Kalemani akunwa na Kasi ya Ujenzi wa mradi wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP)

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1568037511387.png

1568037544055.png

1568037573258.png

KASI ya ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani “imemkuna” Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani baada ya kutembelea eneo la mradi huo Jumapili Septemba 8, 2019 na kukuta hatua muhimu ya ujenzi wa ADIT (njia ya kufika kwenye mifereji mikubwa ya kuchepusha maji) (diversion tunnel), pamoja na miundombinu wezeshi ikiwa imekamilika.

Sambamba na kupigwa kwa hatua hizo muhimu katika utekelezaji wa mradi huo uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Julai 26, 2019 na ambao utazalisha Megawati 2115, pia amepongeza usimamizi na utawala katika mradi huo.

“Hii ni mara yangu ya nane kutembeela mradi huu tangu uanze, leo nimetembelea ili kuangalia masuala makubwa matatu, kasi ya ujenzi, usimamizi na utawala na masuala yote ya ujenzi wa miundombinu wezeshi ili kuona kama imekaa sawasawa.” Alisema Dkt. Kalemani.

Alisema baada ya kuangalia masuala hayo amefurahishwa na hatua iliyofikiwa ambapo amewapongeza wasimamizi wa mradi huo TANESCO na TANROADS ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alitoa maelekezo kuwa lazima ujenzi huo usimamiwe na Watanzania wenyewe na ukamilike katika muda uliopangwa ambao ni miezi 42, ambapo miezi 36 ni ya ujenzi na miezi 6 ya mobilization kwa maana ya maandalizi ya vifaa na watumishi ambapo kazi ilianza Juni 15, 2019 na kazi inakwenda vizuri.” Alifafanmua Dkt. Kalemani.

Akifafanua zaidi Dkt. Kalemani alisema hadi sasa tayari wakandarasi wamekwishatumia miezi nane 8 kati ya 42 na kazi ambazpo zilikuwa zinaendelea kufanyika ni ujenzi wa njia za kuchepusha maji ardhini (diversion tunnel), nilikuja Julai 22, 2019 na nikaelekeza kazi hii ifanyike ndani ya siku 45 na ikamilike. ADIT hiyo yenye urefu wa wa Mita147.6 nashukuru wamemaliza na wameokoa siku 7 kabla ya muda niliotoa.

Mheshimiwa Dkt. Kalemani pia alisisitiza kuwa ni matumaini ya serikali kwamba wakandarasi watamaliza kazi ya ujenzi ndani ya muda na kwamba hakuna muda utakaoongezwa.
“Nimatarajio yetu mkataba unaisha Juni 14, 2022 na nimatumaini yetu pia watatukabidhi mradi huo siku hiyo saa 9;30 alasiri ili na mimi niukabidhi kwa Watanzania.” Alisisitiza na kuongeza…asitokee mtu atakaejaribu kuuchelewesha mradi huo, sisi kama serikali tutahakikisha tunaanza kumchelewesha yeye kwanza kabla hajatuchelewesha sisi kukamilisha mradi huo muhimu kwa taifa letu.” Alionya.

Alisema mradi huo wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni muhimu, bwawa hilo ni kubwa sana aliwataka Watanzania kutunza vyanzo vya maji yanayoelekea kwenye mto Rufiji ili kuwepo uhakika wa upatikanaji wa maji ya kutosha ni bwawa hili litahitaji maji kwenye ujazo wa mita za ujazo bilioni 33.2 hivyo maji ya kutosha yatahitajika.

"Bwawa hili ni kubwa kati ya mabwawa 70 duniani bwawa la JNHPP ni bwawa mojawapo, kati ya mabwawa manne makubwa Afrika bwawa hili ni mojawapo na ni la kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki kwa hivyo Watanzania wanayo kila sababu ya kujivunia na ni wajibu wetu kuyinza na kuhifadhi vyanzo vuya maji." Alisisitiza.

Alisema manufaa ya mradi huo ni pamoja na kuongeza umeme kwenye gridi ya taifa, kusambaza umeme vijijini na kwenye viwanda, pia utasaidia sana kupunguza uharibifu wa mazingira.

Awali akitoa taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo yaliyofikiwa hadi sasa tangu uzinduliwe na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mratibu wa Mradi huo Mhandisi Steven Manda ambaye pia ni Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) alisema, pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa handaki la kuchepusha maji, pia daraja namba mbili kwa maana ya miundombinu wezeshi nalo limekamilika na sasa mashine kubwa na vifaa vya ujenzi vinavushwa kutoka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili kupitia daraja hilo.
 
