Kuna kitu kinaitwa fani na kuna kitu kinaitwa taaluma.. Ukiwa na taaluma kwenye fani fulani wewe si mtaaluma bali mtaalam... Kiingereza tunaita professional... Mimi nina taaluma na ujuzi wa mambo ya mochwari na mambo ya giza... Ni elimu rasmi nilizosomea darasani kwa kufundishwa na wanataaluma... Nimezisomea kiada na ziada...
Kuhitimu fani fulani ili uweze kujivunia na kutambulika Unahitaji kufanya mitihani na kufaulu kisha kutunukiwa daraja la kiwango cha fani yako... Kuna watu huwa wanasoma kufaulu mitihani na sio kuelewa... Kuna watu huwa wanatunukiwa daraja za juu za fani lakini wanakuwa hawajaelimika...
Mwanaridhaa ni mkosefu wa elimu.. Ni mkosefu wa fani... Anafanya tu kwa kujitolea ama kwa malipo kidogo... Mwanaridhaa kwa kiingereza ni amateur.. Anaweza akawa na ujuzi kwenye fani fulani... Lakini ni ujuzi kutokana na mazoea ama ujuzi nje ya mfumo rasmi wa kujifunza maarifa... Kuna wanaridhaa ni bora kuliko wajuzi wale wataalam wa kufaulu mitihani.... Wanaridhaa hawa ni wale ambao hawakusoma lakini wameelimika....
Taaluma na ujuzi vinatofautiana... Vyote ni muhimu lakini kuna vilivyo muhimu zaidi kuliko vingine.... Kuna baadhi ya fani hata ulale saa nane usiku na munde ya kutosha kichwani lakini asubuhi unaweza kuamka na kwenda kazini bila shaka... Lakini kuna taaluma kama hizi hapa chini ambazo kwa kiingereza tungeziita case sensitive
1. WALINZI WA VIONGOZI
kwanza ni lazima kutambua kwamba.. Wenye jukumu hili, lazima wawe askari lakini hupewa mafunzo maalum na ya ziada.. Yakiwemo kiwango kikubwa cha uvumilivu na kutunza siri... Hawa kazi zao hazitangazwi magazetini... Na hupitia mchakato mrefu mpaka kuja kuaminika na kukubalika... Ni watu wa kupangiwa mpaka sehemu za kutembelea nk.. Hawa ndio kama roho ya kiongozi... Ni kaliba inayopewa umuhimu mkubwa na wa kipekee mno.. Kwa kiasi kikubwa hawatakiwi kuwa na msongo wa mawazo....
2.WANYONGAJI
Hapo juu tumeona walinzi wa uhai hapa chini ni watoa uhai... Hapa anaweza kuwa mtu yoyote lakini mwenye huruma na rohongumu kwa wakati mmoja... Sio lazima awe katili... Mafunzo yao ni rahisi lakini magumu... Namna ya kukatisha uhai wa mtu... Yaani kutoa roho.. Kuua. Ama kwa kunyonga kwa kamba, kuchinja kwa kisu au upanga, risasi na hata kutumbukiza kwenye pipa la tindikali
Linapotokea jukumu la kutimiza wajibu wake huandaliwa mapema na kupewa vitu vitakavyomsahaulisha fikra zote juu ya kile anachotarajia kukifanya.... Ajira zao ni za siri na ni chache mno
3. WAHUDUMU WA CHUMBA CHA MAITI
Ajira ya ujuzi pia hii lakini inayoogopwa na wengi... Hapa kuna WAHUDUMU wajuzi na WAHUDUMU wa ridhaa... Ukiachana na elimu juu ya kutunza mwili na hatua zote tangu kupokea maiti mpaka kuikabidhi kwa ajili ya mazishi... Lakini pia ujasiri roho ngumu na kutokuwa mwoga ni vigezo vingine muhimu vinavyomfanya mtu aweze kupata kazi.. Hawa wanaruhusiwa (sio rasmi) hata kutumia vilivyoharamishwa(sio madawa ya kulevya) ili akili zao ziweze kukaa sawa...
