chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,400
- 24,980
Kijana wangu Humphrey Polepole anapaswa kuelewa kuwa kazi ya chini kabisa (minimum responsibility)ya upinzani katika nchi ya kidemokrasia ni kuikosoa na kuizodoa serikali na chama kilichopo madarakani.
Mengine yote yanajengwa katika msingi huu.Kwa upinzani kuisifia serikali ni hiari lakini sio wajibu.
Sasa yeye kama Katibu wa Uenezi wa chama tawala kuitisha press conference kwa lengo la kulaumu upinzani kwa sababu unaikosoa na kuizodoa serikali ni kosa la kimantiki.
Yeye ajikite kujenga hoja za kutetea chama na maamuzi na matendo ya serikali pale bila kuzuia upinzani kufanya kazi yake ya kuzodoa kwa sababu hawezi kuzuia.
Naamini kijana wetu huyu hatapoteza umahiri wa kujenga hoja kama tumjuavyo.
Bado naendelea kuamini kuwa katika teuzi ambazo Mwenyekiti na Rais Magufuli alipatia sana ni pamoja na kumteua Ndugu Polepole kwa nafasi hii.
Abaki tu katika mstari wa kujenga hoja.
My take : Huenda Polepole ametishwa mzigo unaomlemea. Siyo makosa yake bali ya aliyemtwisha.