Nazidi muombea Rais Azidi kupiga kazi
Na kamwe asisikilize Makelele ya Walevi na Vibendera wachache
Ma milioni ya watanzania tuna muelewa saaana
 
Julius Nyerere Airport
Julius Nyerere Bridge
Nyerere Road

halafu na hii Nyerere nini?
Nyerere airport
Nyerere bridge
Nyerere road
Nyerere convection center
Nyerere leadership college
Nyerere national park
Nyerere hydroelectric power project
Mwalimu nyerere foundation center
Kivuko cha nyerere

My take: hii ni too much.inachanganya watu hasa wageni.
 
Nyerere airport
Nyerere bridge
Nyerere road
Nyerere convection center
Nyerere leadership college
Nyerere national park
Nyerere hydroelectric power project
Mwalimu nyerere foundation center
Kivuko cha nyerere

My take: hii ni too much.inachanganya watu hasa wageni.
ni ulimbukeni tu
 
Uzi wenye mambo muhimu kwa ustawi wa Taifa letu hakuna wachangiaji.....ila weka mambo ya mabaharia utaona watakavyomiminika.
Kwani wewe hautoshi kuchangia hii mada?
naona una hasira sana na mabaharia bila shaka kuna baharia kakuchakaza halafu hajakupa hata thumni.
 
Kila siku kabla sijalala huwa siachi kumuombea Mh Rais John Pombe Joseph Magufuli, huyu atakuwa ni kiongozi aliyeacha alama, pamoja na upinzani mkubwa anaokutana nao kutoka nje na ndani ya chama chake ameendelea kusimamia kile anachikiamini na kuhakikisha hatoki ndani ya mstari .

Kipindi cha uchaguzi wengi waliamini atakuwa kiongozi mzuri lakini mashaka yao makubwa yalikuwa huenda akamezwa na mfumo dhalimu wa CCM, lakini kwa kipindi cha miaka 4 amedhihilisha pasipo shaka kwamba yeye ni zaidi ya mfumo.
 
Nyerere airport
Nyerere bridge
Nyerere road
Nyerere convection center
Nyerere leadership college
Nyerere national park
Nyerere hydroelectric power project
Mwalimu nyerere foundation center
Kivuko cha nyerere

My take: hii ni too much.inachanganya watu hasa wageni.
Basi tuiite piere liquid HPP
 
Nyerere airport
Nyerere bridge
Nyerere road
Nyerere convection center
Nyerere leadership college
Nyerere national park
Nyerere hydroelectric power project
Mwalimu nyerere foundation center
Kivuko cha nyerere

My take: hii ni too much.inachanganya watu hasa wageni.
Mv Nyerere

Shule za sek na pr ndo usiseme.

Nadhan angefufuka leo angekuwa na maoni tofauti....nafikiri tu
 
Nyerere airport
Nyerere bridge
Nyerere road
Nyerere convection center
Nyerere leadership college
Nyerere national park
Nyerere hydroelectric power project
Mwalimu nyerere foundation center
Kivuko cha nyerere

My take: hii ni too much.inachanganya watu hasa wageni.
Utekelezaji wa mradi ni safi

Ila hio jina la Nyerere linatumika Sana yaani imekuwa too much .

Nadhani hata yeye mwenyewe angekuwepo angeshangaa

Kwani nchi hii Shujaa ni Nyerere peke yake?

Hata hivyo nawapongeza kwa huo mradi tunahitaji umeme wa uhakika .

Hasa sisi wajasiriamali
 
Kwani nchi hii Shujaa ni Nyerere peke yake?
1. Sababu ya Magu kufanya hivyo ni kuwa, kuna watu walianza kuondoa alama zote alizoziacha Mwalimu (viwanda, umoja, usawa, mashirika n.k).

2. Magu anaweka jina la Nyerere kwenye miradi hiyo kwa kuwa Mwalimu ndiye aliyeanzisha mawazo ya miradi hiyo.
 
1. Sababu ya Magu kufanya hivyo ni kuwa, kuna watu walianza kuondoa alama zote alizoziacha Mwalimu (viwanda, umoja, usawa, mashirika n.k).

2. Magu anaweka jina la Nyerere kwenye miradi hiyo kwa kuwa Mwalimu ndiye aliyeanzisha mawazo ya miradi hiyo.
Nyerere hakuanzisha wazo LA mbuga ya selous.hakuanzisha pia wazo na jengo LA MNF.Na hata hivyo hatuwezi kusema kwa vile alileta wazo basi na jina LA mradi liwe lake.Hebu fikiria,watu wrote duniani walioleta mawazo ya miradi au vitu vingine,miradi hio ilipewa majina yao?

Kutumia jina lake so mbaya Kama ikiwa kwa kiasi tu. Lakini kwa spidi hii hata choo kitaitwa nyerere kwasababu tu ni yeye pia alisisitiza maswala ya afya.

Halafu tuwafikirie na watalii.Uchumi unategemea Sana utalii.Kwanini tuwachanganye wageni? Tunashindwa kubuni majina mengine yanayovutia?
 
Back
Top Bottom