Profesa Kitila Mkumbo amchana Humphrey Polepole

hivi kuna watu bado wanaleta hoja ufisadi wa lowasa???mmefungua mpaka mahakama mbona hamumpeleki?acheni hadaa
 
Kama ni kweli haya ni maneno ya huyo Kitila Mkumbo basi na yeye namshangaa pia, kwani cheo cha H. Polepole ni kipi? Na kazi yake ni ipi, ndani ya CCM?

Tuambie wewe ana "cheo" gani na kazi yake ni ipi eti.....

Wewe fyatuka tu ukia - ashumu tu kuwa Prof. Kitila Mkumbo hajui au amesahau cheo cha boss wako huyo....
 
Chadema tokea wamsafishe fisadi Lowasa hawatakuja kuaminika tena mbele ya macho ya watanzania.

Watabaki kushabikiwa na malofa tu.
Ama kweli CCM haina mwenye akili, hivi hao malofa wanaoshabikia CHADEMA sio watanzania?
 
For what is what is worth kauli ya Polepole na serikari zina uhalali; ni uchonganishi kinacho sambazwa na wapinzani kwa wananchi kutumia wilaya chache zenye uhaba wa chakula na kulazimisha serikari itangaze state of national emergency. Wakati kuna sehemu kama Kigoma zina food surplus ni kitila asiye na hoja hapa Polepole kaja na facts wakati premise za Kitila ni za kufikiria mwenyewe tu.

 
Ndiyo taabu ya kuchukua mchezaji wa chandimu kumpeleka ligi kuu bila hata kuwa mahiri na walau mechi za mchangani!
Pole pole alistahili kujua chama chake kuanzia ngazi ya uchipukizi,shina,kata tarafa,wilaya kabla hajabebeshwa zigo zito la uenezi na itikadi asiyoimudu na inayompwaya!
Kuna wakati alisema atajikita zaidi upande wa ITIKADI kuliko UENEZI. Naona angeshikilia hapo. Aelimishe vijana nini maana ya "Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea" . Maneno haya ni machache kwa kutamka,lakini ni mapana sana ktk kujenga Taifa letu. Viongozi wengi wanayakwepa,vijana wa Chama chetu cha CCM ndiyo kabisaa,sina uhakika ni nini kimetokea! Itikadi ya CCM imejengeka na itaendelea kujengeka ndani ya siasa na Taifa lenye kufuata Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea unless otherwise tukubaliane vinginevyo. Mh, Polepole naomba ujikite huko zaidi ili utuunganishe tuwe wamoja. Andaa makala,vitabu,mihadhara,makongamanonk ili jamii ielimike na kuweza kuona kupambanua hoja au sera kati yetu na vyama mbadala.
 
Polepole ameanza kwa mguu wa kulia! Hana ujanja ule wa kukosoa akiwa ndani maana watamfukuza na kumpoteza!!! Inabidi ajifunze kuwa mwenezi na pia ajifunze uongo na fitina pia uchawi! Pale sio sehemu ya kumuweka mtu mwenye akili za kibinadamu.....lazima ushetani uwe nao!! Unafiki na uongo pia mchawi
 
Polepole atulize kichwa,sasa hivi amekuwa mtu wa kuropoka hadi anatia shaka kama sio Polepole yule wa bunge la katiba.

Tukiweka unafiki pembeni Nape alifanya vizuri sana kwenye nafasi hiyo aliyopo Polepole hivi sasa japo Nape hayupo smart kichwani kama Polepole ila anajua kucheza na maneno.
 
Back
Top Bottom