Amigoh
JF-Expert Member
- May 15, 2016
- 2,029
- 2,926
Kwa hiyo wewe profesa ulietetea wizi wa fedha za Escrow kwa nguvu nyingi mpaka ukatukana watu ni matumbili leo hii unapata wapi ujasiri wa kutuambia watanzania kuwa umeme maji unachelewa kuanza kuzaa faida na umepitwa na wakati?
Kwa hiyo huko Usa na China ambazo ni nchi zilizoendelea kwa kila namna wanapojenga Hydropower stations au kuendelea kutumia HEP kuzalisha umeme ni watu wasio na uelewa wa mambo?
Lini ilishawahi kutokea kupata nishati kama umeme ikawa ni fasheni ya kudai HEP imepitwa na wakati na sasa tutumie gas? Au unaleta dharau zako?
Hasira za wewe kufukuzwa uwaziri kisa tu ulishazoea kupiga madili makuwa hapo wizara ya nishati isiwe sababu ya kutuharibia mipango ya kukamilisha JNHPP. Kaaa kimya uendelee kutafuna posho za Escrow.
Kama kweli ujenzi huo umepitwa na wakati Ethiopia isinge thubutu kufanya maamuzi magumu kiasi ambacho umepelekea kugombana na Misri Hali iliyopelekea kuwa na vuguvuga la Vita.. @ProfesaMuongo