Homeboy
Unajua huu mkataba wa Gas ya Mtwara uko na siri kubwa sana! Kuna wajanja wamekula 10% gharama za ujenzi ni mara nne ya gharama halisi. Ningependa hiyo gas ifike mpaka kanda ya ziwa ili tusiendelee kukata miti kwa kuni za kupikia. Ila wanamtwara waone na wao wananufaikaje. Nilikuwa Geita ni mashimo tupu na uchafuzi wa mazingira ile dhahabu ndugu zetu kule hawaoni sababu yake. Kosa hilo lisiotokee Mtwara. Prof Muhongo afanye kazi kama msomi asipelekeshwe na wanasiasa. kuna siri kubwa sana na huu mradi kumbuka kuna watu wamegawana vitalu wanamtwara wanataka haribu dili. UMENISOMA WA KUKAYA
Mkuu wangu
Masanilo,
Kwanza hapa sitazungumzia hilo la 10% manake nafahamu hata kama mradi wote utabaki Mtwara bado hakuna guarantee kwamba hapatakuwa na 10%. Hapa nitaeleza juu ya gas kusafirishwa kuja Dar na endapo wana-Mtwara wanaweza kunufaika na gesi hiyo.
Awali ya yote, lazima tufahamu kwamba ONLY purified gas ndiyo inaweza kusafirishwa kwa pipelines. Gas in gas wells inakuwa in mixture form na purification inafanyika at or karibu kabisa na visima vya gesi. So, there's no way kwamba Gas inaweza kusafishwa/purified nje ya Mtwara! Hata Gas kutoka Songosongo inasafishwa kule kule kisiwani before the purified gas kuwa transported to Dar es salaam through the pipeline.
After purification kinachobaki ni pure gas for transport/use na byproduct. Hizi byproducts is not waste product bali ni raw materials ambazo zinaweza kutumika kwa matumizi ya vitu vingine kama vile utengenezaji wa mbolea. Kwahiyo, opportunity ya kwanza kwa wana-Mtwara ni hii byproduct ambayo inaweza kutumika kwa ujenzi wa viwanda vya mbolea.....na kama sikosei, nazani inatumika hadi katika utengenezaji wa saruji na bidhaa za plastic.
Mtwara kama Mtwara kuna favorable condition for investments hivyo sioni mwekezaji (say) kwenye sekta ya mbolea akaamua kusafirisha gas byproducts from Mtwara na kwenda kujenga kiwanda cha mbolea sehemu nyingine mbali na Mtwara! Na kama kumbukumbu zangu zipo sawa, nazani kule kuna mwekezaji ambae ana mpango wa kujenga the largest fertilizer factory kule kule Mtwara. Hivyo basi, kitu cha kwanza ambacho wana-Mtwara wanatakiwa kukipigania kwa nguvu zote ni kuhakikisha any investments as a results of natural gas byproducts zinafanyika Mtwara and nowhere else! Na yeyote atakayetaka kufanya nje ya Mtwara hatakuwa na sababu za msingi za kufannya hivyo!
Tukirudi kwenye suala la pipeline, hapa tunapaswa kukumbuka kwamba kinachotaka kujengwa is not just a pipeline but like a Highway Pipeline. Mabomba ya aina hii huwa yanakuwa na outlets. Hivyo basi, hapa kinachotakiwa kupiganiwa na wana-Mtwara ni kuhakikisha lazima kunakuwa na at least one outlet ndani ya Mtwara. Hii outlet ndiyo itakayotoa gesi kwa ajili ya matumizi ya Mtwara, domestically na kwenye viwanda. Uwepo wa hii outlet ndani ya Mtwara ndiyo itakayochochea investment ndani ya Mtwara yenyewe. So, wakati gas inakuja Dar es salaam bado kutakuwa na gas nyingine ndani ya Mtwara yenyewe. Kama alivyozungumza
rmashauri, Dar es salaam kuna mahitaji makubwa sana ya gas. Na hii sio kwamba ni kuipendelea Dar es salaam, bali hali yenyewe ipo hivyo na uletwaji wa Gas Dar es salaam una positive effect not only for wana-Dar es salaam but for the whole Tanzanian economy. Dar es salaam kuna consumption kubwa sana ya energy to the point kwamba, leo hii tukisema umeme wote unaotumika Dar es salaam uhamishiwe mikoani, basi mikoani hapatakuwa na shida tena ya umeme! Mimi nazani ukiondoa miji kama Mwanza na Arusha, si ajabu umeme unaotumika kwenye mikoa yote collectively hauwezi kufukia ule wa Dar es salaam! So, kui-diversify Dar es po salaam with energy sources, kutasaidia sana kuongeza availability of power/energy kwenye mikoa/miji mingine.
Vile vile kuna cku nilikuwa naongea na bwana mmoja, huyu ni senior official wa mamlaka ya bandari. Huyu bwana si mwanasiasa na wala hana affiliation yoyote na mambo ya siasa! Na kimsingi, tulikuwa tunaongelea jambo lingine kabisa ambalo wala halihusiani na masuala ya serikali au ya gesi. Katika maongezi yake aliniambia mpango wa mamlaka ya bandari kupanua bandari ya Mtwara! Sina hakika mpango huo utafanyika lini, lakini mpango kwenye vitabu vya bandari upo!
Nini lengo kuu la kupanua bandari ya Mtwara? Kimsingi kuna kiasi kikubwa sana cha gas kwenye pwani ya Lindi na Mtwara kiasi ambacho ni kingi mno even for the whole Tanzanian economy. So, mpango uliopo ni kufanya exportation ya Liquefied Natural Gas(LNG). So, jambo lingine ambalo wana-Mtwara wanatakiwa kulipigania wana-Mtwara ni hili la kuhakikisha kwamba LNG inakuwa exported just through Mtwara Habor!
Hata hivyo, bado katika hili sina shaka nalo sana coz' sioni ni namna gani Liquefaction Plant (plant to convert gas from gaseous to liquid form) for offshore gas available in Mtwara inaweza kujengwa sehemu nyingine mbali na Mtwara!! Vilevile hii gas ikishakuwa liquefied ni lazima iwe loaded kwenye special ships ambazo ni maalumu for transportation of LNG. So, ukiangalia hapa napo, sioni ni namna gani unaweza kukwepa uwezekano wa bandari ya Mtwara kuwa ndiyo loading terminal.
So, ukiangalia mambo yote hayo utagundua kwamba shughuli nyingi zitakazohusiana na gas zitafanyika Mtwara kwenyewe na challenge iliyopo ni kwa wana-Mtwara wenyewe kuangalia ni namna gani wanaweza ku-take advantage of gas economy/activities in the area.
c.c
THE BIG SHOW,
rmashauri,
JokaKuu,
EMT,
Invisible,
Gesi-Mtwara,
RevolutionaryTZ,
Fidel80,
Ibambasi,
Kobello,
Nambukwa