Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,238
Kuelekea uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kuna changamoto nyingi sana zinazolikabili taifa letu na zinazohitaji uongozi imara mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2015. Na kwa uhalisia inavyoonekana mchuano utakuwa kati ya CHADEMA na CCM. Kama CCM ikimsimamisha Profesa Sospeter Muhongo kuwa mgombea wake wa nafasi ya Urais na CHADEMA kama inavyotegemewa na wengi ikamsimamisha Dr. Willbroad Slaa kuwa mgombea wake kwa nafasi hiyo ya Urais unadhani mchuano wake utakuwaje?
Haya ni baadhi ya mambo ambayo tunaweza Kayatumia kuwapima Muhongo na Slaa kama ni watu wanaofaa au kutofaa kugombea Urais mwaka 2015.
- Tofauti yao ni nini kwenye msimamo kuhusu ufisadi?
- Hadhi yao kwenye kusimamia taasisi ya familia inatofautianaje?
- Unawatofautishaje linapokuja suala la kuchambua dhana mbalimbali za kiuchumi?
- Nani unamwamini zaidi kati yao na sababu zake ni zipi?
- unafikiri kama hawa wakiwa ni wagombea urais kupitia vyama vyao wanayajua matatizo ya wananchi?
- Unaijua misimamo yao kuhusu utangamano (intergration) wa Afrika Mashariki?
Haya ni baadhi ya mambo ambayo tunaweza Kayatumia kuwapima Muhongo na Slaa kama ni watu wanaofaa au kutofaa kugombea Urais mwaka 2015.