Prof. Sospeter Muhongo VS Dr. Peter Slaa 2015!!

Prof. Sospeter Muhongo VS Dr. Peter Slaa 2015!!

kwa hiyo kumbe wewe tunakubaliana kwamba tatizo ni watu(wanaochumia matumbo ) na si taasisi! basi tunatakiwa tushirikiane kila mtu kwa nafasi yake kupinga hao watu.......

Watu nia tatizo ila CHAMASUMU(JANI LA TUMBAKU/Chama Cha Mafisadi)ndio janga kuu,hiki ndo kiendeleza magonjwa DAWA ni kukiondoa na wenye anguvu hiyo ni watu hao hao,so tu-ungane na tuwakatae hao wachumia tumbo na chama chao.
 
Kwani Prof. Muhongo ameonesha nia ya kuutaka urais wa TZ?
Kama sivyo sidhani kama ni sahihi kumjadili kwa kulinganisha
na Dk. Slaa. Huu ni mtazamo wangu tu...
 
Watanzania hatuna viongozi ... wote wamekaa kidizaini. Hawana la maana ni mikelele tu isiyo na mpango wowote.
Na miananchi tulivyo wapumbavu tunashangilia chochote hata kama hakina maana kitakuwa na washabiki.

Mimi kati ya hao wawili simchagui yeyote yule kwa sababu hawana cha maana wanachofanya wanatupigia kelerle tu zisizo na mpango .... hawaeleweki wote hao!!
 
muhongo alichimbiwa biti na yule bibi spika wa bunge akatoa mimacho kwa woga ... teh teh teh
Ni hakika kabisa,bi.kiroboto alimpeleka puta pale bungeni. kwa mujibu wa CNN Dr.Slaa akilitumia jeshi la makamanda wa CHADEMA amesababisha ccm-(wafuga majangiri, mafisadi, wote wana magamba wakashindwa kuvuana) wabadilishe sekretarieti ya chama chao mara kadhaa.
Labda Prof. Muhongo alinganishwe na Lowassa, Mwakyembe, Magufuli,Membe, Sitta).Dr.Slaa alinganishwe na chama chote cha ccm hapo ndiyo utakuwa unamtendea haki Dr.Slaa.
 
Kwani Prof. Muhongo ameonesha nia ya kuutaka urais wa TZ?
Kama sivyo sidhani kama ni sahihi kumjadili kwa kulinganisha
na Dk. Slaa. Huu ni mtazamo wangu tu...
Bishop Hiluka angalau wewe umejenga hoja. Hata kama hajawahi kuutaka Urais haizuii wengine kufikiri kwamba anafaa kuwa Rais!!
 
Last edited by a moderator:
Tatizo la nchi sio mtu ni CCM hata slaa akiwa rais kupitia ccm hamna maendeleo ndi maana tunataka kuformat tuweke operating system mpya ambayo ni Chadema


............CCM haina tatizo hata kidogo, kajikundi kawababe fulani ndiyo wametengeneza style ya 10%. Tukipata kiongozi jasiri kama Sokoine (R.I.P), uchumi wetu utapaa kama rocket ! Na si lazima awe wa CHADEMA.
 
Ni sawa na Mawaziri wote wa Kikwete katika lipi. Kufikiri au kutenda?
Jadili sera za vyama na siyo watu!

Isitoshe Prof hajatangaza wala kuonyesha nia ya kuutaka urais!
 
Umeambiwa tatizo ni mfumo uliowekwa na CCM wa KULINDANA, KUKUMBATIA UFISADI. Hivyo hata Malaika Gabriel atoke mbinguni aje atawale Tanzania ndani ya MFUMO CCM he is doomed to fail. Kama tunataka tuendelea mbele ni kuondokana na MFUMO CCM, that means to VOTE OUT CCM, Tujaribu mfumo mwingine. Don't tell me kuna mtu atakayeweza kubadilisha MFUMO FISADI wa CCM akiwa ndani ya CCM, unless usema anataka kuiua CCM, kitu ambacho hakiwezakani.

Insanity is to repeat the same thing expecting different results. Kama kuna mtu hadi karne hii anajidanganya kwamba there is SINGLE MAN/WOMAN ndani ya CCM ataweza kubadilisha mfumo fisadi wa CCM akiwa ndani ya CCM, then that person is still LIVING IN STONE AGE.

In Summary kila aliyeko CCM NI TATIZO, Lakini si kila aliyeko CDM ni SULUHISHO.

KAMA HAJA KUELEWA akapumzike milele na giza lake.ubinadamu utakuwa ume-mshinda.
 
Jadili sera za vyama na siyo watu!

Isitoshe Prof hajatangaza wala kuonyesha nia ya kuutaka urais!
Chama ni dubwasha gani. Chama si watu na hao watu si ndiyo wanatunga hizo "sera" unazotaka "tuzijadili" bila kuwajadili watakaozitekeleza hizo sera? Mwalimu Nyerere, Ally Hassan Mwinyi, Ben Mkapa, na sasa Jakaya Kikwete wote wameshashika nafasi za Urais. Jee Urais umewafanya wafanane? Inakuwaje U-CCM au U-CHADEMA uwafanye watu wafanane?
 
