Profesa Makame Mbarawa anatushinda kumng'oa?

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,760
6,294
Habari Watanzania,

Binafsi nimeamini Prof. Mbarawa hafai kuwa mtumishi katika kiwango cha Uwaziri katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni waziri muoga, waziri picha tu. Ni Profesa aina ya le profeseri, yani yupo kama hayupo, na mambo mengi ya kuudhi na kuuza nchi hufanyika akiwa tuli kama kunyoa kichwa cha mwendawazimu.

Sasa hivi naamini hata Marehemu JPM alikuwa sahihi kumtimulia mbali pasi hata na kueleza sababu za kumtimua.

Ufafanuzi wa TPA kuhusu kuuzwa bandari ya Dar es Salaam (usiniambia eti kukodisha). Ukishakuwa umepewa sehemu kwa miaka 99, hapo umeuziwa, ndio uhalisia. Yani two good generation gonna live with the same contract and ownership, hata Mangugo alikuwa anafikiria sawasawa.

Kwa msioijua bandari ya Dar es Salaam, nawamegea kidogo.

Hao DP World wamepewa gati namba 5 mpaka 8.

Hayo ndiyo magati ambayo tangu enzi za Kikwete na JPM yamekuwa yakiendelezwa sana. Tena kwa gharama kubwa za serikali. Ambacho hakikuwa kikifanyika ni uwekaji wa mitambo ya kisasa tu, ila upanuzi na ujenzi umetumia fedha nyingi sana za serikali.

Mfano gati namba 5, 6, 7, 8 huku ndio asilimia 90 ya mizigo yote ya bandari ya Dsm imekuwa ikishushwa miaka yote.

Ishu ya kusema eti hakuna mkataba, ni uongo, iweje tujue wamepewa eneo hilo. Hicho ni nini?

Kama hawa DP World ni wakombozi wetu hivyo, kwanini wasipewe gati namba 1 hadi 4?!

Waendelee hapo, tuone ukongwe wao.

Miaka 99, akili au matope?

Tupige kura hapa Prof. Makame Mbarawa atupishe kwanza.
 
Mtafanya nini na mapengo yenu?
Mtamng'oa nani wakati hamkumpanda ninyi?

Kuna vitu hamtakuja kuviweza hivihivi ikiwa hamna vyombo vizuri vyakuwatetea, kama nchi inaenda mrama na jeshi lipo tu Moja kwa Moja mi binafsi lawama ntalipelekea lenyewe!

Humu mtakuwa keyboard warrior tu upige kura baada ya hapo unanguvu gani yakumuondosha?

Tujitafakari upya.
 
Madhara ya Sera za Mwendazake! Aliua Upinzani kwa Ukatili Mkubwa! Na yeye mwenyewe kafa!

Lakini ametuachia Bunge la ma-CCM lisilochaguliwa na Wananchi, ni Bunge lisilotetea Wananchi!

Kwa Bunge hili dhaifu ma-CCM yameamua kugawana Mbao! Bunge litajadiri na kupitisha Nchi kuuzwa!
 
Mbarawa unamuonea tu, kwani ndiye aliyeenda Dubai kupatana?

FB_IMG_1686074170313.jpg
 
Madhara ya Sera za Mwendazake! Aliua Upinzani kwa Ukatili Mkubwa! Na yeye mwenyewe kafa! Lakini ametuachia Bunge la ma-CCM lisilochaguliwa na Wananchi, ni Bunge lisilotetea Wananchi! Kwa Bunge hili dhaifu ma-CCM yameamua kugawana Mbao! Bunge litajadiri na kupitisha Nchi kuuzwa!
Upuuzi.
Wakati Kikwete anagawa gesi kwani wabunge wa upinzani hawakuwepo kututetea?

Wakati Kikwete anataka kugawa bagamoyo kwani hao wapinzani hawakuwepo bungeni? Kwa nini wasingetutetea wakati huo?

Ni ufinyu wa mawazo kumlaumu Magufuli (rip) kwa kosa linalofanywa na Samia. Let's be logical.
 
Mbalawa hawezi kufanya maamuzi ya kuuza bandari kwa waarabu,tusimpe lawama zisizo zake.

Tumedanganywa na kelele za simba na yanga halafu wakaona ndio wakati sahihi kupitisha mambo yao wakati bado tumepumbazika na matokeo ya Yanga kule Algeria.
 
Binafsi naunga mkono ubinafsishaji wa bandari.

Mnaopiga kelele ni kwamba ama ni wezi au mnatumika na wezi, ambao wana hofu ya kupoteza ugali wao.

Mbona hatuoni tija ya bandari miaka yote hii?
 
Back
Top Bottom