Professionals and amateurs (wajuzi na wanaridhaa)

.
IMG_20180320_143032_888.jpg
 
Mshana mada zako bwana huwa zinaniacha mdomo wazi, naomba nije PM tufanye dili la kwenda kuiba pesa benki maana kwa jinsi vyuma vilivyokaza naona hakuna namna sasa
 
Mkuu Mshana itakubidi ufungue chuo cha ujuzi wa ulimwengu na malimwengu.Tatizo ni ithibati ya chuo Ndali atatoa kweli!Kwa mara nyingine tena big up
Am humbled... [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Mshana mada zako bwana huwa zinaniacha mdomo wazi, naomba nije PM tufanye dili la kwenda kuiba pesa benki maana kwa jinsi vyuma vilivyokaza naona hakuna namna sasa
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] tunaweza kufanikiwa kuiba na kutoka salama lakini baada ya hapo ndio tutaanza kuishi maisha ya hofu na kutangatanga kama ndezi
Tutakimbia bila kukimbizwa
Tutaogopa hata vivuli vyetu
Tuyakosa imani hata kwa watu wetu wa karibu
Tutakuwa na wasiwasi na wageni
Simu ikiita tutashtuka... Ikiwa namba ngeni ndio kabisa hata kupokea itakuwa shida
Amani mioyoni itatoweka kuanzia asubuhi mpaka usiku
 
Tunashiriki mauaji kwa namna tofauti kutokana na vyakula tunavyokula... Kanuni ya survival of the fittest...
Tunashiriki mauaji kwa kutumia sumu na dawa mbalimbali
Tunashiriki mauaji kwa mawazo yetu.. Kutamani fulani afe.. Au kupanga mauaji kihisia tuu
Tunashiriki mauaji kwa matendo yetu kisiasa kijamii kimahusiano na hata kiimani
Usiwe unafafanua sana, waache wasomaji washughulishe bongo zao, spoonfeeding imepelekea uvivu wa kujitafutia maarifa kwa kizazi hiki
 
Sometimes cai hakuna namna
 
Kuna kitu kinaitwa fani na kuna kitu kinaitwa taaluma.. Ukiwa na taaluma kwenye fani fulani wewe si mtaaluma bali mtaalam... Kiingereza tunaita professional... Mimi nina taaluma na ujuzi wa mambo ya mochwari na mambo ya giza... Ni elimu rasmi nilizosomea darasani kwa kufundishwa na wanataaluma... Nimezisomea kiada na ziada...
Kuhitimu fani fulani ili uweze kujivunia na kutambulika Unahitaji kufanya mitihani na kufaulu kisha kutunukiwa daraja la kiwango cha fani yako... Kuna watu huwa wanasoma kufaulu mitihani na sio kuelewa... Kuna watu huwa wanatunukiwa daraja za juu za fani lakini wanakuwa hawajaelimika...

Mwanaridhaa ni mkosefu wa elimu.. Ni mkosefu wa fani... Anafanya tu kwa kujitolea ama kwa malipo kidogo... Mwanaridhaa kwa kiingereza ni amateur.. Anaweza akawa na ujuzi kwenye fani fulani... Lakini ni ujuzi kutokana na mazoea ama ujuzi nje ya mfumo rasmi wa kujifunza maarifa... Kuna wanaridhaa ni bora kuliko wajuzi wale wataalam wa kufaulu mitihani.... Wanaridhaa hawa ni wale ambao hawakusoma lakini wameelimika....

