Jamani tuacheni unafiki, ukweli ubaki kuwa ukweli. Huyu jamaa Prof Muhongo sasa hivi ana mwaka mzima wizarani na hajafanya lolote kuhusu elimu kwa wana Mtwara na Lindi sasa kwa nini asiwajibike? 1 yr inatosha kuuelimisha umma. Ukweli ni kwamba Muhongo ni mzee wa sound, ni muongo sana kama lilivyo jina lake kwa sababu zifuatazo:
1. Mwaka jana wakati anawasilisha bajeti yake alitoa kauli za ulaghai na kuuhadaa umma kwamba kuna wabunge wanafanya biashara na Tanesco. Tume ya Bunge ilipoundwa ikabaini yeye na Katibu Mkuu wake Maswi wote walilidanganya Bunge kwa makusudi ili kulinda mikate yao! Ofcoz kwa kosa hilo walipaswa kuachia ngazi lakini wengi tunajua kwamba Serikali ilitumia nguvu nyingi kumrubuni Spika Makinda ili awapunguzie adhabu, hivyo akawapa onyo kinyume na matarajio ya wengi kwamba wangewajibishwa ili kuwa funzo kwa wanaoongopa ndani ya jumba takatifu.
2. Ni Prof Muhongo huyo huyo aliyetoa kauli ya kianaharakati kwamba Tanesco ilikuwa haihitaji mkopo wa kupambana na mgawo wa umeme isipokuwa tatizo lilikuwa kwa Menejimenti. lakini Hotuba ya Muhongo huyohuyo kwa sasa Uk 12 inakiri kutoa ruzuku kwa Tanesco ya mabilioni ya walipa kodi (zaidi ya bil 402 kwa mwaka mmoja tu tangu aingie madarakani). Fedha yote hii imetumika kununua mafuta za kuzalishia umeme. Hii inashangaza sana maana Ngeleja alikuwa akipigiwa kelele kwa kuomba fedha ya kununulia mafuta isiyofikia bil 50 lakini wafitini wake wakaona anachonga deal, sasa kwa ukweli huu nani aliyekuwa makini huyu Muhongo muongo au Ngeleja aliyetolewa kafara kwa wivu, unafiki na fitna za kisiasa?
3. Prof Muhongo na Maswi mwaka jana wakashirikiana kuvunja sheria ya manunuzi kwa kununua mafuta kutoka kampuni ya Puma kinyume na taratibu kwa kigezo cha uzalendo kumbe jamaa waliwekwa sawa, Wabunge walipotaka kuwawajibisha PM akawakingia kifua, ingawa taarifa ya CAG imewaumbua!
4. Pamoja na majigambo mengi aliyoingia nayo wizarani, Prof Muhongo na wasaidizi wake hawajafanya lolote jipya. Angalia hotuba yake, imejaa miradi aliyoianzisha Mr Megawati (Ngeleja). Jamaa hana jipya ila mbwembwe kibao!
5. Prof Muhongo na Naibu wake Simbachawene mwaka jana wakaihadaa dunia kwamba mgawo wa umeme ulikuwa unatengenezwa mezani. Kauli hiyo ililenga kujipatia umaarufu na kuwadhalilisha Ngeleja na Malima, lakini sasa kila mwenye akili timamu anajua kwamba Muhongo na Simbachawene ni waongo na walaghai waliobobea, wanameza matapishi yao. Mfano, mgao wa umeme waliotaka kuutumia kujipatia umaarufu umewaumbua kwa sababu wametumia zaidi ya bil 400 kununua mafuta wakati akina Ngeleja na Malima hawakuwahi kutufikisha huko! Madhara ya ulaghai wao umeifanya Serikali ishindwe kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa mwaka huu-mfano fedha zote zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya umeme vijijini kwa mwaka 2012/2013 zilipelekwa kununua mafuta ya umeme ili kumkinga Muhongo asiaibike kwa kauli zake.
Mwisho,
Ni jambo la kusikitisha kwamba viongozi waongo kama hawa wanafumbiwa macho, sijui Idara ya Usalama wako wapi kumshauri Rais, credibility ya Serikali inashushwa na hawa jamaa,sijui labda tusubiri tuone!