa, Rose Kamili. Mtakumbuka kuwa Rose Kamili alikamatwa jana na Jeshi la polisi akitoa rushwa kwa wapiga kura wa Kalenga ili wamchague Grace Tendega wa CHADEMA. Rose Kamili wakati anakamatwa alikuwa na afya njema na hakupata madhara yoyote na ushahidi wa picha ni kwamba alipanda mwenyewe kwenye gari la polisi

Cha ajabu ni kwamba, baadhi ya vijana wa CHADEMA wakitumia ID ya Molemo, waliweka uzi humu JF kwamba hali ya Rose Kamili ni mbaya. Kwamba Rose Kamili amebakwa na vijana wa Green Guard. Kwamba Rose Kamili amepigwa sana na kwamba mipango imefanyika ili apelekwe KCMC Kwa matibabu zaidi.

Binafsi, nimesikitishwa sana hasa hiyo propaganda ya kubakwa. Hata kama lengo la uzi ule ni kutaka kubatilisha mashtaka ya kutoa rushwa yanayomkabili Rose Kamili, hakika neno kubakwa ni baya sana kutumika si tu kwa Rose kamili bali hata kwa mtu mwingine. Ataficha wapi sura yake huyu mama kwa huo uzushi wa kubakwa? Je atakuwa tena jasiri kusimama Bungeni kujadili hoja inayokuwa mbele yake?

Baada ya kufuatilia zaidi, nimegundua kuwa waliotengeneza propaganda hizo ni kundi la Josephine Mushumbusi ilikumharibia mke mwenzake. Nawashauri sana wanachadema kutafuta maneno ya kutengeneza. Hili la Rose Kamili kubakwa limekaa vibaya.

Ni hayo tu wakuu
 
Pichani shoto ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili akielekezwa sehemu ya kupita wakati wakiondoka ofisi za makao makuu ya CCM mjini Iringa jioni ya leo,akituhumiwa kukutwa akigawa fedha kwa Wanakijiji wa Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini,ambapo Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.

Ikiwa imebaki siku moja kabla ya uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga,Iringa Vijijini,Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili amekamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini akigawa Fedha kwa wanakijiji hao,akijua fika Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.

Mbunge huyo wa Chadema akipakizwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi kwa taratibu nyingine za kisheria.

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili akiwa ndani ya gari ya polisi mara baada ya kukakamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini akituhumiwa kugawa Fedha kwa wanakijiji
 
images
wal-gag65j.jpg
 
Unatudhibitishiaje Uchunguzi wako ni sahihi na kile kilichosemwa sio sahihi..
Mpaka sasa hizi ni pumba tu..
 
Chadema hakuna mtu wa maana wote wanawaza uongo na uzushi wakienda mbele kidogo wanawaza vita hawana jipya.

Yule mama kakamatwa akitoa rushwa eti leo wanapindisha mambo hiki chama vipi.
 
Unatudhibitishiaje Uchunguzi wako ni sahihi na kile kilichosemwa sio sahihi..
Mpaka sasa hizi ni pumba tu..
Kila kitu kipo wazi amaekamatwa katoa macho kama nini kama uliangalia kwenye vyombo vya habari jana ungemhurumia ni aibu sana kwa mwanamke kama yule kuzama kwenye rushwa mbaya kama ile.
 
Wadau, hakika nimesikitishwa sana na huu upotoshwaji unaofanywa na vijana wa Kinondoni, dhidi ya mke wa Dr Slaa, Rose Kamili. Mtakumbuka kuwa Rose Kamili alikamatwa jana na Jeshi la polisi akitoa rushwa kwa wapiga kura wa Kalenga ili wamchague Grace Tendega wa CHADEMA. Rose Kamili wakati anakamatwa alikuwa na afya njema na hakupata madhara yoyote na ushahidi wa picha ni kwamba alipanda mwenyewe kwenye gari la polisi

Cha ajabu ni kwamba, baadhi ya vijana wa CHADEMA wakitumia ID ya Molemo, waliweka uzi humu JF kwamba hali ya Rose Kamili ni mbaya. Kwamba Rose Kamili amebakwa na vijana wa Green Guard. Kwamba Rose Kamili amepigwa sana na kwamba mipango imefanyika ili apelekwe KCMC Kwa matibabu zaidi.

Binafsi, nimesikitishwa sana hasa hiyo propaganda ya kubakwa. Hata kama lengo la uzi ule ni kutaka kubatilisha mashtaka ya kutoa rushwa yanayomkabili Rose Kamili, hakika neno kubakwa ni baya sana kutumika si tu kwa Rose kamili bali hata kwa mtu mwingine. Ataficha wapi sura yake huyu mama kwa huo uzushi wa kubakwa? Je atakuwa tena jasiri kusimama Bungeni kujadili hoja inayokuwa mbele yake?

Baada ya kufuatilia zaidi, nimegundua kuwa waliotengeneza propaganda hizo ni kundi la Josephine Mushumbusi ilikumharibia mke mwenzake. Nawashauri sana wanachadema kutafuta maneno ya kutengeneza. Hili la Rose Kamili kubakwa limekaa vibaya.

Ni hayo tu wakuu

Asante kwa ufafanuzi mkuu, Uzushi ni jadi yao. Wamemdhalilisha sana MAMA ROSE.
 
Unatudhibitishiaje Uchunguzi wako ni sahihi na kile kilichosemwa sio sahihi..
Mpaka sasa hizi ni pumba tu..
Mkuu, hakika uongo ni ule wa akina Molemo kuwa hali ya huyo mama ni mbaya
 
Uzi ni pumba tupu toka lini uliwapenda chadema..
Hakika sijawahi wala sitarajii kupenda CHADEMA. Ila nalaani walichomfanyia mwana CHADEMA mwenzao. Pamoja kuwa Rose Kamili ni mwana chadema lakini pia ni mwanamke anayestahili heshima na kuthaminiwa utu wake
 
Back
Top Bottom