4. WASAFIRISHA PESA
Hawa kwanza ni lazima wawe na taaluma ya uaskari na jeshi, walenga shabaha na wadunguaji... Wenye maamuzi ya mara moja na haraka... Macho imara na wasio na taharuki... Kumbuka siongelei WASAFIRISHA pesa kidogo... Zile pesa za nchi kwenye maroli yenye ving'amuzi yasiyopenya risasi nk
Kabla ya msafara.. Wahusika huandaliwa mapema... Walale wapumzike vya kutosha... Wasiwe na msongo wa mawazo.. Wasiwe na njaa ama shibe wala kiu... Muda ni kitu muhimu kuliko vyote.. Gari hukaguliwa na timu ya mafundi mahiri... Mabunduki hukokiwa kabisa...
Dereva anapangiwa mwendo wa kwenda wapi mpaka wapi aende mwendokasi gani... Askari wasindikizaji macho huwa pima na smg mikononi... Wanakaa hivyo muda wote wa safari... Na wanatakiwa kuwa imara muda wote bila kusinzia
Kuna makundi mengine kama ya wanasayansi na wataalam wa kemikali.. Nao ni watu wa kulindwa na wenye miiko na masharti mengi.... Lakini kama umegundua kitu kwenye huu uzi uhai na pesa ndio vinapewa kipaumbele zaidi kuliko vingine vyote... Kwakuwa bila uhai hakuna pesa na bila pesa hakuna uhai.....
Kilichonishangaza sana ni kwamba SIASA SIO KAZI YA UJUZI
Swali la kizushi.Wanataaluma husomea miaka mingi,mwanataaluma alieanzisha hizo taaluma nani alimfundisha na kumthibitisha ? Kama kuna mtaaluma aliejianzishia kozi kwa nini wasio somea miaka mingi taaluma hio wawe hawana taaluma hali kuna mwenzao aliewaanzishia hizo kozi ?.Mfano.Bill gate alitengeneza window hakuwa mtaaluma,vyuo vikachikuwa window vikaifanya taaluma.Mimi nikijifunza nyumbani sikubariki kama mtaaluma kisa sikufundishwa darasani kwa nini?
Mtazamo wangu: Taaluma na wanataaluma ni mfumo wa serikali wa kudhibit elimu lakini elimu ni kitu huru kipo tu hivyo mtu yeyote anaweza kukipata kwa kusomea au kujisomea nyumbani.Kampuni za ulaya zilishagundua kuwa mfumo wa taaluma hauna maana hivyo zinaajiri hata wasio wanataaluma(google)
Ilitakuwa kuwepo mfumo wa kuthibitisha mtu(interview) kama anaweza kufanya hicho kitu kwa asilimia zinazotakiwa au la.
Naamini mwishoni mwa karne ya 21 na nwanzoni nwa karne ya 22 mfumo wa taaluma utakuw hauna maana.Watu watautupilia mbali.
Karne ya 21 elimu ipo kiganjani bado dunia inafuata mfumo wa elimu ulioanzishwa kabla ya kristo(ajabu kabisa).
Mifumo mingi imepitwa na wakati,Mfano mifumo ya serikali imepitwa na wakati Tunatakiwa tubuni mifumo ya serikali inayoendana na sayansi na teknolojia na sio mifumo ya kina Plato na Karl max.Wakifufuka hao jamaa watatushangaa sana kuona bado tunatumia mifumo yao iliopitwa na wakati katika zama za kiteknolojia.
Tumeaminishwa kila kilichoanzishwa na watu wa zamani kimekamilika(Complete and no caught!), mfano bible na qurani hutakiwi kuvipinga ukibainika unafungwa eti having Shaka ! huu ni ujinga wa karne ya 21.
Dunia imejaa wajinga wengi sana japo wamekariri mawazo hayo ya kale.