Waziri wa nishati na Madini Prof Dr Sospeter Muhongo, tunakuomba ujiudhulu nafasi uliyo nayo sababau umeshindwa kabisa kuiongoza wizara. Vurugu zilizotekea Mtwara kupelekea kuuwawa kwa wananchi na uharibu wa mali za serikali na raia ni ushahidi tosha unahusika. Kulazimisha Gas ije Dar es Salaam kufurahisha wakubwa zako (KInana na wingine) bila kujali wananchi wazawa wa Mtwara ni udhaifu wa kiuongozi. Hili suala kutizamwa kisiasa kuliko uhalisia utaigharimu serikali ya CCM. Tafadhali jiudhulu kuepusha madhara zaidi maana jina lako tayari limeingizwa kwenye historia Prof asiye na uwezo wa kufikiri na kuamua.
Mch Masa Safarini Mtwara
Mch Masa nadhani una malaria Au umetoroka Mirembe wewe. Dunia hii ya karne ya 21 wewe unadhani gesi itasafirishwa Kwa vibuyu Au ndoo. Nchi zilizoendelea zina mitandao ya mabomba ya kusafarisha gesi kutoka Kwenda sehemu mbalimbali Kwa ajili ya matumizi mbalimbali.