Taaluma na ujuzi vinatofautiana... Vyote ni muhimu lakini kuna vilivyo muhimu zaidi kuliko vingine.... Kuna baadhi ya fani hata ulale saa nane usiku na munde ya kutosha kichwani lakini asubuhi unaweza kuamka na kwenda kazini bila shaka... Lakini kuna taaluma kama hizi hapa chini ambazo kwa kiingereza tungeziita case sensitive

1. WALINZI WA VIONGOZI
kwanza ni lazima kutambua kwamba.. Wenye jukumu hili, lazima wawe askari lakini hupewa mafunzo maalum na ya ziada.. Yakiwemo kiwango kikubwa cha uvumilivu na kutunza siri... Hawa kazi zao hazitangazwi magazetini... Na hupitia mchakato mrefu mpaka kuja kuaminika na kukubalika... Ni watu wa kupangiwa mpaka sehemu za kutembelea nk.. Hawa ndio kama roho ya kiongozi... Ni kaliba inayopewa umuhimu mkubwa na wa kipekee mno.. Kwa kiasi kikubwa hawatakiwi kuwa na msongo wa mawazo....

2.WANYONGAJI
Hapo juu tumeona walinzi wa uhai hapa chini ni watoa uhai... Hapa anaweza kuwa mtu yoyote lakini mwenye huruma na rohongumu kwa wakati mmoja... Sio lazima awe katili... Mafunzo yao ni rahisi lakini magumu... Namna ya kukatisha uhai wa mtu... Yaani kutoa roho.. Kuua. Ama kwa kunyonga kwa kamba, kuchinja kwa kisu au upanga, risasi na hata kutumbukiza kwenye pipa la tindikali
Linapotokea jukumu la kutimiza wajibu wake huandaliwa mapema na kupewa vitu vitakavyomsahaulisha fikra zote juu ya kile anachotarajia kukifanya.... Ajira zao ni za siri na ni chache mno

3. WAHUDUMU WA CHUMBA CHA MAITI
Ajira ya ujuzi pia hii lakini inayoogopwa na wengi... Hapa kuna WAHUDUMU wajuzi na WAHUDUMU wa ridhaa... Ukiachana na elimu juu ya kutunza mwili na hatua zote tangu kupokea maiti mpaka kuikabidhi kwa ajili ya mazishi... Lakini pia ujasiri roho ngumu na kutokuwa mwoga ni vigezo vingine muhimu vinavyomfanya mtu aweze kupata kazi.. Hawa wanaruhusiwa (sio rasmi) hata kutumia vilivyoharamishwa(sio madawa ya kulevya) ili akili zao ziweze kukaa sawa...

4. WASAFIRISHA PESA
Hawa kwanza ni lazima wawe na taaluma ya uaskari na jeshi, walenga shabaha na wadunguaji... Wenye maamuzi ya mara moja na haraka... Macho imara na wasio na taharuki... Kumbuka siongelei WASAFIRISHA pesa kidogo... Zile pesa za nchi kwenye maroli yenye ving'amuzi yasiyopenya risasi nk
Kabla ya msafara.. Wahusika huandaliwa mapema... Walale wapumzike vya kutosha... Wasiwe na msongo wa mawazo.. Wasiwe na njaa ama shibe wala kiu... Muda ni kitu muhimu kuliko vyote.. Gari hukaguliwa na timu ya mafundi mahiri... Mabunduki hukokiwa kabisa...
Dereva anapangiwa mwendo wa kwenda wapi mpaka wapi aende mwendokasi gani... Askari wasindikizaji macho huwa pima na smg mikononi... Wanakaa hivyo muda wote wa safari... Na wanatakiwa kuwa imara muda wote bila kusinzia

Kuna makundi mengine kama ya wanasayansi na wataalam wa kemikali.. Nao ni watu wa kulindwa na wenye miiko na masharti mengi.... Lakini kama umegundua kitu kwenye huu uzi uhai na pesa ndio vinapewa kipaumbele zaidi kuliko vingine vyote... Kwakuwa bila uhai hakuna pesa na bila pesa hakuna uhai.....
Kilichonishangaza sana ni kwamba SIASA SIO KAZI YA UJUZI
Uana siasa ni kazi ya kuwaweka wananchi "sawa".
 
IMEKAAJE HII
bachelor of arts degree in political science and philosophy
 
Back
Top Bottom