Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi
Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati.
Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti.
Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mpango wa Serikali leo Aprili 9,2021 bungeni Jijini Dodoma
Waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini amesema Tanzania kuendelea kuwaza kuhusu madini yaliyopo ni kuchelewa huku akikosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.
Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya Maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.
"Kuwekeza katika umeme wa maji halafu unasema utaleta fedha, huko ni kujidanganya kwani umeme wa maji huchukua muda mrefu kuanza kutoa faida, huko wenzetu wamepita wanafanya mambo kisasa” amesema Profesa Muhongo.
Amesema dunia ya sasa imegeuka na madini mengi yanayotarajiwa Tanzania yapo lakini wengine wameelekeza kwenye dhahabu, Tanzanite na madini mengine ya zamani lakini wanaacha kuangalia madini mapya ambayo yataliingizia Taifa fedha nyingi.
NB: Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka sasa kila mtu CCM rangi yake ya zamani imeanza kurudi
Hivi kweli mmeanza kupinga project ya Rufiji baada ya Dkt. Magufuli kudondoka
CCM acheni unafiki