batazoba
Member
- Apr 3, 2012
- 58
- 29
Aliyekuwa waziri wa ardhi na makazi wa Tanzania mh. Anna Tibaijuka anaitaka serikali kubadirisha utaratibu wa mbunge kutokuwa waziri ili wabunge waweze kuwahudumia wapiga kura wao badala ya kutumia muda mwingi kufanya kazi za serikali.
Wadau kama sio uchizi ni nn hiki au ndio kapagawa baada ya kufutwa kwake?
Hilo lilikuwemo ktk rasimu ya katiba mpya kwa wingi wao CCM wote walilipinga sasa imekuwaje baada ya kutolewa alione ni suala la msingi,hiyo inaonyesha kuwa CCM wengi wameburuzwa kumbe wana matakwa yao binafsi na sio kufuata matakwa ya chama hata kama huridhii.
Wadau kama sio uchizi ni nn hiki au ndio kapagawa baada ya kufutwa kwake?
Hilo lilikuwemo ktk rasimu ya katiba mpya kwa wingi wao CCM wote walilipinga sasa imekuwaje baada ya kutolewa alione ni suala la msingi,hiyo inaonyesha kuwa CCM wengi wameburuzwa kumbe wana matakwa yao binafsi na sio kufuata matakwa ya chama hata kama huridhii.
Aliyekuwa Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi Prof Anna Tibaijuka ameibuka na kusema Mbunge anapokuwa Waziri kama ilivyo sasa, anakuwa anafanya kazi za kuitetea Serikali badala ya kuisimamia.
Mbunge huyo wa jimbo la Muleta Kusini amesema pia anakosa nafasi ya kuwatumikia ipasavyo wananchi wa jimbo lake ambao ndio wamemchagua kuwasilisha matatizo yao Serikalini kwa ajili ya utatuzi.
Prof Tibaijuka ameibuka baada ya kuvuliwa wadhifa wake wa uwaziri na Rais Jakaya Kikwete kufuatia kupokea Bil 1.6 kutoka kwa James Rugemalira kinyume na masharti ya maadili kuhusu zawadi kwa mtumishi wa UMMA.
Prof Tibaijuka amesema sasa amerudi jimboni kwake Muleba Kusini kuwatumikia Wananchi. Amesema moja ya changamoto ambayo alikumbana nayo alipokuwa Waziri ni kuwa hakupata muda wa kutosha kuwatumikia Wananchi wa jimbo lake.
Muda mwingi alikuwa analazimika kufanya shughuli za Serikali badala ya kuisimamia Serikali ili itekeleze mahitaji ya wananchi wa jimbo lake kwa wakati. Hivyo kwa kuwa sasa yeye sio Waziri tena, basi anao muda wa kutosha kutatua kero za wananchi.
Ikumbukwe jambo hili la Mawaziri wasitokane na Wabunge lilipendekezwa kwenye rasimu ya pili ya katiba iliyokuwa imewasilishwa bungeni na iliyokuwa tume ya Katiba chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba.
Hata hivyo jambo hilo lilipingwa na bunge la katiba, na wengi waliopinga pendekezo hilo ni wabunge wa Chama cha Mapinduzi akiwemo Prof Anna Tibaijuka.
Sasa ni jambo la kushangaza kumuona Prof Tibaijuka leo anatoa kauli hiyo wakati alipokuwa kwenye bunge la katiba hakusema chochote na alipiga kura ya ndio vipengele vyote vya katiba iliyopendekezwa.