Mleta mada nadhani anapaswa kufanya upembuzi yakinifu. Yeye anataka kudandia hoja jujuu kujipatia yeye na chama chake umaarufu wa kisiasa. Nasema chama chake maana ametaja ccm kama chama cha mhongo. Pili atambue CHADEMA wanashabikia majimbo au kwa maneno mengine kanda na siyo mikoa au wilaya au vijiji kwa hiyo asidhani wala asitegemee ikichukua nchi 2015 basi gesi itatumika mtwara pekee.
Sasa nije niweke mezani nilichokipata baada ya utafiti mdogo sana. Hili swala wanasiasa wanalidandia tu juujuu lakini wenye ajenda ni wafanyabiashara waliozoea kijineemesha kwa udhaifu wetu sisi wananchi wa kuangalia vitu hapa usoni badala ya kuona mbali. Wafanyabiashara hao ni IPTL ambao kimsingi wanaamini kuwa gesi hiyo ikifika Dar es Salaam basi biashara yao ya kuilaghai TANESCO itakua imekufa. Na tutambue wazi hawa jamaa wanaingiza si chini ya bilioni 3 na kimsingi kinachotumika halali ni 2bilion tu. Wengine ni Symbion ambo hata sitaki kusema sana inajulikana wazi mradi waliourithi toka Richmond na kubarikiwa na Mama Clinton alivyokuja hapa. Wengine hao kina Agreco na wenzao ambao wanatambua wazi ujio wa gesi hiyo tayari ni faida kubwa kwa wananchi na ni hasara kubwa kwao.
Lazima ndugu zangu tuelewe kuwa Matajiri wa Madini, gesi, mafuta, unga, silaha, chemikali, kuuza binadamu na majambazi wa kimataifa wanamtandao mpana sana na wengine wanalindwa na nchi zao ambazo zina uwezo mkubwa wa kifedha na usalama wa taifa. Tukumbuke ya Sadam, Gadafi na wengineo si kwamba Marekani na mabeberu wengine wana uchungu nao bali wafanyabiashara wa marekani ndiyo wanaolindwa na nchi zao na kuhakikisha biashara inaleta faida kwa nchi husika. Mbinu zote chafu na nzuri hutumika katika kuhakikisha maslahi yao yanafikiwa kwa kiwango cha hali ya juu, tena hutumia wanasiasa mashuhuri, viongozi wa serikali, wanausalama kama TISS, polisi na hata majeshi. Hivi hatuoni filamu za kina jack chain na Blood Diamond nk hizi zote zina portray ya reality of what is going on in this world.
Hayo ni mawazo yangu. Usalama wa Taifa wanaweza kufuatilia kwa umakini na kupata ukweli wa hili.