Professionals and amateurs (wajuzi na wanaridhaa)

Professionals and amateurs (wajuzi na wanaridhaa)

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,551
Reaction score
860,698
Kuna kitu kinaitwa fani na kuna kitu kinaitwa taaluma.. Ukiwa na taaluma kwenye fani fulani wewe si mtaaluma bali mtaalam... Kiingereza tunaita professional... Mimi nina taaluma na ujuzi wa mambo ya mochwari na mambo ya giza... Ni elimu rasmi nilizosomea darasani kwa kufundishwa na wanataaluma... Nimezisomea kiada na ziada...
Kuhitimu fani fulani ili uweze kujivunia na kutambulika Unahitaji kufanya mitihani na kufaulu kisha kutunukiwa daraja la kiwango cha fani yako... Kuna watu huwa wanasoma kufaulu mitihani na sio kuelewa... Kuna watu huwa wanatunukiwa daraja za juu za fani lakini wanakuwa hawajaelimika...

Mwanaridhaa ni mkosefu wa elimu.. Ni mkosefu wa fani... Anafanya tu kwa kujitolea ama kwa malipo kidogo... Mwanaridhaa kwa kiingereza ni amateur.. Anaweza akawa na ujuzi kwenye fani fulani... Lakini ni ujuzi kutokana na mazoea ama ujuzi nje ya mfumo rasmi wa kujifunza maarifa... Kuna wanaridhaa ni bora kuliko wajuzi wale wataalam wa kufaulu mitihani.... Wanaridhaa hawa ni wale ambao hawakusoma lakini wameelimika....

Taaluma na ujuzi vinatofautiana... Vyote ni muhimu lakini kuna vilivyo muhimu zaidi kuliko vingine.... Kuna baadhi ya fani hata ulale saa nane usiku na munde ya kutosha kichwani lakini asubuhi unaweza kuamka na kwenda kazini bila shaka... Lakini kuna taaluma kama hizi hapa chini ambazo kwa kiingereza tungeziita case sensitive

1. WALINZI WA VIONGOZI
kwanza ni lazima kutambua kwamba.. Wenye jukumu hili, lazima wawe askari lakini hupewa mafunzo maalum na ya ziada.. Yakiwemo kiwango kikubwa cha uvumilivu na kutunza siri... Hawa kazi zao hazitangazwi magazetini... Na hupitia mchakato mrefu mpaka kuja kuaminika na kukubalika... Ni watu wa kupangiwa mpaka sehemu za kutembelea nk.. Hawa ndio kama roho ya kiongozi... Ni kaliba inayopewa umuhimu mkubwa na wa kipekee mno.. Kwa kiasi kikubwa hawatakiwi kuwa na msongo wa mawazo....

2.WANYONGAJI
Hapo juu tumeona walinzi wa uhai hapa chini ni watoa uhai... Hapa anaweza kuwa mtu yoyote lakini mwenye huruma na rohongumu kwa wakati mmoja... Sio lazima awe katili... Mafunzo yao ni rahisi lakini magumu... Namna ya kukatisha uhai wa mtu... Yaani kutoa roho.. Kuua. Ama kwa kunyonga kwa kamba, kuchinja kwa kisu au upanga, risasi na hata kutumbukiza kwenye pipa la tindikali
Linapotokea jukumu la kutimiza wajibu wake huandaliwa mapema na kupewa vitu vitakavyomsahaulisha fikra zote juu ya kile anachotarajia kukifanya.... Ajira zao ni za siri na ni chache mno

3. WAHUDUMU WA CHUMBA CHA MAITI
Ajira ya ujuzi pia hii lakini inayoogopwa na wengi... Hapa kuna WAHUDUMU wajuzi na WAHUDUMU wa ridhaa... Ukiachana na elimu juu ya kutunza mwili na hatua zote tangu kupokea maiti mpaka kuikabidhi kwa ajili ya mazishi... Lakini pia ujasiri roho ngumu na kutokuwa mwoga ni vigezo vingine muhimu vinavyomfanya mtu aweze kupata kazi.. Hawa wanaruhusiwa (sio rasmi) hata kutumia vilivyoharamishwa(sio madawa ya kulevya) ili akili zao ziweze kukaa sawa...

4. WASAFIRISHA PESA
Hawa kwanza ni lazima wawe na taaluma ya uaskari na jeshi, walenga shabaha na wadunguaji... Wenye maamuzi ya mara moja na haraka... Macho imara na wasio na taharuki... Kumbuka siongelei WASAFIRISHA pesa kidogo... Zile pesa za nchi kwenye maroli yenye ving'amuzi yasiyopenya risasi nk
Kabla ya msafara.. Wahusika huandaliwa mapema... Walale wapumzike vya kutosha... Wasiwe na msongo wa mawazo.. Wasiwe na njaa ama shibe wala kiu... Muda ni kitu muhimu kuliko vyote.. Gari hukaguliwa na timu ya mafundi mahiri... Mabunduki hukokiwa kabisa...
Dereva anapangiwa mwendo wa kwenda wapi mpaka wapi aende mwendokasi gani... Askari wasindikizaji macho huwa pima na smg mikononi... Wanakaa hivyo muda wote wa safari... Na wanatakiwa kuwa imara muda wote bila kusinzia

Kuna makundi mengine kama ya wanasayansi na wataalam wa kemikali.. Nao ni watu wa kulindwa na wenye miiko na masharti mengi.... Lakini kama umegundua kitu kwenye huu uzi uhai na pesa ndio vinapewa kipaumbele zaidi kuliko vingine vyote... Kwakuwa bila uhai hakuna pesa na bila pesa hakuna uhai.....
Kilichonishangaza sana ni kwamba SIASA SIO KAZI YA UJUZI
 
Hata mjinga anaweza kuwa mwanasiasa..
downloadfile-3.jpg
 
Zamani nilikuwa nikitoka kwenye kazi zangu za pesa nilikuwa na Rafiki jinsia ya Kike kila nikilalamika anasema Mimi kazi yangu rahisi sana, Yeye anafanya kazi ya Kubalance maiti zinazoingia na kutoka sasa Shughuli inakuja kuna siku hazibalance kabisa aidha Zimepungua au Zimezidi sasa kumkabidhi mwenzako ndio utata unaanza hapo, Tangu hapo nikiona mtu anasema amechoka na kazi huwa nacheka sana alinijenga sana kuona kazi sio ngumu bali ni dhana tu
 
leo utakuwa umekula ile kitu inayokoroma! hongera kwa uzi mzuri...
 
Zamani nilikuwa nikitoka kwenye kazi zangu za pesa nilikuwa na Rafiki jinsia ya Kike kila nikilalamika anasema Mimi kazi yangu rahisi sana, Yeye anafanya kazi ya Kubalance maiti zinazoingia na kutoka sasa Shughuli inakuja kuna siku hazibalance kabisa aidha Zimepungua au Zimezidi sasa kumkabidhi mwenzako ndio utata unaanza hapo, Tangu hapo nikiona mtu anasema amechoka na kazi huwa nacheka sana alinijenga sana kuona kazi sio ngumu bali ni dhana tu
Kumbe nao wana balance sheet kama wahasibu?
 
una taaluma ya mochwari na nguvu za giza... upo kwenye ubora wako mshana jr... nataka kujua tofauti kati ya mchawi na mganga wa kienyeji wale wapiga ramli?? mshana
Mchawi anaharibu mganga anaponya... Mchawi ni sumu mganga ni dawa ya sumu... Mchawi hawezi kuwa mganga lakini mganga anaweza kuwa mganga halafu mchawi
 
Back
Top Bottom