  1. Tofauti yao ni nini kwenye msimamo kuhusu ufisadi? - Kamanda Zitto naona anapigania ufisadi kivitendo mfano kuacha kupokea ruzuku ilhali wengine wote wa CDM wanaendelea kuzitafuna.
  2. Hadhi yao kwenye kusimamia taasisi ya familia inatofautianaje? Slaa ana kashfa kibao za kifamilia
  3. Unawatofautishaje linapokuja suala la kuchambua dhana mbalimbali za kiuchumi? Dr Slaa hana elimu ya uchumi ni mtaalamu wa macho lakini Zitto ni mchumi na mwanasiasa
  4. Nani unamwamini zaidi kati yao na sababu zake ni zipi? Sababu ni vigezo vilivyotolewa
  5. unafikiri kama hawa wakiwa ni wagombea urais kupitia vyama vyao wanayajua matatizo ya wananchi? Wote wanayajua matatizo yetu
  6. Unaijua misimamo yao kuhusu utangamano (intergration) wa Afrika Mashariki? Wote wanaisupport EAC
.

Hebu tujaribu kuvitumia hivyo vigezo kuwalinganisha Zitto na Slaa. Nani atafaa zaidi 2015?

Nakuacha na tafakuri ya leo ili akili ichangamke kidogo:

“It is better to be hated for what you are than to be loved for what you are not.”
-Andre’ Gide
 
Unaamini kwamba kila aliyeko CCM ni tatizo na kila aliyeko CHADEMA ndiye suluhisho??

Tusiendelee kuwa wajinga kwa kdhani kuwa kuna mtu bora kwa nafasi ya Urais, Rais bora hutengenezwa na kuongozwa na katiba. Kila mtu anamapungufu ya kimtazamo ktk maeneo mbalimbali ya maisha na maendeleo hasa ukizingatia tunatoka ktk jamii zenye misingi tofauti na elimu tofauti. Jambo la msingi ni historia ya uadilifu na uchapakazi wake.
Lakini pia ikumbukwe 'Given the circumstances, one can be anything!' CCM ni chama chenye katiba funyu na malezi mabovu, viongozi wake ni walafi na chaguzi zake zimegubikwa na mizengwe yote isiyofaa, kamwe hatutegemei kupata kiongozi muadilifu kotoka chama hicho .... lakini pia misingi ya sera za nchi zinabebwa na ilani za chaguzi za chama badala ya katiba ya nchi, hivyo chama chenye uzoefu mbovu hakiwezi kuaminiwa kwa mabadiliko mazuri, wala kiongozi wake hawezi kuwa na vazi la haki
 
Hebu tujaribu kuvitumia hivyo vigezo kuwalinganisha Zitto na Slaa. Nani atafaa zaidi 2015?

Nakuacha na tafakuri ya leo ili akili ichangamke kidogo:

“It is better to be hated for what you are than to be loved for what you are not.”
-Andre’ Gide

Mbona umechakachua Post yangu??
 
Chama ni dubwasha gani. Chama si watu na hao watu si ndiyo wanatunga hizo "sera" unazotaka "tuzijadili" bila kuwajadili watakaozitekeleza hizo sera? Mwalimu Nyerere, Ally Hassan Mwinyi, Ben Mkapa, na sasa Jakaya Kikwete wote wameshashika nafasi za Urais. Jee Urais umewafanya wafanane? Inakuwaje U-CCM au U-CHADEMA uwafanye watu wafanane?
Usiwe mvivu kufikiri! Ndiyo sababu kuna sera, ilani, mpango kazi nk. Kiongozi bora ni yule anayezingatia malengo ya chama chake! Kwenda nje ya sera za chama kiongozi huyo anastahili kuwajibishwa na hafai! Kwa sababu hata siku moja hakuna atakachokamilisha.
 
kama tatizo sio watu ni ccm; hebu nambie ccm kama chama tatizo lake ni nini(ukiweka mbali watu ambao unasema si tatizo)?.....

Chama ndio chenye TATIZO kwa sera ya kukumbatia MAFISADI kwa faida ya kuficha aibu,hivyo hata awekwe malaika ni kazi bure.
 
Chama ndio chenye TATIZO kwa sera ya kukumbatia MAFISADI kwa faida ya kuficha aibu,hivyo hata awekwe malaika ni kazi bure......

kukumbatia ufisadi ni sera ya chama cha ccm? kwa sababu najua sera za vyama vyote zimeandikwa;hebu niambie hii iko kifungu gani na ni ya mwaka gani?
 
Kwa mfumo wa ccm ukimpa muhongo auongoze na mfumo wa chadema ukaweka jiwe tuh kwangu mimi ni tosha kabisa kuipigia kura chadema,mfumo wa ccm umeoza vibaya sana,muhongo kaingia juzi tu ona leo nayeye alivooza,,
 
Usiwe mvivu kufikiri! Ndiyo sababu kuna sera, ilani, mpango kazi nk. Kiongozi bora ni yule anayezingatia malengo ya chama chake! Kwenda nje ya sera za chama kiongozi huyo anastahili kuwajibishwa na hafai! Kwa sababu hata siku moja hakuna atakachokamilisha......

Kwani huwezi kujenga hoja bila ya kutumia lugha ngumu? Ni chama gani Tanzania viongozi wake wanafuata sera zake?
 
Back
Top Bottom