Prof. Shivji Issa: Nipo nchi gani; baharini au barani?

Prof. Shivji Issa: Nipo nchi gani; baharini au barani?

Hawa wazee wanajitoa ufahamu, wenyewe wameiharibu Nchi kwa kujaza watoto na ndugu zao wasio na uwezo sehemu nyeti zinazoitaji watu makini na wenye vipaji husika kulipaisha Taifa . Wenye nchi yao kwa uhalisia wapo huku bench. Wengine wamekata tamaa wamekuwa walevi kwa sonona.
Kamjaza nani kwa mfano!?
 
Huyu alishapoteza mwelekeo toka baada ya kuvurugwa katiba mpya
 
Depression at its pick walahi
Antidepressants lazima apatiwe haraka walahi
Dawa ya uzeeeeeeee walahi
Elimu yako ni ya bei gani? Sijauliza kiwango kwani ingekuwa na kiwango stahiki usingekuwa unafanya kazi ya kuhukumu humu bali kujadili hoja kwa kiwango cha uelewa wako! Wewe huna uelewa wa kumchallenge prof. Shivji hata kidogo na hata anapopita utaogopa kulinganisha nyayo zako na zake kwani utaziogopa kama sikosei!
Msome tena na ujaribu kuwa na open mind ili umwelewe japo siamini kama una utashi huo.
Kuna hoja zikiletwa hapa na watoto wenzako changia kitoto kwani zinalandana na haiba yako! Lakini hizi za kina prof. Shivji zisome kwa tahadhari na uangalifu mkubwa kwani zinakuzidi uzito wa ubongo wako! Sijakuharibia siku japo nina uhakika usiku wa leo utakuwa mrefu sana kwako! Pole na jirekebishe!
 
Shivji anashangaa majambazi yanakuteka baadaye yankuejesha wakiwa wame kukabizi mobile phone ili uwatoe wasiwasi familia, wakati huohuo wanakuachia toyota 4 wheels drive, equipped with full military arsenal kama ak47, a numbers of short guns, GPS etc..
Ndio anauliza hawa ni majambazi ama majemadari?
 
Hayo ndio majibu kwa nini Professor yupo kimya, amechanganyikiwa hajui yupo wapi kwanza... kudadeki!! . Na bado Professor utachanganyikiwa sana sana. Nikujibu professor upo barani, kwenye nchi iliyopatizwa kwa moto.
 
Yani watanzania bhana!
Why do you always make a big deal out of nothing??

Kitu akikifanya mtu maarufu hata kama hakikua na maana mtakitafutia maana.

Hii ipo hata kwenye kazi mbovu za sanaa za wasanii maarufu

Ili mradi ameimba Fulani basi hata kama hakina maana au kina maana mbaya utaki support, it's foolishness
 
Prof hapa kaongea kwa tumia falsafa kama wewe sio critical au great thinker utatoka kapa.....
 
Wataalam hebu mtudadavulie alikuwa anamaanisha nini huyu msomi.View attachment 906151
Huyu anajigonga gongesha tujue yupo hopeless professor, tulishamtupa Kule alipoipinga rasimu ya warioba ya selikari tatu, pia aliyakana maandiko yake ya kitaaluma kuhusu muungano wa serikari tatu.

Laiti kama kungekuwa na sheria MTU akiyakana machapisho yake afutiwe uprof.huyu tungemwita Mr shivji
 
Majambazi au majemedari!!!! Wasiojulikana au wanaojulikana!!! Jibu sahihi ni lile linalofuata baada ya neno au
 
Nilidhani Tanzania hakuna uhuru wa kujieleza!

Sasa huyu babu Shivji kaandika hiyo mistari yake akiwa wapi? India?
Professor ameandika vitu vya kawaida tuu...ila sasa...watafsiri ndio shida...kila mtu kaja na lake...wala hajasema lolote la ajabu hapa...ila watu wameshaunganisha mistari wanayoijua...ukute mwenzenu ameandika quotes za kutoka kwenye 'hekaya za abunuasi' au esopo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom